Anaeijua historia ya Ikulu ya Magogoni atusimulie, naambiwa ulikuwa msikiti, mzungu akapapenda akageuza makazi yake kisha kuwa Ikulu.
Hili lina ukweli wowote?
Naomba kujuzwa.
Troiker,
Kuna video hapa inaeleza historia ya Ikulu na muelezaji ni Abdallah Mohamed Saleh maarufu kwa jina la Abdallah Tambaza.
Abdallah ni kinying'inya cha ukoo wa Tambaza wamiliki enzi hizo za ardhi ilipo hii leo Ikulu ambayo imejengwa zaidi ya miaka 150 iliyopita.
Abdallah anaijua historia yote ya babu zake kwa majina yao historia ambayo imerithiwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa takriban miaka 200.
Ukimuuliza Abdallah huyo Abdallah aliepewa yeye jina lake ni nani atakushangaza kwani atakutajia na jina la mkewe na wapi waliishi na atakuonyesha hivi sasa kinying'inya mwenye jina la huyo Bi Mkubwa.
Huyu ndiye Abdallah Tambaza aliyeeleza historia ya Ikulu na baadhi ya makaburi ya babu zake yamo ndani ya ua wa Ikulu na ndani ya ua wa ofisi za serikali Magogoni pale Central Establishment.
Hermann von Wissmann aliyeleta jeshi la mamluki kutoka Sudan na Mozambique kuja kupigana na Abushiri bin Salim na Mtwa Mkwawa aliishi katika jengo hilo kama Gavana wa pili wa Germany Ostafrika.
Wissmann ndiye aliyemleta Chief Mohosh Shangaan na Sykes Mbuwane katika ardhi ya Tanganyika kutoka Mozambique na koo hizi mbili zikajakuwa maarufu sana katika mji wa Dar-es-Salaam na katika historia ya kudai uhuru wa Tanganyika.
Hawa Wazulu, Wanubi kutoka Sudan na Wamanyema kutoka Belgian Congo waliwakuta wenyeji wa Dar-es-Salaam akina Tambaza na Chaurembo na koo myingine bado wanahodhi ardhi zao ndani ya utawala wa Wajerumani.
Ndiyo unakuta Kariakoo kulikuwa na Msikiti wa Mtoro, Magomeni Msikiti wa Ndungumbi na Mwinyimkuu wote hawa ndugu kwa nasaba na Uislam.
Sehemu ya Kitumbini pakajengwa Msikiti wa Ibadh, Msikiti wa Waarabu kutoka Yemen na msikiti wa Sunni uliojengwa na Wahindi.
Hali ni hivi kuanzia Mbwamaji, Msasani, Kunduchi hadi Bagamoyo.
Wakoloni baada ya kuchukua jengo lile la Waislam na kufanya makazi ya serikali hawakuweza tena kugusa ardhi zilizokuwa na misikiti na ardhi hizo zikabakia kuwa wakfu hadi hii leo ingawa pakazuka matatizo ya mali za Waislam baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961.