Hivi ni kwanini wanaume mnaongelea sana maovu ya wanawake na kuyaacha ya kwenu?

Hivi ni kwanini wanaume mnaongelea sana maovu ya wanawake na kuyaacha ya kwenu?

Kwahiyo unakubali kwamba jamii inakosea kufanya hivyo??
nimesema vitabu vya Mungu vimemfeva sana mwanaume kuliko mwanamke na hata tukitenda dhambi tunahisi tunastahili kuwa tolerated, sijasema tumeruhusiwa kutenda dhambi.

kwa mfano kama huu mstari wa biblia huoni unamkandamiza mwanamke na si mwanaume? mtoto wa kiume hajaonekana kama anaweza akamtia unajisi babaake kwa kulala na wanawake wengi..

ndo mana nakwambia tumekua programmed na maandiko tangu utotoni kuwaona wanawake kama watu wa chini.View attachment 1208083
 
Eti kisa maandiko yamesema wao ni kichwa wafanye mauchafu eti wanawake wavumilie wao wakikosa wasamehewe hii jamii yetu bado inaishi zama za dark ages kila mtu anahtaji kutendewa sawa na usicho penda kutendewa wewe basi isimutendee mwenzako. Kuna watu wanantanyasika na hivi wenye uelewa mdogo wasio weza kutafakari maandiko ndo wanakuwa hawajielewi ka nyumbu. Napinga uonevu wowote Kwa binadamu yoyote hasa mwanamke, though kuna wanaume wanaoheshimu wanawake ka babangu na wengine matured nawapa sana kongole.
Well Said
 
Rekebisha kauli hapo uliposema mwanaume anajitungia sheria zake na mwanamke anafuata sheria za mwanaume kwahiyo zile sheria za Mungu zimewekwa zifuatwe na kina nani??

Hizo sheria zinatambulika kwa waislam na Wakristo ambao hawazidi bilion 4.

Waliobaki wote hawatambui hizo sheria na wanaongozwa na sheria za Wanaume zikiwepo hizo za Wakristo na Waislamu.
 
Hiyo ni perception yako ka Mimi ninavoamini utofauti wa mwanaume na mwanamke ni maumbile tu ya uzazi the rest wote ni sawa
Wow!! Nimependa sana mitazamo yako mwanadada.

Eti ni kwanini hapa Afrika tuna mabilionea wa kiwango cha dunia wawili tu wa kike wakati wa kiume wako 34?

Pia ni kwanini asilimia 98% ya technological innovation hapa duniani imefanywa na wanaume na sio wanawake ?

Pia Kwanini hiyo sanitary pad uliyoivaa inayofonza damu huko chini mgunduzi wake ni mwanaume na sio mwanamke?

Pia kwanini vitu kama epidural na contraceptive pills ambazo ni kwa ajili ya faida ya mwanamke vimevumbuliwa na mwanaume wala sio mwanamke mwenzenu?

Pia Kwanini ukitaka kujenga nyumba akili yako inakutuma umtafute Hassan, John au Isaya ndio anyanyue tofali na wala sio Esther, Aisha au Mariamu?

Pia kwanini gari yako ikipata mzinga ukienda gereji kuinyoosha lazima uwakute akina Deo, Michael na wala sio akina Joyce au Merry ndio wakunyoshee?

Pia kwanini unapotaka kuajiri mlinzi wa nyumba yako unaenda kuajiri akina Vidume na wala sio wanawake wenzio?

Pia kwanini kwenye matangazo mengi ya kazi huwa tunaona sana hii statement "women are highly encouraged" na sio "men are highly encouraged" ikiwa kama wote tuko sawa?

Pia kwanini kwenye ajari yoyote ile rescue team huwa wana focus kwanza na wanawake na watoto kisha ndio wanakuja wanaume?

....nina maswali mengi sana kufuatia hii kauli yako ngoja nipumzike kwanza
 
Nipe andiko linalowaruhusu wanaume kutenda dhambi
Mimi nadhani mleta uzi Kuna kitu kaamua kujisahaulisha bahati mbaya Kama si makusudi,ukubwa wa mwanamme sio wa kujadili Bali ni qadar aliyoiweka Mungu,ambayo haitabatilika kamwe mpaka kuisha kwa dunia.Vitabu vya Mungu vinatuambia kuwa jumla ya mitume na manabii wa Mungu ni 124000,na wote hao walikuwa ni wanaume,mtoa mada amewahi kujiuliza kwa nini hao wote wawe wanaume tu bila ya mwanamke hata mmoja je Mungu alisahau?je wanawake hawakuwepo??na hata tukija kwenye maisha ya kawaida ya kila siku kati ya mke na mme,ni wapi ambapo mwanamke hutenda zaidi ya kutendwa?mtoa mada anatakiwa afute kauli yake na atuombe radhi wanaume.
 
Nionyeshe sehemu ambapo kuna "men empowerment" katika jamii yoyote, sehemu ambayo kuna "kama mwanamke anaweza, basi mwanaume anaweza pia", Innovations nyingi, go to moon and come back, ni akina Gagarin, Neil Armstrong na sio akina cariha, its just nature...you can do nothing to beat nature.

Kwenye maovu hapo no one is above the other, hakuna mwenye authority ya kutenda au kumtendea mwenzake uovu. But in terms of superiority, try another millennium, not this one!!!
Wewe wasema wanaume wamegundua na kusahau kuwa wanawake hawakuruhusiwa kwenda shule kabisa wala jambo lolote ulitaka wapate wape hyo platform yakufanya hizo gunduzi zao kama hawakuruhusiwa, hyo Armstrong kwenda mwezini kwanza ni tukio lakutengenezwa everything was staged by USA. Mabadiliko Kwa wanawake yalianza baada ya vita vya pili duniani, so ukisema wanawake hawakufanya kitu si kweli, mbona kuna magenious wakubwa tu hata tukio la juzi kugundua black alikuwa ni mdada mbinti mdogo aliweza kunasa.

Nasema jinsia yoyote ikipewa platform nzuri inaweza Fanya mambo makubwa mno.
 
Umeongea kama vile the real Ariana Grande anavyotiaga huruma... 🙂 anyways Kuna mambo yanasikitisha sana...

Tatizo bindamu wa siku hizi ni wabishi sana...

Kingine mpaka sisi wanaume tunaawangushia lawana nyingi wanawke sababu Eve kwenye bustani ya Eden tayari alisha mess up... kwa hivyo, hiyo mentally inaendelea vizazi kwa vizazi...

Cc: mahondaw
 
Ukiona mtu anatafuta justification ya jinsia yake basi ujue hana uhakika na jinsia yake.
Kwani nani kasema nyie ni wanawake?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Na Mwanamke anayefanya Abortion ni sawa na Mwanaume anayepiga punyeto. Wote wauaji.
Abortion ni kitendo cha kutoa mimba, na mimba ni pale tu mbegu za kiume zinapokutana na mayai ya kike sasa mwanaume anaejichua anafanyaje abortion au huo uuaji angali mbegu zake zinakua hazijakutana na mayai ya mwanamke
 
Kufikiria jambo Kwa mapana zaidi Kwa kuangalia Kwa muktadha tofauti wa faida na hasara. In short ni Ku go beyond something. I think umenielewa.
Safi sana,nakupa mfano mmoja tu ili unionyshe namna gani unaweza kufikiria nje ya box. Japo uko nje ya mada.

Hivi unaweza kufijiria nje ya box juu ya jambo la haki sawa na kufanana kwa haki ?
 
Wow!! Nimependa sana mitazamo yako mwanadada.

Eti ni kwanini hapa Afrika tuna mabilionea wa kiwango cha dunia wawili tu wa kike wakati wa kiume wako 34?

Pia ni kwanini asilimia 98% ya technological innovation hapa duniani imefanywa na wanaume na sio wanawake ?

Pia Kwanini hiyo sanitary pad uliyoivaa inayofonza damu huko chini mgunduzi wake ni mwanaume na sio mwanamke?

Pia kwanini vitu kama epidural na contraceptive pills ambazo ni kwa ajili ya faida ya mwanamke vimevumbuliwa na mwanaume wala sio mwanamke mwenzenu?

Pia Kwanini ukitaka kujenga nyumba akili yako inakutuma umtafute Hassan, John au Isaya ndio anyanyue tofali na wala sio Esther, Aisha au Mariamu?

Pia kwanini gari yako ikipata mzinga ukienda gereji kuinyoosha lazima uwakute akina Deo, Michael na wala sio akina Joyce au Merry ndio wakunyoshee?

Pia kwanini unapotaka kuajiri mlinzi wa nyumba yako unaenda kuajiri akina Vidume na wala sio wanawake wenzio?

Pia kwanini kwenye matangazo mengi ya kazi huwa tunaona sana hii statement "women are highly encouraged" na sio "men are highly encouraged" ikiwa kama wote tuko sawa?

Pia kwanini kwenye ajari yoyote ile rescue team huwa wana focus kwanza na wanawake na watoto kisha ndio wanakuja wanaume?

....nina maswali mengi sana kufuatia hii kauli yako ngoja nipumzike kwanza
Hahahaha!!! Mkuu atakuuliza wewe umegundua nini,?
 
Kushindwa kuyatafakari na kuyaelewa maandiko vzur n dhahiri kuwa yatakupoteza kabisa, mimi ni mwanaume ila nmeona madhara ya manyanyaso kwa wanawake maana sio kwa wao tu hata kwa watoto inawaathiri sana ila wengi hawalioni hili, mwanaume sio kuwa hivi kama mwanamke wako hakuheshim kwa kumfanyia mema unadhani atakuheshim ukimfanyia mabaya? Wanawake wanateseka sana na waliowahi kupitia hali hizi watakubaliana na mimi.
Inatia moyo kuona kuwa kuna wanaume wanatambua thamani ya wanawake kwenye hii jamii iliyopigwa upofu na mfumo dume na kusingizia kuwa kila kitu tunachofanya wanawake ni kutaka haki sawa hongereni na endeleeni na moyo huo huo
 
Back
Top Bottom