Hivi ni kweli ile Ikulu ya Dar Magogoni ulikuwa msikiti zama hizo?

Hivi ni kweli ile Ikulu ya Dar Magogoni ulikuwa msikiti zama hizo?

Acha uongo wewe.
Mwaka 8991 wakati Govonor wa kwanza wa Kijerumani anaingia nchini, Ikulu ya Dar ilikua inaendelea kujengwa, ambapo ilikuja kukamilika mwaka 8996.
Wakati huohuo, Mwaka huo 8991 mzee Tambaza ndiyo alizaliwa. Unataka kutuambia mzee Tambaza alikua akimiliki eneo heo tangu akiwa Tumboni?
And kukumbusha tu, wakati Govonor wa German anaingia, jengo hilo lilikua limeanza kujengwa chini ya Uongozi wa Bushiri ambao wakishirikiana na wwnyeji (wazaramo) walipigana kuwapinga wajerumani, ndipo Mjerumani akamshawishi Mwarabu atulize watu wake yaani wenyeji, waka kaa chini Mjerumani na Mwarabu wakayajenga ambapo Mjerumani alimlipa kiasi kikubwa cha hela Mwarabu, na Mwarabu akasepea akaachia Jiji na Ikulu na kysepea zake Zanzibar.
Sasa hao wanao claim jengo lilikua lao wanatumia vigezo gani wakati mwenye jengo na mwenye mji aliviyza akasepa?
Hiyo miska vp chifu?
 
Acha uongo wewe.
Mwaka 8991 wakati Govonor wa kwanza wa Kijerumani anaingia nchini, Ikulu ya Dar ilikua inaendelea kujengwa, ambapo ilikuja kukamilika mwaka 8996.
Wakati huohuo, Mwaka huo 8991 mzee Tambaza ndiyo alizaliwa. Unataka kutuambia mzee Tambaza alikua akimiliki eneo heo tangu akiwa Tumboni?
And kukumbusha tu, wakati Govonor wa German anaingia, jengo hilo lilikua limeanza kujengwa chini ya Uongozi wa Bushiri ambao wakishirikiana na wwnyeji (wazaramo) walipigana kuwapinga wajerumani, ndipo Mjerumani akamshawishi Mwarabu atulize watu wake yaani wenyeji, waka kaa chini Mjerumani na Mwarabu wakayajenga ambapo Mjerumani alimlipa kiasi kikubwa cha hela Mwarabu, na Mwarabu akasepea akaachia Jiji na Ikulu na kysepea zake Zanzibar.
Sasa hao wanao claim jengo lilikua lao wanatumia vigezo gani wakati mwenye jengo na mwenye mji aliviyza akasepa?
Soma tena,Soma uelewe!!! Video pia umeekewa,tazama!! Hakuna mtu aliesema ilikua ni jengo la Tambaza family,bali taasisi ya dini!!
 
Soma tena,Soma uelewe!!! Video pia umeekewa,tazama!! Hakuna mtu aliesema ilikua ni jengo la Tambaza family,bali taasisi ya dini!!
Umesema eneo lile lilikua linamilikiwa na Mzee Tambaza, wakati Mzee Tambaza alikua hajaxaliwa na lilikua linamilikiwa na Bushiri ambaye aliwauzia wajerumani na kusema.
Sasa hiyo taasisi ya dini ililitoa wapi hili eneo wakati mwenye eneo aliliuza kwa Mjerumani?
 
Inside10,
Nimeileta hii kutoka pengine naona inafaa kusomwa hapa.

HISTORIA YA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA KIGOMA UJIJI

Utangulizi

Ndugu yetu mmoja siku chache zilizopita aliturushia picha ya nyumba ya Suleiman Kagobe akaeleza kuwa nyumba hiyo ndipo alipofikia Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Julius Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika katika miaka ya 1950.

Wengi tulivutiwa na historia hiii khasa kwa kuona kuwa mbele ya nyumba hiyo kulikuwa umejengwa mnara kama kumbukumbu ya historia hii.

Watu wakaandika kutaka kupata historia zaidi ya Suleiman Kagobe.

Mimi nikaandika na kumtwisha mzigo huu Hamisi Hababi afanye hima atuletee historia iliyokamilika.

Hapo chini ni historia kamili ya mzalendo na mpigania uhuru wa Tanganyika Sheikh Suleiman Kagobe kama ilivyoandikwa na ndugu yetu Hamisi Hababi na yeye kama alivyoelezwa na Mzee Brambath Ali Kiyola.

Mzee Brambath Ali Kiyola pichani hapo chini alishiriki harakati nyingi za TANU Kigoma wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika wakati huo akiwa kijana mdogo katika TANU Youth League.

Karibuni.

"Nyumba hiyo iliyopo kwenye picha ni nyumba ya marehem Sheikh Suleiman Kagobe, ambaye ndio baba wa Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe, Mzee Omar Suleiman Kagobe na M'baya Suleiman Kagobe, pamoja na dada zao watatu.

Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe ni miongoni mwa warithi wa elimu ya Dini ya Kiislam kutoka kwa baba yake na baadae alikwenda kusoma kwa Sheikh Hassan bin Ameir na Sheikh Abdallah Saleh Al Farsy Zanzibar.

Sheikh Mtumwa aliporudia Kigoma alikuwa kapata maarifa mengi ya dini na dunia.

TAA ilipoanzishwa Kigoma Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe akachaguliwa kuwa rais wa kwanza wa TAA Kigoma akiwa katika uongozi na Saadan Abdu Kandoro.

Nyumba ya kwa Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe tangu baba yao Sheikh Suleiman akiwa hai ilikuwa mojawapo ya Zawiyatul Qadiriyya Ujiji.

Katika Tanganyika Khalifa wa Qadiriyya alikuwa Sheikh Muhammad Ramiyya wa Bagamoyo.

Qadiriyya ilikuwa na nguvu kubwa Pwani ya Afrika ya Mashariki hadi Bara Tabora, Kigoma, Ujiji hadi Upare, Moshi na kupanda Machame Nkuu Kilimanjaro.

Hii ni historia inayohitaji muda wake maalum kuihadithia; kote huko bendera ya Qadiriyya ilipepea.

Qadiriyya chini ya uongozi wa Sheikh Hassan bin Ameir ina historia ya pekee katika kueneza Uislam na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Wanazuoni maarufu kutoka Dar es Salaam, Mombasa, Tanga na Zanzibar walifika Ujiji katika Zawiyya iliyokuwa nyumbani kwa Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe kusomesha.

Miongoni mwa wanazuoni wa kukumbukwa kufika na kufundisha Ujiji ni Sheikh Al Amin bin Ali Mazrui kutoka Mombasa, Sheikh Hassan bin Ameir na Sheikh Abdallah Saleh Al Farsy.

Nyumba hii ilisomesha dini kwa ukamilifu wake wote na haikubaki nyuma katika medani ya siasa za kuikomboa Tanganyika kutoka ukoloni wa Waingereza.

Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe ndiye mtu aliyekuja na kadi za kwanza za TANU na alikabidhiwa Dar es Salaam na Sheikh Hassan bin Ameir azifikishe Kigoma na Ujiji.

Kadi hizi zilianza kuuzwa majumbani kwa siri na Bi Mwanzige bint Khamis Kazukamwe.

Kwenye harakati za kudai uhuru, nyumba hii ikawa ndiyo ikifikiwa na wageni mbalimbali kutoka kila upande wa Tanganyika.

Ugeni mashuhuri ambao hautosahaulika ni ule wa uongozi wa TANU Makao Makuu, New Street Dar es Salaam ukiongozwa na Rais wa TANU Julius Nyerere, Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU Sheikh Suleiman Takadir na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya TANU Bi. Titi Mohamed.

Ilikuwa mwaka wa 1955.

Katika ziara hii ya kukumbukwa ni hotuba ya Mwalimu Nyerere na Sheikh Suleiman Takadir ambaye katika hotuba yake ya Ujiji Sheikh Suleiman Takadir alikuwa akinukuu aya mbalimbali za Quran Tukufu.

Sheikh Suleiman Takadir alikuwa hodari wa kutoa hotuba kama hizi.

Ziara ya pili nyumbani kwa Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe ilikuwa ya Mufti Sheikh Hassan bin Ameir alipokuja kuifanyia kampeni TANU iliyotishiwa uimara wake na baadhi ya masheikh waliokuwa UTP wakiongozwa na Sheikh Omar Kakolwa na Sheikh Mussa Rehani.

UTP ilikuwa ikifadhiliwa na mfanyabiashara mkubwa Gullamhusein Rajabali Ladak na nduguze Kamrudin Rajabali Ladak na Sadrudin Rajabali Ladak.

Familia hii ya Kiasia ilkuwa na ushawishi sana katika jamii ya Waafrika wa Kigoma na Ujiji wakati huo.

Kwenye ziara hii ndiyo Sheikh Hassan Bin Ameir alimshawishi Sheikh Mussa Rehani na Sheikh Omar Kakolwa kuhama UTP na kuingia TANU na Sheikh Mussa Rehani akakabidhiwa kadi ya TANU msikiti wa Ijumaa Kitongoni Ujiji.

Kupatikana kwa Uhuru wa Tanganyika na mbio zake, kati ya mwaka 1962 mpaka 1963, Sheikh Mtumwa Suleiman Kagobe alihamia Ukerewena na hapo nyumbani akamuacha mdogo wake Mzee Omar Suleiman Kagobe.

Serikali na chama cha TANU waliamua kuweka kumbukumbu ya historia hii kwa kujenga mnara huo unaoonekana pembeni mwa nyumba na ungalipo mpaka sasa.''

We Mzee Ni Mdini Sana.
Hivi Kila Mtu Akisema Alete Historia Za Familia Au Dini Yake Uku Kutatosheleza kweli .
Nyerere Alitembelea Watu Wengi Katika Tanzania Yote kutaka Ushauri Na Mawazo Tofauti.
 
We Mzee Ni Mdini Sana.
Hivi Kila Mtu Akisema Alete Historia Za Familia Au Dini Yake Uku Kutatosheleza kweli .
Nyerere Alitembelea Watu Wengi Katika Tanzania Yote kutaka Ushauri Na Mawazo Tofauti.
Kambiko,
Udini ni kuandika historia inayoeleza wapigania uhuru ambao historia iliwasahau?

Watu gani wengi ambao Nyerere aliwatembelea?

Watu hao si ndiyo hawa ambao hawakutajwa katika historia ya uhuru nami nimeandika historia zao?

Kufanya hivi kwako ni udini?

Hivi kutowataja wapigania hawa katika historia ndiyo si udini?
 
Kwa mujibu wa Tambaza ile ilikuwa ni Islamic Propagation Centre na sio msikiti au Islamic Propagation Centre ndo msikiti ndugu zetu Waislam watutoe tongotongo.
By the way majengo mengi ya enzi ya ukoloni yalitaifishwa na serikali sio ya waarabu tu hata ya wazungu hivyo sioni cha maana ya kujimilikisha vya mwarabu au mzungu na kudai vilikuwa vya dini fulani wakati baada ya kutaifishwa vilitumika na dini zote mpaka na sisi tusio na dini.
 
Kwa mujibu wa Tambaza ile ilikuwa ni Islamic Propagation Centre na sio msikiti au Islamic Propagation Centre ndo msikiti ndugu zetu Waislam watutoe tongotongo.
By the way majengo mengi ya enzi ya ukoloni yalitaifishwa na serikali sio ya waarabu tu hata ya wazungu hivyo sioni cha maana ya kujimilikisha vya mwarabu au mzungu na kudai vilikuwa vya dini fulani wakati baada ya kutaifishwa vilitumika na dini zote mpaka na sisi tusio na dini.
Smart...
Tatizo kubwa na la muda mrefu nchini petu ni kuogopa chochote kinachohusiana na Uislam.

Ukisoma historia ya Vita Vya Maji Maji utakuta majina ya makamanda Waislam walioonyongwa na Wajerumani yamekwepwa kuandikwa sawasawa.

Abdulrauf Songea Mbano jina limekatwa anaitwa Songea Mbano.

Khadija Mkomanile jina limekatwa anaitwa Mkomanile.

Tembelea Sekenke Songea Makumbusho ya Maji Maji utayaona haya.

Hassan Omari Makunganya aliyenyongwa Kilwa jina limekatwa ni Makunganya.

Njoo katika kuasisi harakati za kuunda African Association 1929 majina ya waasisi yanakwepwa.

Hutoyaona majina ya Mzee bin Sudi, Ali Said Mpima, Ibrahim Hamisi kwa kuwataja wachache.

Wala hutosoma popote kuwa pembeni ya AA kulikuwa na chama kingine Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika).

Njoo kwenye historia ya TAA.

Utasikia Nyerere akachukua uongozi mwaka wa 1953.

Huyo mwenye TAA yake Abdulwahid Kleist Sykes aliyempokea na kumtia Nyerere katika uongozi wa chama hicho hatajwi kabisa.

Hata ukiwaeleza kuwa wanaipindisha historia hawakubali kusikiliza.

Sasa kama kuna majengo yaliyotaifishwa kwani hilo kama ni kweli ndiyo sisi tusieleze historia ya mababu zetu na historia ya ardhi yetu ilipokuwa zawiyya leo Ikulu pakisomeshwa Uislam?

Kuna tatizo gani ilhali sisi ni Waislam na tupo kwetu Dar es Salaam vizazi kwa vizazi?

Au kwa kuwa wewe huijui historia ya wazee wako basi mwiko sisi kueleza historia ya wazee wetu?
 
Troiker,
Kuna video hapa inaeleza historia ya Ikulu na muelezaji ni Abdallah Mohamed Saleh maarufu kwa jina la Abdallah Tambaza.

Abdallah ni kinying'inya cha ukoo wa Tambaza wamiliki enzi hizo za ardhi ilipo hii leo Ikulu ambayo imejengwa zaidi ya miaka 150 iliyopita.

Abdallah anaijua historia yote ya babu zake kwa majina yao historia ambayo imerithiwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa takriban miaka 200.

Ukimuuliza Abdallah huyo Abdallah aliepewa yeye jina lake ni nani atakushangaza kwani atakutajia na jina la mkewe na wapi waliishi na atakuonyesha hivi sasa kinying'inya mwenye jina la huyo Bi Mkubwa.

Huyu ndiye Abdallah Tambaza aliyeeleza historia ya Ikulu na baadhi ya makaburi ya babu zake yamo ndani ya ua wa Ikulu na ndani ya ua wa ofisi za serikali Magogoni pale Central Establishment.

Hermann von Wissmann aliyeleta jeshi la mamluki kutoka Sudan na Mozambique kuja kupigana na Abushiri bin Salim na Mtwa Mkwawa aliishi katika jengo hilo kama Gavana wa pili wa Germany Ostafrika.

Wissmann ndiye aliyemleta Chief Mohosh Shangaan na Sykes Mbuwane katika ardhi ya Tanganyika kutoka Mozambique na koo hizi mbili zikajakuwa maarufu sana katika mji wa Dar-es-Salaam na katika historia ya kudai uhuru wa Tanganyika.

Hawa Wazulu, Wanubi kutoka Sudan na Wamanyema kutoka Belgian Congo waliwakuta wenyeji wa Dar-es-Salaam akina Tambaza na Chaurembo na koo myingine bado wanahodhi ardhi zao ndani ya utawala wa Wajerumani.

Ndiyo unakuta Kariakoo kulikuwa na Msikiti wa Mtoro, Magomeni Msikiti wa Ndungumbi na Mwinyimkuu wote hawa ndugu kwa nasaba na Uislam.

Sehemu ya Kitumbini pakajengwa Msikiti wa Ibadh, Msikiti wa Waarabu kutoka Yemen na msikiti wa Sunni uliojengwa na Wahindi.

Hali ni hivi kuanzia Mbwamaji, Msasani, Kunduchi hadi Bagamoyo.

Wakoloni baada ya kuchukua jengo lile la Waislam na kufanya makazi ya serikali hawakuweza tena kugusa ardhi zilizokuwa na misikiti na ardhi hizo zikabakia kuwa wakfu hadi hii leo ingawa pakazuka matatizo ya mali za Waislam baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961.
Kwa hiyo unataka kusema jengo lile lote la Ikulu lilikuwepo tayari? Wacha upuuzi haukuwa msikiti bali ofisi Islamic propagation center na haikuwa vile kama ilivyo leo! Upanuzi mkubwa ulifanywa.
 
Kwa hiyo unataka kusema jengo lile lote la Ikulu lilikuwepo tayari? Wacha upuuzi haukuwa msikiti bali ofisi Islamic propagation center na haikuwa vile kama ilivyo leo! Upanuzi mkubwa ulifanywa.
Geza,
Unachosema ni kweli kuna mengi yamefanywa kuendeleza ujenzi wa jengo hilo na wala haukuwa msikiti.

Ni bahati mbaya sana umetumia neno , "upuuzi."
 
Coca...
Kwa nini unatumia lugha za kejeli?

Kuna haja gani ya kutukana kivazi cha watu katika jamii?

Mavazi yanatokana na mila na utamaduni wa watu.

Makobadhi ni viatu wanavyovaa Waswahili kama ilivyo wengine wanavyovaa viatu vya aina yao katika jamii zao.

''Kelele'' kwa Abdallah Tambaza kuhojiwa na Zuhura Yunus kuhusu historia ya wazee wake na uhusiano wao na Ikulu?

Unasema ''tumechoka,'' huo wingi unawajumuisha watu gani pamoja na wewe ambao wamechoka?

Uliyochoka ni wewe na kama umechoka kipi kizito kilichokutia uchovu?

Tanzania ni nchi ya wastaarabu na watu waungwana.

Kuwa na adabu huo ndiyo utu.
Hakuna kilichodaiwa.
Mda wote kitu Fulani kilikua cha ostadh huyu, kile cha sheikh yulee.
Haya kusanyeni vyotee muwe navyoo. Kelele zimezidi khaaaaah.
 
Mzee Wangu Mohamed Said naomba ufafanuzi hapa, kuna mada nilisoma humu kwamba eneo lote la ferry /magogoni/Mzizima lilinunuliwa na Sultan Bargash wa kutoka Zanzibar na ndo alianza kujenga hapo panapoitwa ikulu na ndo aliita mji huo Dar ur Salaam kutoka Mzizima/Kunduchi

Swali langu je Sultan alinunua kutoka ukoo wa Tambaza? Na lini Sultan alikoma kuwa mmiliki wa eneo hilo? Je Mjerumani alipata eneo kwa mauziano na Sultani au ali koloni alipoanza kuikalia Tanganyika? Kati ya Sultan na Tambaza nani hasa mwenye eneo??
 
Mzee Wangu Mohamed Said naomba ufafanuzi hapa, kuna mada nilisoma humu kwamba eneo lote la ferry /magogoni/Mzizima lilinunuliwa na Sultan Bargash wa kutoka Zanzibar na ndo alianza kujenga hapo panapoitwa ikulu na ndo aliita mji huo Dar ur Salaam kutoka Mzizima/Kunduchi

Swali langu je Sultan alinunua kutoka ukoo wa Tambaza? Na lini Sultan alikoma kuwa mmiliki wa eneo hilo? Je Mjerumani alipata eneo kwa mauziano na Sultani au ali koloni alipoanza kuikalia Tanganyika? Kati ya Sultan na Tambaza nani hasa mwenye eneo??
Mbuyi...
Ninavyofahamu mimi ni kuwa ukoo wa Tambaza walimiliki hodhi kubwa ya ardhi kuanzia Muhimbili, Upanga yote Ocean Road hadi Magogoni.

Sultan Sayyid Majid akanunua sehemu ya Ocean Road hadi Magogoni ambapo leo ilipo Ikulu.

Sultan alikoma kuwa mmiliki walipoingia Wajerumani na kuchukua majengo aliyojenga Sayyid Majid Ocean Road hadi majengo yaliyokuja kugeuzwa kuwa makazi ya Gavana wa Kijerumani.

Hodhi asili ni mali ya ukoo wa Tambaza ila walimuuzia Sultan.

Hizi ardhi akina Tambaza walibakinazo kidogo Upanga na walitoa kiwanja kimoja hapo Upanga kama wakfu kwa Waislam na ukajengwa Msikiti maarufu wa Maamur.
 
JENGO LIJENGWE NA MJERUMANU MSEME MSIKITI.


AMA KWELI
Tatizo hamjui kusoma!

هُوَ الَّذِي بَعَثَ فِي الْأُمِّيِّينَ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ

[ AL - JUMUA' - 2 ]
Yeye ndiye aliye mpeleka Mtume kwenye watu wasio jua kusoma, awasomee Aya zake na awatakase, na awafunze Kitabu na hikima, ijapo kuwa kabla ya haya walikuwa katika upotofu ulio dhaahiri.
 
db23f75a9b1e280a7a8677e424076501.jpg
 
Smart...
Nasikitika umetumia neno "kafiri."

Historia niijuayo mimi kwa kusoma nyaraka na kwa kuhadithiwa sikukuta chembelecho "kuwamba ngoma."

Sijaona hiki kujitokeza.

Nina vitabu viwili nilivyoandika vya historia nikitumia nyaraka za wenyewe wahusika.

Kitabu cha kwanza ni kuhusu ukoo wa Sykes katika kupigania uhuru wa Tanganyika na ndani ya historia hii utaona Uislam ulivyotumika.

Kitabu cha pili ni kuhusu ukoo wa Nkya Machame ulivyohusika kuingiza Uislam Uchaggani.

Nimesoma nyaraka zao zenye umri wa miaka 100 na kupata maelezo ya historia ya ukoo wao ikienda nyuma takriban miaka 200.

Sikusoma nyaraka yoyote inayoonyesha kujikweza.

Vitabu hivi vipo atakae na asome.

Vitabu hivi vyote viwili ni matokeo ya historia ya wenyewe wananchi waliokuwapo wakati wamishionari wanaingia nchini wakifuatiwa na wakoloni kwanza Wajerumani kisha Waingereza.

Nimebahatika kumsoma Mwingereza John Iliffe akieleza historia ya Tanganyika na nimemsoma Mjerumani Bruno Gutmann akieleza historia ya Wachagga wakati Wajerumani wanaingia Kilimanjaro.

Historia niliyoandika mimi kuhusu koo hizi mbili moja kutoka Uchaggani na nyingine kutoka Mzizima hazimo katika historia zilizotangulia kuandikwa na hawa Wazungu ingawa kwa mbali Iliffe kautaja ukoo wa Sykes.

Wewe baada ya kunisoma mimi umekuja na lugha ya "neutrality," "mental slavery," na "foreign religion."

Sababu ya kujihami na maneno haya ni kushtushwa kwako na historia ya Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Wala si kweli kuwa wewe huna dini.
Wewe ni Mkristo.

Hoja zako ndizo zinazodhihirisha ukweli huu na wala si kweli kuwa hupendi dini kwa kuwa haina asili yako.

Wewe unataabishwa na historia ya kweli.

Mzee wangu nayasadiki uyasemayo japo umeninukuu tofauti, niliposema mwamba ngozi sikumaanisha kujikweza maana yangu ilikuwa nzuri tu ni kwamba kama historia iliandikwa na mkristo au kwa influence ya mzungu ni ngumu kuwataja waislamu especially pale walipoplay important roles, the same apply kama ingeandikwa na muislamu na mashaka kama wangemtaja mkristo katika umuhimu wake.

Kuhusu 'neutrallity' yangu sikupingi ni kweli natoka familia ya kikristo ila baada ya kuchimbua historia za kale zaidi na kufanikiwa kujua origin of those religious and why they were made, ninamaanisha ninaposema si mfuasi wa dini yoyote, ninafuata kile kilichasababisha dini kuwako yaani maisha ya kiroho.
 
Back
Top Bottom