Hivi ni kwanini tumeshindwa kujenga O'bey, Masaki, Ada Estate au Upanga nyingine?

Umemaliza, tufunge mjadala ili wenzetu waendelee kumsifu "mungu" wao ambaye ni mfano wa kuigwa duniani.
 
Serikali iingilie,mtu akitaka kununua na kujenga kitu lazima aombe permission na akionyesha hataleta madhara kwenye mipango mji ndio aruhusiwe...

Second, ni kuimpose stricter rules,kwa wanaodump uchafu iwe mtu mmoja au familia..walipishwe fines za kutosha
 
Ni kweli kuna sehemu nilienda hadi nikajiuliza kama kuna viongozi wa serikali, yaani sisi waafrica tuna upumbafu mwingi sana sijui tupoje aisee

nenda mbagala ukaone namna jenga uza walivyo jenga nyumba za hovyo..
 
Tofauti kati yetu na wenye miji iliyopangwa ni kuwa wakati wao miji inajengwa na taasisi sisi inajengwa na watu binafsi
 
Hata huko Masaki kuko hovyo, obey kunatia aibu Bora hata bunju kwa Sasa kuko vizuri kidogo
Nenda Gaborone tu pale uone tofauti. Unapita mitaa unaona ilivyopangwa vizuri. Makazi yanaeleweka. Sehemu ya makazi ni makazi na sehemu ya biashara ni biashara.

Ukipata barabarani Gaborone huoni mavibanda vibanda. Barabara ziko nyeupe na safi hadi miundombinu inapendeza.
Sie tumejenga fly-over Ubungo ila hata huoni uzuri wake. Pembeni tu na chini ni mavibanda ya machinga yamejazana hovyo hovyo.

Tunajenga njia sita sijui nane kimara hadi Kibaha ila hata haipendezi. Ni mavibanda tu ya machinga yamejaa pembeni. Sehemu za makazi unakuta mabiashara na sehemu za biashara ndo kumewekwa hoehae.

Nawaambia nchi hii ikitaka mabadiriko ya kweli na chanya hii CCM ni kuitoa kabisa madarakani
 
Wasomi wetu wa mipango miji wanachozingatia ni kupata gpa kubwa basi.
 
Moderators hivi huu uzi unastahili kuwa kwenye jukwaa la hoja mchanganyiko??? Wakati unawagusa wanasiasa wa nchi hii ambao ni policy makers???

Embu urudisheni jukwaa la siasa!
 
Waulize watu wa halmashauri. Watu hawana upeo wala maono. Ni moja ya sababu naunga mkono MAGU kutowaongezea mishahara wafanyakazi wa serikali -tena ikiwezekana wapunguziwe- hawa watu hawafanyi kazi zao.
Hawa watu ni ovyo kabisa sijafaham wanapangilia nini jamani kama kwa arusha hali ni mbaya kuna wengine hawana hata njia za kupita kurudi makwao pia kwanzia uhuru mpaka leo kuna viwanja havijahakikiwa wala kujulikana na huezi pangilia kitu usichokifaham kiukweli tz tupo tupo tu .....lakini tusiishie kulaumu nini kifanyike ?
 
Nchi yetu inahitaji mabadiliko makubwa ya kifikra na kiuongozi hata na mifumo ili wataalamu watumike effectively, huku bongo nyumba za makazi, hapo hapo biashara nyumba zimebanana hamna hata garden au miti kupo kupo tu hovyo, very shame, na Sasa hivi nchi nzima imekuwa takataka kila mahali vibanda vya machinga na maturubali kila sehemu zimekuwa soko waweza ingia bank pembeni ukakuta muuza vitunguu na nyanya inasikitisha Sana, jamani viongozi wenye dhamana tumieni vizuri nafasi zenu kuleta mabadiliko chanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…