Hivi ni kwanini tumeshindwa kujenga O'bey, Masaki, Ada Estate au Upanga nyingine?

Watabuni na kujenga Masaki na O’bay kwa mtaji gani wa uzoefu?
Mtu katoka bush, halafu ndio mkurugenzi wa mipango miji, unategemea nini hapo.
Hata huko Masaki, O’bay anakusikia tu, hajawahi kuishi huko, naye anakaa Bonyokwa!
 
In other words GPA ifanye ku include ubunifu/creativity...na pia wawe exposed na jinsi nchi nyingine zinavyotengeneza miji yao..
Sure my dear I wonder huku watu wamekumbatia GPA kuliko ubunifu, hata elimu kwa wenzetu ni very simple inayo encourage ubunifu na ku solve changamoto za jamii husika while huku kwetu tuna cremisha sijui Keynesian theory, Rostows development theory wakati applicability yake huku kwetu ni tofauti kabisa
 
Singida wanajitahidi kwa kuupanga mji,,tatizo wakazi wamekomaa na nyumba za 1947
 
Umeongea ukweli mtupu Tz ni Takataka,miji yetu ni hovyo nenda Harare uone mji ulivyopangika tunashindwa kwenda kujifunza kwa wenzetu?
 
Wacha watu wajitafutie chakula Mzee, wewe unaita uchafu mwenzio ndo anapokula na kuvaa sababu ya hivyo vibanda unvyoita uchafu.
 
Wacha watu wajitafutie chakula Mzee, wewe unaita uchafu mwenzio ndo anapokula na kuvaa sababu ya hivyo vibanda unvyoita uchafu.
Na nyie ndo mnaofanya hii nchi iwe ya kishenzi. Polee sana.

Soma mada kwa kutulia alafu ndo toa mawazo yako. Hakuna mtu anayepinga watu kujitafutia. Suala ni hao watu wapangiwe maeneo maalum yaliyojengwa vizuri na kisasa, yenye miundombinu Bora inayopendeza.

Tatizo CCM imewafanya mfikiri kuwa kuishi vizuri katika maeneo mazuri ni kama bahati tu kumbe ndo hivyo mnavyotakiwa kuishi.
 
Alafu cha kusikitisha kuna wataalam wanazalishwa kila mwaka na vyuo kama Ardhi University. Kuna maprofesa kabisa wa haya mambo ila ndo hivyo wanabaki kujisifu tu na PhD zao
 
Mtazamo wako ndo wenye changamoto, tunaishi vizuri tu. Mimi binafsi sikwaziki na kuwepo kwa vibanda kila mahali.
 
Idara ya ardhi, mipango miji haijielewi. Viwanja vinagawiwa bila ya kupimwa, na hakuna utaratibu wa nyumba za eneo au mtaa fulani ziwe vipi kimuonekano unaofanana au mpangilio.
 
Tilizoea kuishi maporini unategemea mambo ya planning ya miji tuijulie wapi haya mambo tuwaachie mabeberu wapange miji yao sisi tushazoea kukata pori tunajenga
Hiu ni Kweli mkuu,hapa niko na mdogo wangu tukicheza cheza cheza juu ya miti huku tukila matunda na asali na baadae tutaenda kuiba mahindi ya wanakijiji,na jua likipoa tunarudi zetu kulala huko mtini.
 
Kule kuna sewerage system, pia mpangilio wa nyumba ilikuwa mzuri, miti ilipandwa ikapendezesha maeneo yale.
Sidhani kama huko mbweni wamejenga sewerage system, au kuna vyoo na matanki ya maji machafu.
 
Kule kuna sewerage system, pia mpangilio wa nyumba ilikuwa mzuri, miti ilipandwa ikapendezesha maeneo yale.
Sidhani kama huko mbweni wamejenga sewerage system, au kuna vyoo na matanki ya maji machafu.
Hio ilikua enzi hizo siku hizi kule kumejaa baa za kutosha na maduka ya mangi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…