Naomba kujua hili.
Wanawapelekesha ,
Wanawatumikisha
Wanakaripia lakini wala hamlalamiki mnaona sawa tu ni kwanini, yaani tuseme tu wenye sura nyeupe , nyeusi wanawahanya sana.
Hata dada mweupe watu wanamuhanya.
Huwa shida nini? Au wao ni nuru nyie ni giza maana sio kiasi hicho.
Kuwaogopa au kujiona dhaifu mnyonge mbele ya mzungu,Hii hutokea bila hata mhusika kuamua, subconsciously,mtu mweusi amefanywa mtumwa,ukaja ukoloni, sasa hv kuna ukoloni Mambo Leo kwa miaka zaidi ya 200+, hii ina madhara kwenye Saikolojia, ukielimishwa, hii, Hari hupotea,
Nimefanya kazi, na wazungu kuanzia South Afrika mpaka US, kwanza wao wakikutana na, mwafrika,wanaamini wao ni Bora kwa kila kitu, na wewe mweusi inabidi utii Hilo,
Hii ni Hari ya kujiona Bora kuliko jamii nyingine, hata kwenye makabila ya ki Afrika, mfano wahaya, wachaga, nk hujiona wao ni Bora, wasomi sana, wana intelligence kubwa kuliko wengine,
Au, jinsi wakenya wakija bongo, hata kama wana elimu ndogo, watawababaisha wabongo wenye degree, na wabongo subconscious ly wanaamini wakenya wapo juu. Na wanaigeria wanajiona wapo juu ya wakenya!
Mitazamo, inaanzia kichwani,jinsi, unavyofikiri, madhara ya kutawaliwa yalitifunya tujione wanyonge Hari hii inatibika kwa elimu ya kujitambua tu.