Hivi ni kwanini wanaume mnaongelea sana maovu ya wanawake na kuyaacha ya kwenu?

Hivi ni kwanini wanaume mnaongelea sana maovu ya wanawake na kuyaacha ya kwenu?

Vitabu vya Mungu vimemfeva sana mwanaume kuliko mwanamke.
Tumekua programmed tangu utotoni kwamba men are more superior and more deserving than women.

Unknowingly, we feel entitled to do wrongs and be tolerated, but a woman is supposed to behave properly at all times. We have been programmed like that.

Laumu vitabu vya Mungu, sio wanaume. kama vitabu vya Mungu vingeandikwa katika maudhui ya usawa basi maisha, na jinsi tunawavyowachukulia wanawake ingekua tofauti.

Kwa vile hatuwezi kubadili maandiko, hata mtoto wa kiume utakaemzaa kesho atakuzwa na mafundisho haya haya tuliyokuzwa nayo sisi na atabehave kama tunavyobehave sisi watu wazima, na hii endless cycle haitaweza kuwa broken.


Hana haja ya kulaumu vitabu vya dini. hiyo ni Nature tuu. Hata wanyama wanajua hilo.
 
""eti wanaume hatuna cha ziada kuwashinda""
nimekunukuu hapo juu hizi sasa ni dharau hata hivyo kosa sio lenu tumewaachia uhuru Sana mpaka mnatuona tuko sawa

nyie dawa yenu ilikuwa kushinda jikoni kukaa nyumbani kutokwenda shule kuzaa na kulea basi kama walivyofanya mababu zetu

nikujibu tu uzi wako kwamba ulioandika ni kazi bure tumeumbwa kuwa dominator, viongozi, daraja la juu kuliko nyie vitu Kama hivyo kuonekana kweny jamii wala usi judge we
mwenyewe umekubali tunaishi mfumo dume hayo maswali mengi ya nini? tubadilike ama? tuwe Kama nyie tukae jikoni
 
Marianah huu ndio Ulimwengu.

Ulimwengu wa pande mbili.

Giza na Nuru. Nuru inatawala giza.

Muumba na muumbaji.

Mtawala na mtawaliwa.

Masikini na Tajiri.

Mungu na Shetani.

Mwanaume na Mwanamke.

Mweupe na Mweusi. N.k.

Mwanamke yupo kundi la kutawaliwa. Hata afanye jambo gani zuri mtawaliwa ni mtawaliwa tuu. Atabaki kuwa mtumwa wa Mwanaume.

Utahangaika sana Kupambana na Nature.

Hilo lipo wazi hata kwa Viumbe wengine waliowengi.

Mwanamke akienda porini akikutana na Nyani au Sokwe hawezi kumtisha kwa lolote. Sokwe atamchukulia kama mwanamke tuu. Nyani atakuchukulia kama mwanamke tuu. Na ndivyo ilivyo. Wewe ni mwanamke utabaki kama mwanamke na utachukuliwa kama mwanamke.

Yaani tunaweza kusema. Mwanamke yupo upande dhaifu wakati Mwanaume yupo upande mkuu.

Hata Mungu pamoja ya kuwa hana Jinsia lakini Bado anaitwa Baba. Yaani mwenye nguvu, Mamlaka, Asiyekosea, Mtawala.

Mungu hawezi itwa Mama wala mwanamke kwa kuwa Mwanamke anasifa ya Kutawaliwa, Hana nguvu, anayekosea mara kwa mara, Anayeenda kila mwezi katika unajisi wake n.k.

Mwanamke pamoja na umuhimu wake lakini mpaka dunia inaisha atabaki kuonekana mkosaji siku zote.

Hata huko Ulaya wanapojitahidi kutetea haki zao lakini bado Mwanamke anachukuliwa kama kiumbe duni tuu.

Kuhusu Uovu. Dhambi ni dhambi haijalishi ni nani anaifanya.

Lakini Biblia inamtambua mwanamke kwa namna kadhaa. Moja ya namna hizo ni kuwa mwanamke ni kiumbe dhaifu sana.

Pia biblia uisemayo inamchukulia Mwanamke kama daraja la chini kabisa.

Moja, Biblia inamtaka mwanamke asihubiri mbele ya wanaume hasa wanaume halisi. Hii ni kutokana na kuwa Mwanaume hapaswi kuisikiliza sauti ya mwanamke bali mwanamke ndiye anapaswa kusikiliza sauti ya mwanaume.

Pili, Mwanamke maumbile yake yanamfinya na kumdunisha awapo kwenye makutano. mfano Biblia inamkataza Mwanamke aliyekatika siku zake kuingia mahali pa ibada. Yaani kanisani au msikitini.

Tatu, Mwanamke mchawi anatakiwa kuuawa. Lakini Biblia imenyamaza kuhusu mwanaume mchawi. Je haikujua kama kuna wanaume wachawi. Jibu ni hapana. Ilijua.

Lakini kwa vile Mwanamke yupo tabaka la chini kwa habari za jinsia ndio maana kawekewa sheria nyingi kuliko mtawala.

Wanaume ndio watawala ndio maana wanaweka sheria wazitakazo na zinazowanufaisha.

Hata Mungu kwa vile ndiye mtawala ndio maana akatuwekea sheria.

Wewe utabaki kulia lia humu lakini huna utakapofika. Ukirudi nyumbani utaosha vyombo, utapika, utafua kama sio zako ni za watoto. Utapangiwa muda wa Kurudi nyumbani. Yaani wewe umetawaliwa.

Kama hujanielewa hutanielewa tena.
 
Mamii wanaume ni dhaifu sana, maumivu yao hupoa kwa muda mrefu sana hivyo kwa kusema madhaifu yetu kunawapa a certain releaf.

Kwa upande wa kujisifia kwa kufanya maovu na kujiona ni sahihi kwao kufanya hivyo basi husababishwa na malezi mabovu, maumivu ya muda ambayo hayajapoa, kujipa moyo, kukosa hofu ya Mungu, kukosa utashi, kukosa utu, kuwa na uchumi mbovu(hivyo faraja pekee ni maovu hayo) lakini pia ni kukosa akili.
 
Kwani wewe mpagani Dada??? Maswali yako yote yamejibiwa na Mungu Soma kitabu kitakatifu, ukiendelea kubishana basi endelea kubishana na Mungu....
Huwezi kuwa sawa na Mwanaume hata kama ukivaa suruali mama weeee,
Na hiyo ni nature huwezi kuibadili, kubali tuu kuwa wewe ni mwanamke na sisi ni Wanaume,ukishajua nafasi yako vzr, huwezi kupoteza muda kubishana na mambo ambayo majibu yake Yapo wazi
 
Baada ya kusoma taarifa yote, nime-observe vitu vichache.
  1. Mwandishi dada Marianah wewe ni mwandishi mzuri, matumizi ya alama - 100%, matumizi ya aya - 100%, mtiririko wa habari husika - 100%, kutochanganya lugha - 100% nk nk.
  2. Content ya ulichokiandika - sina comment.
  3. Inawezekana kabisa msukumo wa ulichokiandika umetokana na kelele za wanaume kulalamika kwenye mitandao, lakini naamini kuna msukumo mwingine nje ya huo, na kwa vile 3, 7, 8 na 10.
All in all, wewe ni moja ya wanawake wachache humu wanaoweza kuandika andishi likaenda kwa mtiririko mzuri, likasomeka hata kama content ni 0.

Nikipata muda nitakuelewa, big up.
 
Back
Top Bottom