Hivi ni kweli ile Ikulu ya Dar Magogoni ulikuwa msikiti zama hizo?

Hiyo miska vp chifu?
 
Soma tena,Soma uelewe!!! Video pia umeekewa,tazama!! Hakuna mtu aliesema ilikua ni jengo la Tambaza family,bali taasisi ya dini!!
 
Soma tena,Soma uelewe!!! Video pia umeekewa,tazama!! Hakuna mtu aliesema ilikua ni jengo la Tambaza family,bali taasisi ya dini!!
Umesema eneo lile lilikua linamilikiwa na Mzee Tambaza, wakati Mzee Tambaza alikua hajaxaliwa na lilikua linamilikiwa na Bushiri ambaye aliwauzia wajerumani na kusema.
Sasa hiyo taasisi ya dini ililitoa wapi hili eneo wakati mwenye eneo aliliuza kwa Mjerumani?
 
We Mzee Ni Mdini Sana.
Hivi Kila Mtu Akisema Alete Historia Za Familia Au Dini Yake Uku Kutatosheleza kweli .
Nyerere Alitembelea Watu Wengi Katika Tanzania Yote kutaka Ushauri Na Mawazo Tofauti.
 
We Mzee Ni Mdini Sana.
Hivi Kila Mtu Akisema Alete Historia Za Familia Au Dini Yake Uku Kutatosheleza kweli .
Nyerere Alitembelea Watu Wengi Katika Tanzania Yote kutaka Ushauri Na Mawazo Tofauti.
Kambiko,
Udini ni kuandika historia inayoeleza wapigania uhuru ambao historia iliwasahau?

Watu gani wengi ambao Nyerere aliwatembelea?

Watu hao si ndiyo hawa ambao hawakutajwa katika historia ya uhuru nami nimeandika historia zao?

Kufanya hivi kwako ni udini?

Hivi kutowataja wapigania hawa katika historia ndiyo si udini?
 
Kwa mujibu wa Tambaza ile ilikuwa ni Islamic Propagation Centre na sio msikiti au Islamic Propagation Centre ndo msikiti ndugu zetu Waislam watutoe tongotongo.
By the way majengo mengi ya enzi ya ukoloni yalitaifishwa na serikali sio ya waarabu tu hata ya wazungu hivyo sioni cha maana ya kujimilikisha vya mwarabu au mzungu na kudai vilikuwa vya dini fulani wakati baada ya kutaifishwa vilitumika na dini zote mpaka na sisi tusio na dini.
 
Smart...
Tatizo kubwa na la muda mrefu nchini petu ni kuogopa chochote kinachohusiana na Uislam.

Ukisoma historia ya Vita Vya Maji Maji utakuta majina ya makamanda Waislam walioonyongwa na Wajerumani yamekwepwa kuandikwa sawasawa.

Abdulrauf Songea Mbano jina limekatwa anaitwa Songea Mbano.

Khadija Mkomanile jina limekatwa anaitwa Mkomanile.

Tembelea Sekenke Songea Makumbusho ya Maji Maji utayaona haya.

Hassan Omari Makunganya aliyenyongwa Kilwa jina limekatwa ni Makunganya.

Njoo katika kuasisi harakati za kuunda African Association 1929 majina ya waasisi yanakwepwa.

Hutoyaona majina ya Mzee bin Sudi, Ali Said Mpima, Ibrahim Hamisi kwa kuwataja wachache.

Wala hutosoma popote kuwa pembeni ya AA kulikuwa na chama kingine Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika).

Njoo kwenye historia ya TAA.

Utasikia Nyerere akachukua uongozi mwaka wa 1953.

Huyo mwenye TAA yake Abdulwahid Kleist Sykes aliyempokea na kumtia Nyerere katika uongozi wa chama hicho hatajwi kabisa.

Hata ukiwaeleza kuwa wanaipindisha historia hawakubali kusikiliza.

Sasa kama kuna majengo yaliyotaifishwa kwani hilo kama ni kweli ndiyo sisi tusieleze historia ya mababu zetu na historia ya ardhi yetu ilipokuwa zawiyya leo Ikulu pakisomeshwa Uislam?

Kuna tatizo gani ilhali sisi ni Waislam na tupo kwetu Dar es Salaam vizazi kwa vizazi?

Au kwa kuwa wewe huijui historia ya wazee wako basi mwiko sisi kueleza historia ya wazee wetu?
 
Kwa hiyo unataka kusema jengo lile lote la Ikulu lilikuwepo tayari? Wacha upuuzi haukuwa msikiti bali ofisi Islamic propagation center na haikuwa vile kama ilivyo leo! Upanuzi mkubwa ulifanywa.
 
Kwa hiyo unataka kusema jengo lile lote la Ikulu lilikuwepo tayari? Wacha upuuzi haukuwa msikiti bali ofisi Islamic propagation center na haikuwa vile kama ilivyo leo! Upanuzi mkubwa ulifanywa.
Geza,
Unachosema ni kweli kuna mengi yamefanywa kuendeleza ujenzi wa jengo hilo na wala haukuwa msikiti.

Ni bahati mbaya sana umetumia neno , "upuuzi."
 
Geza,
Unachosema ni kweli kuna mengi yamefanywa kuendeleza ujenzi wa jengo hilo na wala haukuwa msikiti.

Ni bahati mbaya sana umetumia neno , "upuuzi."
Hawa watoto wa jana ni wakupuuza tu sheikh wangu.
 
Mda wote kitu Fulani kilikua cha ostadh huyu, kile cha sheikh yulee.
Haya kusanyeni vyotee muwe navyoo. Kelele zimezidi khaaaaah.
 
Mzee Wangu Mohamed Said naomba ufafanuzi hapa, kuna mada nilisoma humu kwamba eneo lote la ferry /magogoni/Mzizima lilinunuliwa na Sultan Bargash wa kutoka Zanzibar na ndo alianza kujenga hapo panapoitwa ikulu na ndo aliita mji huo Dar ur Salaam kutoka Mzizima/Kunduchi

Swali langu je Sultan alinunua kutoka ukoo wa Tambaza? Na lini Sultan alikoma kuwa mmiliki wa eneo hilo? Je Mjerumani alipata eneo kwa mauziano na Sultani au ali koloni alipoanza kuikalia Tanganyika? Kati ya Sultan na Tambaza nani hasa mwenye eneo??
 
Mbuyi...
Ninavyofahamu mimi ni kuwa ukoo wa Tambaza walimiliki hodhi kubwa ya ardhi kuanzia Muhimbili, Upanga yote Ocean Road hadi Magogoni.

Sultan Sayyid Majid akanunua sehemu ya Ocean Road hadi Magogoni ambapo leo ilipo Ikulu.

Sultan alikoma kuwa mmiliki walipoingia Wajerumani na kuchukua majengo aliyojenga Sayyid Majid Ocean Road hadi majengo yaliyokuja kugeuzwa kuwa makazi ya Gavana wa Kijerumani.

Hodhi asili ni mali ya ukoo wa Tambaza ila walimuuzia Sultan.

Hizi ardhi akina Tambaza walibakinazo kidogo Upanga na walitoa kiwanja kimoja hapo Upanga kama wakfu kwa Waislam na ukajengwa Msikiti maarufu wa Maamur.
 
JENGO LIJENGWE NA MJERUMANU MSEME MSIKITI.


AMA KWELI
Tatizo hamjui kusoma!

هُوَ الَّذِي بَعَثَ فِي الْأُمِّيِّينَ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ

[ AL - JUMUA' - 2 ]
Yeye ndiye aliye mpeleka Mtume kwenye watu wasio jua kusoma, awasomee Aya zake na awatakase, na awafunze Kitabu na hikima, ijapo kuwa kabla ya haya walikuwa katika upotofu ulio dhaahiri.
 
Mzee wangu nayasadiki uyasemayo japo umeninukuu tofauti, niliposema mwamba ngozi sikumaanisha kujikweza maana yangu ilikuwa nzuri tu ni kwamba kama historia iliandikwa na mkristo au kwa influence ya mzungu ni ngumu kuwataja waislamu especially pale walipoplay important roles, the same apply kama ingeandikwa na muislamu na mashaka kama wangemtaja mkristo katika umuhimu wake.

Kuhusu 'neutrallity' yangu sikupingi ni kweli natoka familia ya kikristo ila baada ya kuchimbua historia za kale zaidi na kufanikiwa kujua origin of those religious and why they were made, ninamaanisha ninaposema si mfuasi wa dini yoyote, ninafuata kile kilichasababisha dini kuwako yaani maisha ya kiroho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…