Habari za usiku huu wana jukwaa, kabla ya yote naomba kwanza niwasihi sana wale wavivu wa kusoma nyuzi ndefu kwamba huu uzi tafadhali kabla hamjatoa comments zozote naombeni muusome wote kama ulivyo kuanzia mwanzo hadi mwisho halafu ndiyo mtoe comments maana kuna watu wana tabia ya kukurupuka kuchangia vitu ambavyo tayari vimeshafafanuliwa kwenye uzi.
Kama kichwa cha mada kinavyojieleza, leo nataka niongee na wanaume wanaoongelea sana maovu ya wanawake na kuyaacha ya kwao kana kwamba wanaume hawakosei kwenye jamii wakati maovu yote yanayofanywa na wanawake ni sawa tu na maovu yote yanayofanywa na wanaume lakini kabla sijaendelea naomba niorodheshe kwanza maovu yanayofanywa na wanawake na jinsi yanavyoendana na maovu yanayofanywa na wanaume.
1. Wanawake wanaochepuka wanaendana na Wanaume wanaochepuka
2. Wanawake wanaozalishwa bila ndoa/nje ya ndoa wanaendana na Wanaume wanaozalisha bila ndoa/nje ya ndoa
3. Wanawake wanaojiuza wanaendana na Wanaume wanaowanunua
4. Wanawake wasagaji wanaendana na Wanaume mashoga
5. Wanawake wanaopenda kutembea na waume za watu wanaendana na Wanaume wanaopenda kutembea na wake za watu
6. Wanawake wanaopenda kutoka na mijibaba alias sugardaddies kwa ajili ya pesa wanaendana na Wanaume wanaopenda kutoka na mijimama alias sugarmummies kwa ajili ya pesa
7. Wanawake waliopo kwenye mahusiano kwa sababu ya pesa tu wanaendana na Wanaume waliopo kwenye mahusiano kwa sababu ya mbunye tu
8. Wanawake wanaopenda kuhudumiwa (kupewa pesa, kununuliwa vitu et al) na wapenzi wao wanaendana na Wanaume wanaopenda kulelewa (kupikiwa, kufuliwa et al) na wapenzi wao
9. Wanawake wasio na utii kwa waume zao wanaendana na Wanaume wasio na upendo kwa wake zao
10. Wanawake wanaowaacha wanaume waliowasomesha wanaendana na Wanaume wanaowaacha wanawake walioanza nao kwenye umasikini
Hayo ni machache mengine mnaweza kuongezea ila nimeona nijikite zaidi kwenye maovu yanayohusiana na ngono kwa sababu ndiyo janga kubwa kwenye jamii na nilitaka niwaoneshe ni namna gani jinsia zote zina maovu yake kwenye jamii, sasa hapa najua wapo watu watakaoleta habari za kutaka usawa sijui ushindani sikilizeni niwaambie, wanawake na wanaume tutatofautiana kote lakini siyo kwenye uovu yaani tutatofautiana kwenye jinsia, nafasi na majukumu lakini tofauti zote hizo siyo sababu ya wanaume kufanya maovu vile wanavyojisikia eti kwa sababu tu wao ndiyo wako juu ya wanawake
Wapo wengine watasema eti wanaongelea sana maovu ya wanawake kwa sababu wanawake ndiyo wanaopata madhara kuliko wanaume kwamba wanaume wao linapokuja kwenye swala la mahusiano ya kimapenzi hawana cha kupoteza kabisa ila niwaambie tu kuwa bado hiyo siyo sababu ya wanaume kufanya maovu vile wanavyojisikia eti ili tu kuwakomoa wanawake sasa mbona na magonjwa ya zinaa nayo hayaangalii jinsia na yanaua wote wanawake na wanaume kwa mtindo ule ule??
Halafu pia kinachonishangaza kama kweli wanaume hamna cha kupoteza kwenye mapenzi kwanini ninyi ndiyo mnaoongoza kwa kuyalalamikia na kuyaongelea maovu ya wanawake humu mitandaoni na mitaani kila siku?? Kuna mmoja alisema eti mnafanya hivyo kwa lengo la kutusaidia sasa kama kweli mngekuwa mna nia ya kuwasaidia hao wanawake wenye hayo maovu kwanini muishie kuongea kwa mdomo tu na siyo kufanya kwa vitendo??
Eti unakuta mwanaume anasema "kuna demu jana nilimtongoza akakubali muda ule ule na akanipa mzigo muda ule ule" halafu anamalizia kwa kusema "daah wanawake wa siku hizi mnajirahisisha sana acheni umalaya la sivyo wanaume tutaendelea kupiga na kusepa au kuzalisha na kuacha" sasa mwanaume kama huyu unamuona tu ni jinsi gani alivyo mnafiki yaani anajifanya kusikitishwa na wimbi la wadada kujirahisisha wakati huo huo yeye ndiye kinara wa kuwatongoza hao wadada ili wajirahisishe sasa kama kweli huyu mwanaume angekuwa hapendi wanawake wajirahisishe kwanini asiache kuwatongoza na kuwaomba mizigo kama hana nia nao??
Namaanisha kama wanaume mna nia ya kutusaidia wanawake na mmeona kwa maneno haisaidii kwanini msifanye kwa vitendo kwa kuacha hayo mambo yanayowafanya wanawake wajirahisishe kwenu?? Halafu wanaume wengi utasikia wanasema "kwanini mwanamke ukitongozwa ukubali" badala ya kuuliza "kwanini mwanaume anatongoza pasipo na nia ya dhati" yaani wanalazimisha ionekane kama mwanaume kutongoza siyo kosa ila mwanamke kukubali ndiyo kosa wakati actually kinachoanza ni kutongoza halafu kinachofuata ndiyo kukubali au kukataa hivyo lazima tukubali kuwa mwanaume anayetongoza na mwanamke anayekubali wote wana makosa na haya yote ni kutokana na tamaduni kandamizi zilizoanzishwa na mababu zetu enzi hizo bibi zetu wakiwa hawana sauti kwenye jamii hivyo walitupiwa mizigo yote na walilazimishwa kuikubali watake wasitake nasikitika kusema kuwa mamlaka ambayo wanaume walipewa na Mungu juu ya wanawake babu zetu waliyatumia vibaya kwa bibi zetu yaani waliyatumia kuwakandamiza badala ya kuwalinda
Kitendo cha kulazimisha kwamba mwanaume akitenda dhambi ni sawa ila mwanamke akitenda dhambi ni kosa ni kinyume hata na maandiko kwa sisi tunaoamini katika Mungu na Dini yaani jamii yetu imejenga mitazamo ya hovyo inayochagizwa na mfumo dume kwamba eti maovu ya mwanaume hayatakiwi kuhojiwa wala kurekebishwa bali maovu ya mwanamke ndiyo yanatakiwa kuhojiwa na kurekebishwa halafu wanalazimisha kwamba eti ni Mungu ndiyo ametaka hivyo ni mungu gani huyo aliyesema wanaume mtende dhambi mnavyojisikia eti ili tu mjitofautishe na wanawake na muonekane mko juu ya wanawake?? Ukweli ni kwamba tofauti kati ya mwanamke na mwanaume haipo kwenye dhambi hata siku moja yaani imefikia hatua wanaume wanajisifia umalaya na tena wanakataa kabisa eti mwanaume haitwi malaya bali kidume ukiuliza hiyo ni kwa mujibu wa nani hawana majibu wanakuja na mapovu!!
Kama kila jinsia imeshindwa kubadilika kwa nafasi yake na kusubiria eti jinsia nyingine ndiyo ianze kubadilika halafu nayo ndiyo itafuata basi niwasihi tu tuache kusubiri meli kwenye uwanja wa ndege au embe chini ya mkorosho mimi naona ifike pahala jamii iache uongo na unafiki kama tumeamua kukemea maovu tukemee kwa jinsia zote na kama tumeamua kuacha yaendelee tuache kwa jinsia zote after all wanaume si hamna cha kupoteza bwana so why mjihangaishe?? Ninyi endeleeni kupiga na kusepa au kuzalisha na kuacha halafu tutaona mwisho wake maana hata hivyo pamoja na malalamiko yote haya ya wanaume kwa wanawake naona ni kama vile mnajaribu kudeki bahari au kufagia jangwa tu!!
Kwa kuhitimisha naomba niseme tu kuwa hiki nilichokiandika ni robo tu ya nilichonacho ila kwa sasa naomba niishie hapa lakini bado nina mengi ya kuandika hapa sitayamaliza ila nitajaribu kuyajibu kwenye comments kutegemeana na maoni ya wadau japo najua nitaoga mapovu ya kutosha hasa kutoka kwa jinsia ya kiume lakini sitajali nayakaribisha ila wale wazee wa kukisia maisha ya watu wale wa "wewe utakuwa na stress za wanaume siyo bure" au wale wa "wewe unapenda kujilinganisha na wanaume" maana wenzetu mkiguswa kidogo tu mnakimbilia kusema wanawake tunataka usawa au ushindani na wanaume utafikiri labda wanaume mna kitu cha ziada mmependelewa nacho yaani labda wenzetu hamfi mnapaa mbinguni moja kwa moja kama mlivyo na ingekuwa hivyo mbona ningebadili jinsia kabisa niwe mwanaume ili nisife ila tofauti na hapo sijaona cha kunifanya nitake kujilinganisha na mwanaume maana hapa duniani kinaogopwa kifo tu kwa sababu hakikwepeki ila mengine yote yanakwepeka tu na tunayoweza kupambana nayo tunapambana nayo kikubwa uhai sasa leo naomba mje na hoja tafadhali hizo kauli zenu za ushindani sijui usawa siyo hoja bali ni mihemko tu
Nipo....