Hivi ni kwanini tunapenda kuitana "Mkuu"?

Hivi ni kwanini tunapenda kuitana "Mkuu"?

Inasaidia sana kuwajua wanaJF huku mtaani.. Maana mtu akiniambia "niaje Mkuu" automatically najua 'atakuwa mJF' huyu.
 
Nimekuwa msomaji mzuri wa comments za watu hapa JF, tusaidizane hili. Hivi ni kwanini JF watu huitana MKUU hasa wakati wa kuchangia kwenye threads?
 
Nimekua msomaji mzuri wa comments za watu hapa JF, tusaidizane hili. Hivi ni kwanini JF watu huitana MKUU hasa wakati wa kuchangia kwenye threads?
Mkuu Umewahi kusoma kitabu cha Allan Quarteman?
 
Ndio neno pendwa lenye mvuto wa pekee na lenye kuonyesha heshima kati ya member na member, hata kama pana tokea minyukano na tofauti za kihoja.... Pale mmoja anapo muita mwingine mkuu, tayari hushusha munkari na kulainisha ukali wa tofauti za wahusika.
Ngoja wengine waje wakujibu
 
Ahsante kwa jibu zuri Kiongozi
 
kupitia JF nimefanikiwa kuchomeka neno MKUU kwa wafanyakazi wenzangu ofisini na sasa tunaitana Mkuu hata boss hutu-address 'MKUU' hata vikaoni. ukweli ni kuwa JF ni darasa la waungwana japo kwa sasa nidhamu si kama ile miaka ya nyuma nikiwa msomaji kabla sijaanza kuchangia.
 
Ahahahhah..... Mleta mada pole sana. Hapa jf ni home of great thinkers kwa hiyo hata ukitafsiri kwa kiswahili ni nyumbani au makazi ya wafikiriaji wakubwa au wakuu wa fikra.
Kama wewe unaona jina mkuu au cheo cha ukuu hakikufai ni vizuri ukaomba kuondolewa kundini au jumba la wafikiriaji wakuu.
Pia fanya uchunguzi utajua kweli hapa wakuu wanaleta hoja na mawazo makuu au makubwa na mazito... Endelea kufuragia cheo cha ukuu japo daliki zinaonyesha kinakupwelepweta au kwa kiswahili kingine ukuu unakupwaya.
 
Back
Top Bottom