Hivi ni kwanini wanaume mnaongelea sana maovu ya wanawake na kuyaacha ya kwenu?

Hivi ni kwanini wanaume mnaongelea sana maovu ya wanawake na kuyaacha ya kwenu?

Bora wewe umekubali kuwa kumbe wanaume mna kiburi tu cha asili lakini siyo kwamba ninyi hamna maovu lakini ninyi kuwa watawala bado haiwapi ruhusa ya kutenda dhambi mnavyojisikia hiyo mifano iliyotolewa na ni moja ya unfair treatments tu kama unfair treatments nyingi sasa boss anapojihalalishia makosa kwani yupo sahihi si ukweli unabaki kuwa anakosea??

Maandiko yako wazi kwamba hakuna jinsia inayoruhusiwa kutenda dhambi regardless ya sababu mtakazozitoa kumbukeni kuna mtawala mmoja tu aliyetuumba na aliye juu yetu wote na akatuwekea sheria zake wanaume mliambiwa mtutawale wanawake hamkuambiwa mpinge sheria za muumba na kujiwekea za kwenu after all kama ingekuwa kuwa mtawala ndiyo ticket ya kufanya makosa basi Mungu angekuwa wa kwanza kufanya hivyo maana hakuna atakayemhoji wala kumuuliza chochote!!
Qur'an inasema "Wanaume ni viongozi wa wanawake"

Mtume Muhammad akasema "Laiti ingeruhusiwa kiumbe kumsujudia kiumbe mwenzie, basi mke angemsujudia mumewe. Hebu tazama daraja alilopewa mwanaume.

Wote waalimu, inawezekana mmoja ni mkubwa kuliko mwingine, mmesoma chuo kimoja ila mmoja ni mwalimu mkuu. Lazima apewe heshima yake. Yaani sisi ni waalimu wakuu. Haina maana hatukosei, laa. Tunakosea, ila mwenye dhamana, cheo, wadhifa, madaraka et al ni rahisi kujihalalishia makosa yake lakini ukikosea wewe atakusema sana na kukuonya. Mfano huo huo, mwalimu mkuu anaweza kuchelewa kurudi likizo kwa siku 3 na uaimuulize chochote. Sasa na wewe iga kuchelewa, akuandikie utoe maelezo.

Dada, we jua tu mwanaume ana mamlaka juu yako, ana wadhifa, cheo, ni kiongozi wako, ana daraja ya juu yako. Tuko sawa kimaumbile (sio 100%) lakini sisi wanaume tunajiona na ndivyo ilivyo ni watu wenye mamlaka juu yenu. Ni kawaida kwa mwenye mamlaka kujihalalishia mambo yake au akajitete na kutaka akubalike na aeleweke anavyotaka yeye.

Jiwe si unamuona sometimes anavunja katiba. Lakini nani anamhoji? Tutabaki kulalama tu sisi kama raia ndivyo wake zetu mtaendelea kulalamika lakini kimsingi sisi tuna kiburi cha asili.

Tuna ile ideology "unataka kushindana na mimi"

Hujawahi kusikia mtu akichaha mifukoni anasemaga "Leo nipo kama mwanamke kabisa" Haina maana hakuna wanawake matajiri, basi tu tunamaanisha ile hali ya wanawake kuwa ni watu wa kuamrishwa. Na mwanaume ukiwa huna hela ni kama mwanamke tu unaweza kuambiwa kufanya chochote na ukatii.

Dunia imeumbwa hivyo. Vitu viwili viwili na kimoja kinatawala kingine. Gizi na nuru, mke na mume, mtawala na matawaliwa, tajiri na masikini et al. Haina maana kimoja hakina umuhimu? No, ila kimoja kinamtawala kingine na lakini katika maisha lazima viwepo vyote otherwise hakuna maana yoyote ya huo mfumo.

Nadhani tumeelewana.
 
Sasa wanaume mnachofanya mnapinga sheria za Mungu mnasahau kwamba aliyewapa huo utawala aliweka na sheria za kutulimir wote na hakuwapa mamlaka ya kubadilisha sheria zake bali kuwatawala wanawake tu
Sio vibaya kuamini hivyo Mkuu.

Ila uhalisia ni kuwa hatupo 50/50.

Duniani kuna mtawala na mtawaliwa.
Mtawala ndiye anaweka sheria alafu mtawaliwa ndiye anazifuata. Ukilijua hili utaelewa maisha ni nini.

Mwanamke ni mtawaliwa tokea siku ya kwanza anaumbwa na Mungu. Kulingana na Biblia.
 
Safi kabisa na huu ndiyo ukweli
Wanaume wapumbavu ndo huangaika na mambo ya wanawake Kwa kuwa negative and bitter Kwa sababu ya kuumizwa pia malezi ya jamii husika aoiyokulia amezoea kuona mamake akiteswa na babake, Dada hata mashangazi na yeye anakua hivo hivo. Yani kuna wanaume wasiojielewa kutwa kulaumu wanawake Mara single mother, Malaya utafikiri wanawake wanajifanya wenyewe. Huyo ni mpumbavu na hajakua bado ana utando wa kutokujielewa.

Mazingira, trauma za utoto na lack of self esteem zimemuathiri, wanawake wenzangu kuweni makini na hao watu, watakuharibu akili yako na kukufanya usiwe na thamani kisa matatizo, kabla ya mahusiano na mjinga was lhivo mchunguze behavior zake ukiona mambo ya wanawake yana mtesa mwache, maana anahtaji kujiponya nafsi yake
 
But that doesn't give men authority to do evils as much as you want remember we have only one ruler who created us all and gave us commandments to follow so....
A woman was created to be ruled by a man, will always be under a man's authority, obey and respect him. Katika dunia hii, ondoa kitu kinaitwa usawa, there's no such a thing. Kwa vile mume kafanya kwanini mimi nisifanye, if you get into a relationship with that attitude, hakika mahusiano yatakuwa yanakushinda kila siku, utakuwa unabadilisha wapenzi kila siku.
 
Kwahiyo wewe unaona hayo mambo yote kuwepo duniani ni sawa??
Hapana shida mkuu. Hata kiulimwengu Mtawala ndiye anayepanga sheria kwa mtawaliwa.

mtawaliwa kazi yake ni kufuata sheria tuu.

Mfano. CCM ambacho ni chama tawala hapa nchini. Hiki kinaunda sheria zozote zinazowanufaisha wao na kuwakandamiza watawaliwa ambao ni Upinzani hapa ni CHADEMA, ACT n.k.

Vyama vya upinzani vitataka haki sawa lakini kamwe havitaipata haki hiyo mpaka siku vitakapokuwa chama tawala.

Mfano wa pili.
Muafrika na Mzungu
Mzungu ni mtawala na ndiye anamuwekea sheria Muafrika. Hata bara letu limechorwa mipaka na hao watawala.

Mzungu akifanya uovu huwezi sikia watu wakilalamika. Unajua kwa nini. Ni kwa sababu mtawala hafanyi makosa.

Huko uzunguni hata usikie kuna mauaji huwezi sikia watu duniani wakilalamika sana.

Haya njoo Afrika. Muafrika ni mtawaliwa. Huyu hata afanye kakosa kadogo utasikia Waafrika wajinga sana. Waafrika hawajitambui. Yaani maneno mengi ya kejeli na dhihaka.

Ndivyo ilivyo mtawaliwa akifanya kosa lazima aonekane mbaya tofauti na mtawala.

Hivyo mwanamke kwa vile ni mtawaliwa hata afanye kosa dogo kiasi gani lazima alaumiwe. Hiyo ni nature.

Na hapo ndipo utaona kuwa dunia haipo 50/50.
 
Ila hilo halibadilishi ukweli kwamba hakuna jinsia iliyoruhusiwa kutenda dhambi
Si kweli......!! Nimemaanisha nilichotaka kumaanisha. You're inferior.
 
Haya
Mke wa mjomba alimwambia baby nataka kwenda kusoma walau niwe na degree diploma haitoshi

Anko akajibu inatosha sana na ajira unayo hukuolewa kwangu kusoma siku utakayoamua kwenda masomoni beba kila kilichochako usirudi hapa. Mjadala ukafungwa

Mpaka Leo bibie yupo anatumikia taifa kupitia ualimu na ndoa pia
 
Na ndio mtu anapotumia biblia vibaya kujitetea anatoka kwenye context ya kiuhalisia, mie nimegrow as christian tangu utoto, nimeona wazazi, uncles wana wake mbona hawajibehave kuonea mwingine hasa mwanamke, my bibi ndo kabisa hakuwaga na tabia za kuwafundisha wanawe wakiume jinsi ya kuishi na wake Ali mind business tena ukiwa mkubwa chukua mji wako na mkeo.

So hyo ya kusema naweza mfundisha mwanangu jinsi ya kuishi na wake nakosea nitamfundisha misingi hafu usifikiri mambo ya 60&70s ukiapply kwenye nahusiano ya sasa ita work up ni big no kila zama na kitabu chake nabii tusicremishe maisha, mambo yamebadilika mno, inabidi kuwalea watoto kwenye misingi mizuri ya haki, utu, na heshima na sio kuonea wengine then kimbilia maandiko eti mwanamke dhaifu.

Mbona sikuhizi wanawake wanachapa kazi, kulea na kuzaa nyie wanaume mumebakiwa na nini zaidi ya daily kulalamika wanawake hawasikii.
Ndo mana nakwambiaje, ni mfumo uliwekwa kupitia vitabu vya Mungu jinsi ya mwanamke na mwanaume wanavyotakiwa kubehave kwenye jamii.

Huo mfumo unaotaka wewe uwepo inabidi uwekewe utaratibu wake ili usije ukakinzana na mafunzo ya kwenye dini.

kwa sababu mtoto wako wa kiume akipelekwa mafundisho atafundishwa misimamo ya kibiblia kuhusu wanawake na wanaume katika jamii.

akirudi mtaani na akienda shuleni anakutana na misingi mipya ya iliyowekwa na utandawazi.

akikaribia kuoa, mama mzazi anampa lisala kuhusu wanawake. yani mama mzazi anaogopa mtoto wake wa kiume asipelekeshwe na mke wake na anataka ahakikishe mtoto wake wa kiume ana uwezo wa kumtawala mke wake.

mwanamke huyo huyo anaelilia usawa, ndo huyohuyo anaemnong'oneza mtoto wake wa kiume asipelekeshwe na mke wake. Na akijua mtoto wake anatawaliwa, atavuruga tu hio ndoa.

Cariha rafki angu haya mambo yanakinzana sana.
 
Vitabu vya Mungu vimemfeva sana mwanaume kuliko mwanamke.
Tumekua programmed tangu utotoni kwamba men are more superior and more deserving than women.

Unknowingly, we feel entitled to do wrongs and be tolerated, but a woman is supposed to behave properly at all times. We have been programmed like that.

Laumu vitabu vya Mungu, sio wanaume. kama vitabu vya Mungu vingeandikwa katika maudhui ya usawa basi maisha, na jinsi tunawavyowachukulia wanawake ingekua tofauti.

Kwa vile hatuwezi kubadili maandiko, hata mtoto wa kiume utakaemzaa kesho atakuzwa na mafundisho haya haya tuliyokuzwa nayo sisi na atabehave kama tunavyobehave sisi watu wazima, na hii endless cycle haitaweza kuwa broken.
King Mbappe SHIKAMOO[emoji119]
 
Wewe hata Picha huoni jiongeze wewe. Wanaume sasa hivi muanzishe chama chenu cha kuwapa empowerment mko weak mumesahaulika sana, shauri yenu endeleeni Ku cremisha maandiko mnashtuka kuvuta blanket kumekucha.
Hahah!!! Kiuhalisia na kivitendo wanawake bado sana lakini kimaneno mko mbali sana. N.B wanaume hawahitaji vyama wala msimamizi kwasababu wanajitosheleza kiutendaji..
 
Hamhitaji vyama lakini ndo mnapuputika sana kuliko wanawake nyie mumesahaulika sana matokeo yake mumeshaanza kubaki nyuma mambo mengi, yani sikuhizi mumekuwa magoigoi, after 10 to 20 years mtaanza kulia lia it will be too late
Hahah!!! Kiuhalisia na kivitendo wanawake bado sana lakini kimaneno mko mbali sana. N.B wanaume hawahitaji vyama wala msimamizi kwasababu wanajitosheleza kiutendaji..
 
Back
Top Bottom