Hivi ni kwanini wanaume mnaongelea sana maovu ya wanawake na kuyaacha ya kwenu?

Hivi ni kwanini wanaume mnaongelea sana maovu ya wanawake na kuyaacha ya kwenu?

Hiyo ni perception yako ka Mimi ninavoamini utofauti wa mwanaume na mwanamke ni maumbile tu ya uzazi the rest wote ni sawa
Hiyo ni fact, ilifanyiwa research miaka mingi sana. Proved that a woman is inferior to a man in many ways, many ways...
 
Na ndio mtu anapotumia biblia vibaya kujitetea anatoka kwenye context ya kiuhalisia, mie nimegrow as christian tangu utoto, nimeona wazazi, uncles wana wake mbona hawajibehave kuonea mwingine hasa mwanamke, my bibi ndo kabisa hakuwaga na tabia za kuwafundisha wanawe wakiume jinsi ya kuishi na wake Ali mind business tena ukiwa mkubwa chukua mji wako na mkeo.

So hyo ya kusema naweza mfundisha mwanangu jinsi ya kuishi na wake nakosea nitamfundisha misingi hafu usifikiri mambo ya 60&70s ukiapply kwenye nahusiano ya sasa ita work up ni big no kila zama na kitabu chake nabii tusicremishe maisha, mambo yamebadilika mno, inabidi kuwalea watoto kwenye misingi mizuri ya haki, utu, na heshima na sio kuonea wengine then kimbilia maandiko eti mwanamke dhaifu.

Mbona sikuhizi wanawake wanachapa kazi, kulea na kuzaa nyie wanaume mumebakiwa na nini zaidi ya daily kulalamika wanawake hawasikii.
sasa hapo hapo unasema mtu anatumia biblia vibaya, hapohapo unasema biblia imepitwa na wakati kana kwamba sio tena swala la kutumia biblia vibaya ni swala la wakati.
anyway nimalizie tu kwa kusema tumekuwa programmed kubehave this way. sina la ziada hapo.
 
Hamhitaji vyama lakini ndo mnapuputika sana kuliko wanawake nyie mumesahaulika sana matokeo yake mumeshaanza kubaki nyuma mambo mengi, yani sikuhizi mumekuwa magoigoi, after 10 to 20 years mtaanza kulia lia it will be too late
Unazungumzia kusahaulika kwenye nini hasa? Maana inawezekana tunazungumzia nyanja tofauti..
 
Kushindwa kuyatafakari na kuyaelewa maandiko vzur n dhahiri kuwa yatakupoteza kabisa, mimi ni mwanaume ila nmeona madhara ya manyanyaso kwa wanawake maana sio kwa wao tu hata kwa watoto inawaathiri sana ila wengi hawalioni hili, mwanaume sio kuwa hivi kama mwanamke wako hakuheshim kwa kumfanyia mema unadhani atakuheshim ukimfanyia mabaya? Wanawake wanateseka sana na waliowahi kupitia hali hizi watakubaliana na mimi.
Wewe ni mpumbavu.
Hao wanao nyanyasika si wajitoe kwenye hayo manyanyaso.hamjakatazwa kuishi mnavyotaka ndomana mnatembea uchi tunawanunua kama nyanya sikoni.
Wewe sio mwanaume utakua na jinsia mbili.
Masaidie mkeo kubeba mimba ili tuwe sawa.
 
Binadamu ni mfano wa Mungu na siyo wanyama na wala hatukuagizwa tufuate maisha ya wanyama bali tumewekewa sheria zetu sisi kama binadamu hivyo usijilinganishe na wanyama hata siku moja binadamu tuna maisha baada ya kifo ila wanyama hawana sasa kama hadi hapo bado haujaona tofauti kubwa kati ya wanyama na binadamu basi utakuwa na tatizo mahali

Wewe ndio unatatizo mahali. Unapoambiwa binadamu ni mfano wa Mungu unajua ni nini kinazungumziwa.

Embu nenda kwa Magombo ya Suleiman utaelewa mimi na wewe nani mwenye matatizo.
 
sasa hapo hapo unasema mtu anatumia biblia vibaya, hapohapo unasema biblia imepitwa na wakati kana kwamba sio tena swala la kutumia biblia vibaya ni swala la wakati.
anyway nimalizie tu kwa kusema tumekuwa programmed kubehave this way. sina la ziada hapo.
Kumbe na wewe umeng'amua hiyo cognitive dissonance....
 
Habari za usiku huu wana jukwaa, kabla ya yote naomba kwanza niwasihi sana wale wavivu wa kusoma nyuzi ndefu kwamba huu uzi tafadhali kabla hamjatoa comments zozote naombeni muusome wote kama ulivyo kuanzia mwanzo hadi mwisho halafu ndiyo mtoe comments maana kuna watu wana tabia ya kukurupuka kuchangia vitu ambavyo tayari vimeshafafanuliwa kwenye uzi.

Kama kichwa cha mada kinavyojieleza, leo nataka niongee na wanaume wanaoongelea sana maovu ya wanawake na kuyaacha ya kwao kana kwamba wanaume hawakosei kwenye jamii wakati maovu yote yanayofanywa na wanawake ni sawa tu na maovu yote yanayofanywa na wanaume lakini kabla sijaendelea naomba niorodheshe kwanza maovu yanayofanywa na wanawake na jinsi yanavyoendana na maovu yanayofanywa na wanaume.

1. Wanawake wanaochepuka wanaendana na Wanaume wanaochepuka

2. Wanawake wanaozalishwa bila ndoa/nje ya ndoa wanaendana na Wanaume wanaozalisha bila ndoa/nje ya ndoa

3. Wanawake wanaojiuza wanaendana na Wanaume wanaowanunua

4. Wanawake wasagaji wanaendana na Wanaume mashoga

5. Wanawake wanaopenda kutembea na waume za watu wanaendana na Wanaume wanaopenda kutembea na wake za watu

6. Wanawake wanaopenda kutoka na mijibaba alias sugardaddies kwa ajili ya pesa wanaendana na Wanaume wanaopenda kutoka na mijimama alias sugarmummies kwa ajili ya pesa

7. Wanawake waliopo kwenye mahusiano kwa sababu ya pesa tu wanaendana na Wanaume waliopo kwenye mahusiano kwa sababu ya mbunye tu

8. Wanawake wanaopenda kuhudumiwa (kupewa pesa, kununuliwa vitu et al) na wapenzi wao wanaendana na Wanaume wanaopenda kulelewa (kupikiwa, kufuliwa et al) na wapenzi wao

9. Wanawake wasio na utii kwa waume zao wanaendana na Wanaume wasio na upendo kwa wake zao

10. Wanawake wanaowaacha wanaume waliowasomesha wanaendana na Wanaume wanaowaacha wanawake walioanza nao kwenye umasikini

Hayo ni machache mengine mnaweza kuongezea ila nimeona nijikite zaidi kwenye maovu yanayohusiana na ngono kwa sababu ndiyo janga kubwa kwenye jamii na nilitaka niwaoneshe ni namna gani jinsia zote zina maovu yake kwenye jamii, sasa hapa najua wapo watu watakaoleta habari za kutaka usawa sijui ushindani sikilizeni niwaambie, wanawake na wanaume tutatofautiana kote lakini siyo kwenye uovu yaani tutatofautiana kwenye jinsia, nafasi na majukumu lakini tofauti zote hizo siyo sababu ya wanaume kufanya maovu vile wanavyojisikia eti kwa sababu tu wao ndiyo wako juu ya wanawake

Wapo wengine watasema eti wanaongelea sana maovu ya wanawake kwa sababu wanawake ndiyo wanaopata madhara kuliko wanaume kwamba wanaume wao linapokuja kwenye swala la mahusiano ya kimapenzi hawana cha kupoteza kabisa ila niwaambie tu kuwa bado hiyo siyo sababu ya wanaume kufanya maovu vile wanavyojisikia eti ili tu kuwakomoa wanawake sasa mbona na magonjwa ya zinaa nayo hayaangalii jinsia na yanaua wote wanawake na wanaume kwa mtindo ule ule??

Halafu pia kinachonishangaza kama kweli wanaume hamna cha kupoteza kwenye mapenzi kwanini ninyi ndiyo mnaoongoza kwa kuyalalamikia na kuyaongelea maovu ya wanawake humu mitandaoni na mitaani kila siku?? Kuna mmoja alisema eti mnafanya hivyo kwa lengo la kutusaidia sasa kama kweli mngekuwa mna nia ya kuwasaidia hao wanawake wenye hayo maovu kwanini muishie kuongea kwa mdomo tu na siyo kufanya kwa vitendo??

Eti unakuta mwanaume anasema "kuna demu jana nilimtongoza akakubali muda ule ule na akanipa mzigo muda ule ule" halafu anamalizia kwa kusema "daah wanawake wa siku hizi mnajirahisisha sana acheni umalaya la sivyo wanaume tutaendelea kupiga na kusepa au kuzalisha na kuacha" sasa mwanaume kama huyu unamuona tu ni jinsi gani alivyo mnafiki yaani anajifanya kusikitishwa na wimbi la wadada kujirahisisha wakati huo huo yeye ndiye kinara wa kuwatongoza hao wadada ili wajirahisishe sasa kama kweli huyu mwanaume angekuwa hapendi wanawake wajirahisishe kwanini asiache kuwatongoza na kuwaomba mizigo kama hana nia nao??

Namaanisha kama wanaume mna nia ya kutusaidia wanawake na mmeona kwa maneno haisaidii kwanini msifanye kwa vitendo kwa kuacha hayo mambo yanayowafanya wanawake wajirahisishe kwenu?? Halafu wanaume wengi utasikia wanasema "kwanini mwanamke ukitongozwa ukubali" badala ya kuuliza "kwanini mwanaume anatongoza pasipo na nia ya dhati" yaani wanalazimisha ionekane kama mwanaume kutongoza siyo kosa ila mwanamke kukubali ndiyo kosa wakati actually kinachoanza ni kutongoza halafu kinachofuata ndiyo kukubali au kukataa hivyo lazima tukubali kuwa mwanaume anayetongoza na mwanamke anayekubali wote wana makosa na haya yote ni kutokana na tamaduni kandamizi zilizoanzishwa na mababu zetu enzi hizo bibi zetu wakiwa hawana sauti kwenye jamii hivyo walitupiwa mizigo yote na walilazimishwa kuikubali watake wasitake nasikitika kusema kuwa mamlaka ambayo wanaume walipewa na Mungu juu ya wanawake babu zetu waliyatumia vibaya kwa bibi zetu yaani waliyatumia kuwakandamiza badala ya kuwalinda

Kitendo cha kulazimisha kwamba mwanaume akitenda dhambi ni sawa ila mwanamke akitenda dhambi ni kosa ni kinyume hata na maandiko kwa sisi tunaoamini katika Mungu na Dini yaani jamii yetu imejenga mitazamo ya hovyo inayochagizwa na mfumo dume kwamba eti maovu ya mwanaume hayatakiwi kuhojiwa wala kurekebishwa bali maovu ya mwanamke ndiyo yanatakiwa kuhojiwa na kurekebishwa halafu wanalazimisha kwamba eti ni Mungu ndiyo ametaka hivyo ni mungu gani huyo aliyesema wanaume mtende dhambi mnavyojisikia eti ili tu mjitofautishe na wanawake na muonekane mko juu ya wanawake?? Ukweli ni kwamba tofauti kati ya mwanamke na mwanaume haipo kwenye dhambi hata siku moja yaani imefikia hatua wanaume wanajisifia umalaya na tena wanakataa kabisa eti mwanaume haitwi malaya bali kidume ukiuliza hiyo ni kwa mujibu wa nani hawana majibu wanakuja na mapovu!!

Kama kila jinsia imeshindwa kubadilika kwa nafasi yake na kusubiria eti jinsia nyingine ndiyo ianze kubadilika halafu nayo ndiyo itafuata basi niwasihi tu tuache kusubiri meli kwenye uwanja wa ndege au embe chini ya mkorosho mimi naona ifike pahala jamii iache uongo na unafiki kama tumeamua kukemea maovu tukemee kwa jinsia zote na kama tumeamua kuacha yaendelee tuache kwa jinsia zote after all wanaume si hamna cha kupoteza bwana so why mjihangaishe?? Ninyi endeleeni kupiga na kusepa au kuzalisha na kuacha halafu tutaona mwisho wake maana hata hivyo pamoja na malalamiko yote haya ya wanaume kwa wanawake naona ni kama vile mnajaribu kudeki bahari au kufagia jangwa tu!!

Kwa kuhitimisha naomba niseme tu kuwa hiki nilichokiandika ni robo tu ya nilichonacho ila kwa sasa naomba niishie hapa lakini bado nina mengi ya kuandika hapa sitayamaliza ila nitajaribu kuyajibu kwenye comments kutegemeana na maoni ya wadau japo najua nitaoga mapovu ya kutosha hasa kutoka kwa jinsia ya kiume lakini sitajali nayakaribisha ila wale wazee wa kukisia maisha ya watu wale wa "wewe utakuwa na stress za wanaume siyo bure" au wale wa "wewe unapenda kujilinganisha na wanaume" maana wenzetu mkiguswa kidogo tu mnakimbilia kusema wanawake tunataka usawa au ushindani na wanaume utafikiri labda wanaume mna kitu cha ziada mmependelewa nacho yaani labda wenzetu hamfi mnapaa mbinguni moja kwa moja kama mlivyo na ingekuwa hivyo mbona ningebadili jinsia kabisa niwe mwanaume ili nisife ila tofauti na hapo sijaona cha kunifanya nitake kujilinganisha na mwanaume maana hapa duniani kinaogopwa kifo tu kwa sababu hakikwepeki ila mengine yote yanakwepeka tu na tunayoweza kupambana nayo tunapambana nayo kikubwa uhai sasa leo naomba mje na hoja tafadhali hizo kauli zenu za ushindani sijui usawa siyo hoja bali ni mihemko tu

Nipo....
Ahsante sana Dada, hakika umenena vyema.
 
Wewe ni mpumbavu.
Hao wanao nyanyasika si wajitoe kwenye hayo manyanyaso.hamjakatazwa kuishi mnavyotaka ndomana mnatembea uchi tunawanunua kama nyanya sikoni.
Wewe sio mwanaume utakua na jinsia mbili.
Masaidie mkeo kubeba mimba ili tuwe sawa.
Sasa unapaniki nini mkuu.? Ungerusha na ngumi kabisa maana matusi hayatoshi hapa mpumbavu kati yangu nawewe nani? Ongea uhalisia acha kuropoka ujinga kwani mimba n manyanyaso? Au ndio usawa ulioumaanisha ?
 
Wewe hata Picha huoni jiongeze wewe. Wanaume sasa hivi muanzishe chama chenu cha kuwapa empowerment mko weak mumesahaulika sana, shauri yenu endeleeni Ku cremisha maandiko mnashtuka kuvuta blanket kumekucha.
Endelea kujifariji
 
Wewe ni mpumbavu.
Hao wanao nyanyasika si wajitoe kwenye hayo manyanyaso.hamjakatazwa kuishi mnavyotaka ndomana mnatembea uchi tunawanunua kama nyanya sikoni.
Wewe sio mwanaume utakua na jinsia mbili.
Masaidie mkeo kubeba mimba ili tuwe sawa.
Mkuu haina haja ya kutukanana katika majadiliano. Kutofautiana kimawazo siyo dhambi..
 
Wewe ni mpumbavu.
Hao wanao nyanyasika si wajitoe kwenye hayo manyanyaso.hamjakatazwa kuishi mnavyotaka ndomana mnatembea uchi tunawanunua kama nyanya sikoni.
Wewe sio mwanaume utakua na jinsia mbili.
Masaidie mkeo kubeba mimba ili tuwe sawa.
Duuh!
 
Hiyo ni fact, ilifanyiwa research miaka mingi sana. Proved that a woman is inferior to a man in many ways, many ways...
Si kweli napinga huo utafiti hzo ni stereotypes tu za mwandishi na kwanini ili muonekane wanaume ni lazima mumu undermine mwanamke why?
 
Wewe jana ulikuwa wa kwanza kupingana na maandiko
Acha uongo wako ww
Hii tabia umeanza lini kuniwekea maneno mdomoni??

Jana nlikua busy Sana Sidhan Kama nliingia jf

Karibu Denmark Stockholm city tule bata
 
Sasa wanaume mnachofanya mnapinga sheria za Mungu mnasahau kwamba aliyewapa huo utawala aliweka na sheria za kutulimir wote na hakuwapa mamlaka ya kubadilisha sheria zake bali kuwatawala wanawake tu


Sasa si umuambie huyo Mungu kuwa sisi ni wabaya. Yeye karidhika na namna tunavyowaongoza ndio maana kaacha tuendelee kuwatawala tutakavyo.

Nyie wanawake sio watu wakutufundisha namna ya kufanya sheria za Mungu.

Wewe utabaki kulalamika. Utapita kama walivyopita wanawake wengine lakini hakuna litakalo badilika.

Tutawaongoza tutakavyo. Tukiamua tuwasikilize tutawasikiliza. Tukiamua kutowasikiliza hatuwasikilizi.

Kwa akili yako ulidhani Hawa alipoambiwa atatawaliwa na mwanaume ulidhani Mungu aliongea porojo.

Huna utakalo badili. Zaidi endelea kupoteza muda wako kubadilisha mambo yaliyoshindikana tokea dunia kuumbwa
 
Acha uongo wako ww
Hii tabia umeanza lini kuniwekea maneno mdomoni??

Jana nlikua busy Sana Sidhan Kama nliingia jf

Karibu Denmark Stockholm city tule bata
Mkuu hivi Stockholm ni mji wa Sweden au Denmark?
 
Back
Top Bottom