Fisrt things first kwahiyo unataka kusema kwamba yale maandiko yote yaliyowaongelea wanawake tu hayawahusu wanaume??
Kuna andiko linasema "mwanamume atawaacha baba yake na mama nyake naye ataambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja" kwahiyo kwa sababu halijamuongelea mwanamke hapo utasema halimuhusu??
Kuna andiko linasema "(mwanamume) aziniye na mwanamke hana akili kabisa afanya jambo litakalomuangamiza nafsi yake" kwahiyo kwa sababu halijamuongelea mwanamke hapo utasema halimuhusu??
Tofauti ya mwanaume na mwanamke ipo kubwa sana tu na hayo uliyoyaandika baadhi ni ukweli ila hapo uliposema wanaume mnajichangulia sheria na kujiwekea zinazowapendelea ni uongo kwa sababu mimi kwa uelewa wangu wa biblia hasa kwenye maswala ya uzinzi na uasherati sijaona sehemu inayowaruhusu wanaume kutenda dhambi zaidi maandiko yamekataza kwa jinsia zote na hilo litoshe tu kusema kwamba kila jinsia inatakiwa kuwa sahihi kwa nafasi yake and last but not least ulivyosema nikirudi nyumbani nitapika nitaosha vyombo lol utadhani hizo kazi huwa unanifanyia wewe
Mkuu hivyo ndivyo ilivyo hata ukikataa.
Walioandika hiyo Biblia ni Wanaume.
Walioandika hiyo Quran ni wanaume.
walioandika vitabu vya dini karibu zote duniani ni wanaume. Hao Budha, Hindu, Shinto, Voodoo, Bahaula, N.k. wote ni wanaume.
Huyo Mungu unayemsema anatambulika kama amebeba dhima ya Kiume. Amependelea wanaume zaidi.
Sipo Biased ila najaribu kuelezea uhalisia.
Mwanaume ndiye mtawala wakati mwanamke ni mtawaliwa.
Mtawala ndiye mtungaji wa Sheria hata katika jamii zisizo na dini zenye asili ya Abrahamu.
mtawala ndiye anaamua nini kiwe nini kisiwe akisaidiwa na Nature ambayo ndiyo watu huita Mungu.
Hiyo ni kwa habari ya Jinsia.
Kwa habari ya Rangi. Mtawala ni rangi nyeupe. Yaani wazungu kwa jamii zao.
Hao ndio hutunga sheria na hata mipaka ya nchi zetu wao ndio waliipanga na kuichora.
Wazungu huko kwao sio kwamba hawana mambo ya ajabu. Sio kwamba hawauani. Wanauana tena sana lakini kwa nini wao dunia iwapondi sana. Jibu ni moja ni kwa sababu wao ni watawala.
Lakini Muafrika akifanya uovu kidogo utaona watu wakitukana. Mara waafrika wajinga, mara waafrika ni makatili. Lakini yote ni kwa sababu Waafrika ni tabaka tawaliwa.
Mtawala hapewi lawama sana ukilinganisha na mtawaliwa.
Kama hujanielewa.
Mfano Mungu na Shetani.
Mungu ni mtawala. Yeye ndiye anaweka sheria kwa vile ni mtawala. Mungu hata akiadhibu dunia na kuiletea majanga lakini Bado watu watamsifia au kama ni kukosoa watakosoa kidogo.
Lakini shetani ambaye ni mtawaliwa hata akiua mtu mmoja utasikia watu wakimlaani sana.
Ndivyo hata kwa habari ya mwanamke na mwanaume.
Mwanaume hata akifanya umalaya huwezi sikia watu wakimtukana na kumkejeli. Hii ni kutokana yeye ni mtawala.
Lakini mwanamke fanya kidogo yaani usizini bali mkumbatie tuu hata mwanaume mbele za watu uone watu wayakavyokushukia. Watakutukana na kukupa maneno ya kejeli. Hii ni kutokana mwanamke ni Mtawaliwa.
Mtawaliwa hata afanye kizuri vipi hawezi kusifiwa. Mtawaliwa ni mtu wa kulaumiwa siku zote.
Ndio maisha hayo Marianah. Utahangaika lakini hakuna atakayekusaidia. Hata huyo Mungu hanaatakachofanya kwenye hayo malalamiko yako. Kwani yeye ndiye aliyeweka mambo yaende hivyo.
Zaidi ya yote. Tuishi kwa kupendana iwe ni tabaka tawala au Tawaliwa. Iwe ni Simba au Swala.
Kalagabaho