Hannah
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 9,679
- 39,087
Kwa hiyo kuwa juu yetu, au kuwa mtawala ndio inawapa uhalali wa kufanya dhambi?Qur'an inasema "Wanaume ni viongozi wa wanawake"
Mtume Muhammad akasema "Laiti ingeruhusiwa kiumbe kumsujudia kiumbe mwenzie, basi mke angemsujudia mumewe. Hebu tazama daraja alilopewa mwanaume.
Wote waalimu, inawezekana mmoja ni mkubwa kuliko mwingine, mmesoma chuo kimoja ila mmoja ni mwalimu mkuu. Lazima apewe heshima yake. Yaani sisi ni waalimu wakuu. Haina maana hatukosei, laa. Tunakosea, ila mwenye dhamana, cheo, wadhifa, madaraka et al ni rahisi kujihalalishia makosa yake lakini ukikosea wewe atakusema sana na kukuonya. Mfano huo huo, mwalimu mkuu anaweza kuchelewa kurudi likizo kwa siku 3 na uaimuulize chochote. Sasa na wewe iga kuchelewa, akuandikie utoe maelezo.
Dada, we jua tu mwanaume ana mamlaka juu yako, ana wadhifa, cheo, ni kiongozi wako, ana daraja ya juu yako. Tuko sawa kimaumbile (sio 100%) lakini sisi wanaume tunajiona na ndivyo ilivyo ni watu wenye mamlaka juu yenu. Ni kawaida kwa mwenye mamlaka kujihalalishia mambo yake au akajitete na kutaka akubalike na aeleweke anavyotaka yeye.
Jiwe si unamuona sometimes anavunja katiba. Lakini nani anamhoji? Tutabaki kulalama tu sisi kama raia ndivyo wake zetu mtaendelea kulalamika lakini kimsingi sisi tuna kiburi cha asili.
Tuna ile ideology "unataka kushindana na mimi"
Hujawahi kusikia mtu akichaha mifukoni anasemaga "Leo nipo kama mwanamke kabisa" Haina maana hakuna wanawake matajiri, basi tu tunamaanisha ile hali ya wanawake kuwa ni watu wa kuamrishwa. Na mwanaume ukiwa huna hela ni kama mwanamke tu unaweza kuambiwa kufanya chochote na ukatii.
Dunia imeumbwa hivyo. Vitu viwili viwili na kimoja kinatawala kingine. Gizi na nuru, mke na mume, mtawala na matawaliwa, tajiri na masikini et al. Haina maana kimoja hakina umuhimu? No, ila kimoja kinamtawala kingine na lakini katika maisha lazima viwepo vyote otherwise hakuna maana yoyote ya huo mfumo.
Nadhani tumeelewana.
Au ndio mkifanya dhambi zinageuka kuwa "haki" huku zetu wanawake zinaonekana kinyaa?