Hivi ni kweli ile Ikulu ya Dar Magogoni ulikuwa msikiti zama hizo?

Hivi ni kweli ile Ikulu ya Dar Magogoni ulikuwa msikiti zama hizo?

Kuna bingwa wa ngano atakuja hapa punde na uislamu unaonewa
Inside10,
Nimeileta hii kutoka pengine naona inafaa kusomwa hapa.

HISTORIA YA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA KIGOMA UJIJI

Utangulizi

Ndugu yetu mmoja siku chache zilizopita aliturushia picha ya nyumba ya Suleiman Kagobe akaeleza kuwa nyumba hiyo ndipo alipofikia Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Julius Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika katika miaka ya 1950.

Wengi tulivutiwa na historia hiii khasa kwa kuona kuwa mbele ya nyumba hiyo kulikuwa umejengwa mnara kama kumbukumbu ya historia hii.

Watu wakaandika kutaka kupata historia zaidi ya Suleiman Kagobe.

Mimi nikaandika na kumtwisha mzigo huu Hamisi Hababi afanye hima atuletee historia iliyokamilika.

Hapo chini ni historia kamili ya mzalendo na mpigania uhuru wa Tanganyika Sheikh Suleiman Kagobe kama ilivyoandikwa na ndugu yetu Hamisi Hababi na yeye kama alivyoelezwa na Mzee Brambath Ali Kiyola.

Mzee Brambath Ali Kiyola pichani hapo chini alishiriki harakati nyingi za TANU Kigoma wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika wakati huo akiwa kijana mdogo katika TANU Youth League.

Karibuni.

"Nyumba hiyo iliyopo kwenye picha ni nyumba ya marehem Sheikh Suleiman Kagobe, ambaye ndio baba wa Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe, Mzee Omar Suleiman Kagobe na M'baya Suleiman Kagobe, pamoja na dada zao watatu.

Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe ni miongoni mwa warithi wa elimu ya Dini ya Kiislam kutoka kwa baba yake na baadae alikwenda kusoma kwa Sheikh Hassan bin Ameir na Sheikh Abdallah Saleh Al Farsy Zanzibar.

Sheikh Mtumwa aliporudia Kigoma alikuwa kapata maarifa mengi ya dini na dunia.

TAA ilipoanzishwa Kigoma Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe akachaguliwa kuwa rais wa kwanza wa TAA Kigoma akiwa katika uongozi na Saadan Abdu Kandoro.

Nyumba ya kwa Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe tangu baba yao Sheikh Suleiman akiwa hai ilikuwa mojawapo ya Zawiyatul Qadiriyya Ujiji.

Katika Tanganyika Khalifa wa Qadiriyya alikuwa Sheikh Muhammad Ramiyya wa Bagamoyo.

Qadiriyya ilikuwa na nguvu kubwa Pwani ya Afrika ya Mashariki hadi Bara Tabora, Kigoma, Ujiji hadi Upare, Moshi na kupanda Machame Nkuu Kilimanjaro.

Hii ni historia inayohitaji muda wake maalum kuihadithia; kote huko bendera ya Qadiriyya ilipepea.

Qadiriyya chini ya uongozi wa Sheikh Hassan bin Ameir ina historia ya pekee katika kueneza Uislam na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Wanazuoni maarufu kutoka Dar es Salaam, Mombasa, Tanga na Zanzibar walifika Ujiji katika Zawiyya iliyokuwa nyumbani kwa Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe kusomesha.

Miongoni mwa wanazuoni wa kukumbukwa kufika na kufundisha Ujiji ni Sheikh Al Amin bin Ali Mazrui kutoka Mombasa, Sheikh Hassan bin Ameir na Sheikh Abdallah Saleh Al Farsy.

Nyumba hii ilisomesha dini kwa ukamilifu wake wote na haikubaki nyuma katika medani ya siasa za kuikomboa Tanganyika kutoka ukoloni wa Waingereza.

Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe ndiye mtu aliyekuja na kadi za kwanza za TANU na alikabidhiwa Dar es Salaam na Sheikh Hassan bin Ameir azifikishe Kigoma na Ujiji.

Kadi hizi zilianza kuuzwa majumbani kwa siri na Bi Mwanzige bint Khamis Kazukamwe.

Kwenye harakati za kudai uhuru, nyumba hii ikawa ndiyo ikifikiwa na wageni mbalimbali kutoka kila upande wa Tanganyika.

Ugeni mashuhuri ambao hautosahaulika ni ule wa uongozi wa TANU Makao Makuu, New Street Dar es Salaam ukiongozwa na Rais wa TANU Julius Nyerere, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU Sheikh Suleiman Takadir na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya TANU Bi. Titi Mohamed.

Ilikuwa mwaka wa 1955.

Katika ziara hii ya kukumbukwa ni hotuba ya Mwalimu Nyerere na Sheikh Suleiman Takadir ambaye katika hotuba yake ya Ujiji Sheikh Suleiman Takadir alikuwa akinukuu aya mbalimbali za Quran Tukufu.

Sheikh Suleiman Takadir alikuwa hodari wa kutoa hotuba kama hizi.

Ziara ya pili nyumbani kwa Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe ilikuwa ya Mufti Sheikh Hassan bin Ameir alipokuja kuifanyia kampeni TANU iliyotishiwa uimara wake na baadhi ya masheikh waliokuwa UTP wakiongozwa na Sheikh Omar Kakolwa na Sheikh Mussa Rehani.

UTP ilikuwa ikifadhiliwa na mfanyabiashara mkubwa Gullamhusein Rajabali Ladak na nduguze Kamrudin Rajabali Ladak na Sadrudin Rajabali Ladak.

Familia hii ya Kiasia ilkuwa na ushawishi sana katika jamii ya Waafrika wa Kigoma na Ujiji wakati huo.

Kwenye ziara hii ndiyo Sheikh Hassan Bin Ameir alimshawishi Sheikh Mussa Rehani na Sheikh Omar Kakolwa kuhama UTP na kuingia TANU na Sheikh Mussa Rehani akakabidhiwa kadi ya TANU msikiti wa Ijumaa Kitongoni Ujiji.

Kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika na mbio zake, kati ya mwaka 1962 mpaka 1963, Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe alihamia Ukerewena na hapo nyumbani akamuacha mdogo wake Mzee Omar Suleiman Kagobe.

Serikali na chama cha TANU waliamua kuweka kumbukumbu ya historia hii kwa kujenga mnara huo unaoonekana pembeni mwa nyumba na ungalipo mpaka sasa.''

1684698112187.png

1684698160335.png
 
Kin...
Si kazi ya Rais Muislam kushughulika na mambo ya Waislam.
Rais yuko pale kuwashughulikia wananchi wa imani zote.

Au una hofu Rais ambae si Muislam haweze kuwafanyia Waislam uadilifu?

Kama Waislam kudai vitu kwa nini husemi wadai kiwanja walipojenga ofisi ya African Association ambako leo kuna Ofisi Ndogo ya CCM?

Au kwa nini wasidai jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika ambalo leo linamilikiwa na serikali?

Au kwa nini wasijdai mali za EAMWS?

Kama kudai Waislam wana mengi ya kudai katika historia ya uhuru wa Tanganyika katika hali na mali.

Unataka Waislam wadai hadi ihsani zao?

View attachment 2629964
Hili ni Jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika lililojengwa mwaka wa 1936 kama shule kwa ajili ya watoto wa Kiislam Al Jamiatul Islamiyya Muslim School leo ni Shule ya Msingi ya Lumumba.​
Shukrani sheikh kwa kumbukumbu muhimu.
 
Troiker,
Kuna video hapa inaeleza historia ya Ikulu na muelezaji ni Abdallah Mohamed Saleh maarufu kwa jina la Abdallah Tambaza.

Abdallah ni kinying'inya cha ukoo wa Tambaza wamiliki enzi hizo za ardhi ilipo hii leo Ikulu ambayo imejengwa zaidi ya miaka 150 iliyopita.

Abdallah anaijua historia yote ya babu zake kwa majina yao historia ambayo imerithiwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa takriban miaka 200.

Ukimuuliza Abdallah huyo Abdallah aliepewa yeye jina lake ni nani atakushangaza kwani atakutajia na jina la mkewe na wapi waliishi na atakuonyesha hivi sasa kinying'inya mwenye jina la huyo Bi Mkubwa.

Huyu ndiye Abdallah Tambaza aliyeeleza historia ya Ikulu na baadhi ya makaburi ya babu zake yamo ndani ya ua wa Ikulu na ndani ya ua wa ofisi za serikali Magogoni pale Central Establishment.

Hermann von Wissmann aliyeleta jeshi la mamluki kutoka Sudan na Mozambique kuja kupigana na Abushiri bin Salim na Mtwa Mkwawa aliishi katika jengo hilo kama Gavana wa pili wa Germany Ostafrika.

Wissmann ndiye aliyemleta Chief Mohosh Shangaan na Sykes Mbuwane katika ardhi ya Tanganyika kutoka Mozambique na koo hizi mbili zikajakuwa maarufu sana katika mji wa Dar-es-Salaam na katika historia ya kudai uhuru wa Tanganyika.

Hawa Wazulu, Wanubi kutoka Sudan na Wamanyema kutoka Belgian Congo waliwakuta wenyeji wa Dar-es-Salaam akina Tambaza na Chaurembo na koo myingine bado wanahodhi ardhi zao ndani ya utawala wa Wajerumani.

Ndiyo unakuta Kariakoo kulikuwa na Msikiti wa Mtoro, Magomeni Msikiti wa Ndungumbi na Mwinyimkuu wote hawa ndugu kwa nasaba na Uislam.

Sehemu ya Kitumbini pakajengwa Msikiti wa Ibadh, Msikiti wa Waarabu kutoka Yemen na msikiti wa Sunni uliojengwa na Wahindi.

Hali ni hivi kuanzia Mbwamaji, Msasani, Kunduchi hadi Bagamoyo.

Wakoloni baada ya kuchukua jengo lile la Waislam na kufanya makazi ya serikali hawakuweza tena kugusa ardhi zilizokuwa na misikiti na ardhi hizo zikabakia kuwa wakfu hadi hii leo ingawa pakazuka matatizo ya mali za Waislam baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961.
Duuuh hizi maelezo [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Sasa nimeelewa kwanini babu naye alikimbia akaenda kuishi msasani
 
Ni kweli,hadi leo pale Ikulu mlangoni kuna maandishi ya sura moja wapo za Quran, infact ilikua ni chuo cha mafunzo ya dini,taasisi kubwa ya dini. Eneo lile lilikua likimilikiwa na familia ya Mzee Tambaza,alimiliki eneo kubwa sana kuanzia Upanga mpaka posta baharini.

Naomba kuambatanisha na ushahidi wa video ambapo hadi leo upo pale Ikulu.
View attachment 2629211
View attachment 2629208
Kwahiyo mnatakaje, mpewe ikulu iwe msikiti au vipi?!
 
Most Muslims wana shida sana,wamejaa inferiority ya hali ya juu.Wanatamani sana wao ndio wanengekuwa wengi hapa Nchini bahati mbaya hawafiki hata 1/3 ya Watanzania wote laiti kama wangekuwa hata nusu tu ya Watanzania tungekiona cha moto.
Sijui huwa wanapandikizwa vitu gani kuhusu watu wa dini zingine.
 
Mpaka Kanisa la St. Joseph Cathedral hapa posta ya zamani wamesema ulikua ni Msikiti wa Sultani.
 
Eco...
Nitakugusia kuhusu wingi au uchache wa Waislam hayo mengine ya "complex" tunaweza kujadili wakati mwingine baadae.

Nilikuwa katika mhadhara University of Iowa na Wamarekani wakanitolea takwimu zao kuwa Waislam ni "minority" Tanzania.

Niliwaeleza kuwa hizo takwimu zao hazina ukweli unaoweza kutiwa nguvu na ushahidi.

Tanganyika mwaka wa 1905 katika Vita Vya Maji Maji Waislam ndiyo walionyanyua silaha dhidi ya Wajerumani katika juhudi ya kuikomboa nchi.

Kumbukumbu ya Maji Maji Songea kuna kaburi la halaiki wamezikwa majemadari 67 wote Waislam.

Waislam ndiyo pia waliopigania uhuru wa Tanganyika kuanzia 1929 walipounda African Association harakati za kuwaunganisha wananchi wote zilipoanza.

Ukitaka majina yao nitakuwekea hapa.

Nikamaliza kwa kusema kuwa hakuna nchi duniani iliyokombolewa na kudaiwa uhuru wake na "minorities."

Iangalie historia ya uhuru wa India ulioongozwa na Nehru na Mohamed Ali Jinnah.

Historia kama hii nikawaambia Wamarekani ndiyo inayofanya takwimu zao kuwa Waislam ni wachache Tanzania ziwe hazina ukweli.

Wasome historia ya uhuru wa Tanganyika.

Ukumbi ulikuwa kimya kabisa.

Huu mjada ulimvutia sana Jonathon Glassman Mkuu wa Department of African History Northwestern University akanialika chuoni kwake kufanya mjadala mwingine kama huu.

Nilikwenda Northwestern University na tukafanya mjadala.

Kwa kuhitimisha ni kuwa kwanza Glassman yeye ameandika kuhusu Tanzania na ana vitabu "War of Words War of Stones," (2013) na "Feats and Riots, (1994), vinaeleza historia ya Zanzibar na Tanganyika kwa hiyo si mgeni na Tanzania.

Walikuwa kimya hawakunipinga.

Pili kuanzia 1999 Glassman amekuwa akiniletea wanafunzi wake Ph D kunihoji kuhusu historia ya Tanganyika.

Mmoja wa wanafunzi wake ni James Brennan ambae ameandika sana kuhusu Tanzania na kitabu chake maarufu ni "Taifa," (2012).

Glassman na mwanafunzi wake Brennan walikuwapo kwenye mhadhara huu na walikuwa kimya.

Hawakunipinga.
Wao wanaujua ukweli.

Glassman na Brennan kilipotoka kitabu cha Abdul Sykes mwaka wa 1998 kila mmoja kwa wakati wake aliandika pitio la kitabu hicho na kuchapwa katika Cambridge Journal of African History mwaka wa 1999.

Katika kutoa neno la shukurani mwisho wa mhadhara Jonathon Glassman alisema kuwa mimi nimesaidia sana katika kuiweka sawa historia ya uhuru wa Tanganyika kwa kueleza yale ambayo yeye hakuyajua na kwa hakika hayakuwa hadhir kwa wengi.

Kubwa ni hili la kuwa Julius Nyerere alipata madaraka ya kuwa kiongozi wa kudai uhuru wa Tanganyika kwa kuungwa mkono na kundi kubwa la Waislam.

Ikiwa huijui historia ya Julius Nyerere na wazalendo waliomuunga mkono nifahamishe.

Ukisoma kitabu cha Abdul Sykes hili utaliona waziwazi.

Hakuna taifa duniani ambalo uhuru wake uliongozwa katika ukombozi na "minority."
 
Mpaka Kanisa la St. Joseph Cathedral hapa posta ya zamani wamesema ulikua ni Msikiti wa Sultani.
Fab...
Hili la kuwa St. Joseph's Cathedral ulikuwa msikiti nami pia nimesoma mahali lakini hakuna ushahidi hivyo siamini.
 
Most Muslims wana shida sana,wamejaa inferiority ya hali ya juu.Wanatamani sana wao ndio wanengekuwa wengi hapa Nchini bahati mbaya hawafiki hata 1/3 ya Watanzania wote laiti kama wangekuwa hata nusu tu ya Watanzania tungekiona cha moto.
Sijui huwa wanapandikizwa vitu gani kuhusu watu wa dini zingine.
Mbona hapa unaonekana wewe ndio una hiyo inferiority ya hali ya juu? inaonekana hata ukweli kwenye hii thd umekuumiza sana,ulitamani yangekuja majibu ambayo yangekufurahisha wewe zaidi,
historia hua haipindishwi.
 
Kin...
Si kazi ya Rais Muislam kushughulika na mambo ya Waislam.
Rais yuko pale kuwashughulikia wananchi wa imani zote.

Au una hofu Rais ambae si Muislam haweze kuwafanyia Waislam uadilifu?

Kama Waislam kudai vitu kwa nini husemi wadai kiwanja walipojenga ofisi ya African Association ambako leo kuna Ofisi Ndogo ya CCM?

Au kwa nini wasidai jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika ambalo leo linamilikiwa na serikali?

Au kwa nini wasijdai mali za EAMWS?

Kama kudai Waislam wana mengi ya kudai katika historia ya uhuru wa Tanganyika katika hali na mali.

Unataka Waislam wadai hadi ihsani zao?

View attachment 2629964
Hili ni Jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika lililojengwa mwaka wa 1936 kama shule kwa ajili ya watoto wa Kiislam Al Jamiatul Islamiyya Muslim School leo ni Shule ya Msingi ya Lumumba.​
Wadai na kuchukua vitu vyao vyote, tumechoka na kelele zenu nyie wavaa kobazi khaaah.
 
Mpaka Kanisa la St. Joseph Cathedral hapa posta ya zamani wamesema ulikua ni Msikiti wa Sultani.
Walichukue nalooo tushachoka kelele za wafahidhina [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wadai na kuchukua vitu vyao vyote, tumechoka na kelele zenu nyie wavaa kobazi khaaah.
Coca...
Kwa nini unatumia lugha za kejeli?

Kuna haja gani ya kutukana kivazi cha watu katika jamii?

Mavazi yanatokana na mila na utamaduni wa watu.

Makobadhi ni viatu wanavyovaa Waswahili kama ilivyo wengine wanavyovaa viatu vya aina yao katika jamii zao.

''Kelele'' kwa Abdallah Tambaza kuhojiwa na Zuhura Yunus kuhusu historia ya wazee wake na uhusiano wao na Ikulu?

Unasema ''tumechoka,'' huo wingi unawajumuisha watu gani pamoja na wewe ambao wamechoka?

Uliyochoka ni wewe na kama umechoka kipi kizito kilichokutia uchovu?

Tanzania ni nchi ya wastaarabu na watu waungwana.

Kuwa na adabu huo ndiyo utu.
Hakuna kilichodaiwa.
 
Anaeijua historia ya Ikulu ya Magogoni atusimulie, naambiwa ulikuwa msikiti, mzungu akapapenda akageuza makazi yake kisha kuwa Ikulu.

Hili lina ukweli wowote?

Naomba kujuzwa.
Wale Mashekh ubwabwa wanawaharibu sana waumini njaa.

Hili jambo halina ukweli hata 1%,ukianza kusikiliza story ikichagizwa na maneno inasemekana mara mjukuu wa Mzee ndio kizazi Mzee fulani mmiliki wa kisutu tafuta kazi za kufanya kwasababu watu wakikosa cha kusema ukimbilia kuzusha inasemekana inasemekana ebu na ikokosekana inasemekana story hainogi.
 
Fab...
Hili la kuwa St. Joseph's Cathedral ulikuwa msikiti nami pia nimesoma mahali lakini hakuna ushahidi hivyo siamini.

Ule ulikuwa msikiti Babu wa Babu zetu wameacha maandishi.

Lazima tudai mali za waislamu.
 
Ni kweli,hadi leo pale Ikulu mlangoni kuna maandishi ya sura moja wapo za Quran, infact ilikua ni chuo cha mafunzo ya dini,taasisi kubwa ya dini. Eneo lile lilikua likimilikiwa na familia ya Mzee Tambaza,alimiliki eneo kubwa sana kuanzia Upanga mpaka posta baharini.

Naomba kuambatanisha na ushahidi wa video ambapo hadi leo upo pale Ikulu.
View attachment 2629211
View attachment 2629208
Acha uongo wewe.
Mwaka 1891 wakati Govonor wa kwanza wa Kijerumani anaingia nchini, Ikulu ya Dar ilikua inaendelea kujengwa, ambapo ilikuja kukamilika mwaka 1896.
Wakati huohuo, Mwaka huo 8991 mzee Tambaza ndiyo alizaliwa. Unataka kutuambia mzee Tambaza alikua akimiliki eneo heo tangu akiwa Tumboni?
And kukumbusha tu, wakati Govonor wa German anaingia, jengo hilo lilikua limeanza kujengwa chini ya Uongozi wa Bushiri ambao wakishirikiana na wwnyeji (wazaramo) walipigana kuwapinga wajerumani, ndipo Mjerumani akamshawishi Mwarabu atulize watu wake yaani wenyeji, waka kaa chini Mjerumani na Mwarabu wakayajenga ambapo Mjerumani alimlipa kiasi kikubwa cha hela Mwarabu, na Mwarabu akasepea akaachia Jiji na Ikulu na kysepea zake Zanzibar.
Sasa hao wanao claim jengo lilikua lao wanatumia vigezo gani wakati mwenye jengo na mwenye mji aliviyza akasepa?
 
Anaeijua historia ya Ikulu ya Magogoni atusimulie, naambiwa ulikuwa msikiti, mzungu akapapenda akageuza makazi yake kisha kuwa Ikulu.

Hili lina ukweli wowote?

Naomba kujuzwa.
Halikuwahi kuwa Msikiti, ule ukweli kwamba lilianza kujengwa na na kukaliwa na Mwarabu halilifanyi jengo kuwa Msikiti.
Hata wakati Mwarabu anamuuzia Mjerumani, ikumbukwe hilo jengo lilikuwa halijakamilika.
Mjerumani ndiye aliyekuja kulikamilisha
 
Back
Top Bottom