Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 6,156
- 10,974
Wanawake hupenda wanaume machachari ambao hawajatulia hata kidogo. Sie walokole tutaishia kupendwa na mama zetu tu. Nilibakisha kamoja, nako kameyeyuka yeyu kisa tulikuwa tukiongozana kuelekea somewhere, kwa bahati mbaya akakatiza mwanamke mmoja hivi ameushona mtrako wa kwenda, mlainiiii, halafu unanesa nesa, nikausindikiza kwa macho huku nikizuia shingo isirotate ili nisimkwaze mchumba wangu, muda huo mchumba wangu alikuwa busy anachat njiani
Nilishtushwa na swali, "Mbona huangalii nyashi kama wenzio?" Nikabaki nacheka tu, akamalizia kwa kusema, "Tatizo lako huna hekaheka, umepoa kama uji wa mgonjwa, nilidhani simu yako huwa unaieka Airplane Mode unapokuwa na mimi, kumbe huna wa ziada wa kukusumbua sumbua", kisha akacheka, kiutani utani tu penzi likavuja na kufa kabisa
Mtaani kwangu kuna kijana mwenzangu hatari sana unaambiwa, ananunua nyapu kuliko maelezo, cha ajabu vibinti vya Form Thrii, wakina Dazeti, majimama, mke za mtu zinamgombania kuliko kawaida. Mwenzie natoka nje na ka baibo kangu, maji ya uhai pembeni na kiredio changu chenye flash iliyosheheni ngoma za Awilo Longomba, cha ajabu kila binti ninayemuita, anaishia kusema "Seriously!" na kuondoka
Wanawake kuweni na huruma, wengine tuko single