Marianah huu ndio Ulimwengu.
Ulimwengu wa pande mbili.
Giza na Nuru. Nuru inatawala giza.
Muumba na muumbaji.
Mtawala na mtawaliwa.
Masikini na Tajiri.
Mungu na Shetani.
Mwanaume na Mwanamke.
Mweupe na Mweusi. N.k.
Mwanamke yupo kundi la kutawaliwa. Hata afanye jambo gani zuri mtawaliwa ni mtawaliwa tuu. Atabaki kuwa mtumwa wa Mwanaume.
Utahangaika sana Kupambana na Nature.
Hilo lipo wazi hata kwa Viumbe wengine waliowengi.
Mwanamke akienda porini akikutana na Nyani au Sokwe hawezi kumtisha kwa lolote. Sokwe atamchukulia kama mwanamke tuu. Nyani atakuchukulia kama mwanamke tuu. Na ndivyo ilivyo. Wewe ni mwanamke utabaki kama mwanamke na utachukuliwa kama mwanamke.
Yaani tunaweza kusema. Mwanamke yupo upande dhaifu wakati Mwanaume yupo upande mkuu.
Hata Mungu pamoja ya kuwa hana Jinsia lakini Bado anaitwa Baba. Yaani mwenye nguvu, Mamlaka, Asiyekosea, Mtawala.
Mungu hawezi itwa Mama wala mwanamke kwa kuwa Mwanamke anasifa ya Kutawaliwa, Hana nguvu, anayekosea mara kwa mara, Anayeenda kila mwezi katika unajisi wake n.k.
Mwanamke pamoja na umuhimu wake lakini mpaka dunia inaisha atabaki kuonekana mkosaji siku zote.
Hata huko Ulaya wanapojitahidi kutetea haki zao lakini bado Mwanamke anachukuliwa kama kiumbe duni tuu.
Kuhusu Uovu. Dhambi ni dhambi haijalishi ni nani anaifanya.
Lakini Biblia inamtambua mwanamke kwa namna kadhaa. Moja ya namna hizo ni kuwa mwanamke ni kiumbe dhaifu sana.
Pia biblia uisemayo inamchukulia Mwanamke kama daraja la chini kabisa.
Moja, Biblia inamtaka mwanamke asihubiri mbele ya wanaume hasa wanaume halisi. Hii ni kutokana na kuwa Mwanaume hapaswi kuisikiliza sauti ya mwanamke bali mwanamke ndiye anapaswa kusikiliza sauti ya mwanaume.
Pili, Mwanamke maumbile yake yanamfinya na kumdunisha awapo kwenye makutano. mfano Biblia inamkataza Mwanamke aliyekatika siku zake kuingia mahali pa ibada. Yaani kanisani au msikitini.
Tatu, Mwanamke mchawi anatakiwa kuuawa. Lakini Biblia imenyamaza kuhusu mwanaume mchawi. Je haikujua kama kuna wanaume wachawi. Jibu ni hapana. Ilijua.
Lakini kwa vile Mwanamke yupo tabaka la chini kwa habari za jinsia ndio maana kawekewa sheria nyingi kuliko mtawala.
Wanaume ndio watawala ndio maana wanaweka sheria wazitakazo na zinazowanufaisha.
Hata Mungu kwa vile ndiye mtawala ndio maana akatuwekea sheria.
Wewe utabaki kulia lia humu lakini huna utakapofika. Ukirudi nyumbani utaosha vyombo, utapika, utafua kama sio zako ni za watoto. Utapangiwa muda wa Kurudi nyumbani. Yaani wewe umetawaliwa.
Kama hujanielewa hutanielewa tena.