Hivi ni kweli kileleni mwa mlima Kilimanjaro kuna shimo?

Kuna kipindi nilipandaga kule sasa kipindi nashuka nilikaa kidogo pale gilmans kwa bahati mbaya nikasahau camera aina ya Nikon,Nilishindwa kuirudia japo kuwa camera yenyewe haikuwa ya kwangu ilinibidi niongee na mmiliki kiutu uzima.
Kwani ilikuwaje mkuu
 
Kwayo mkuu kiuhalisia shimo lipo
 
Kuna crater kubwa. Pale volcano ilipofumukia .google program ya G.P.S (earth) utaliona hilo shimo juu kileleni.
 
Daaah!! Afadhali nimepata pa kujifunza kitu.
Hv gharama za kukwea mlima pale ni kiasi gn ikiwa ni gharama ya jumla mkuu? Maana natamani sn kufanya utalii wa ndani huko kaskazini mwishoni mwa mwaka huu. Natanguliza shukrani mkui
 
Kuna crater kubwa. Pale volcano ilipofumukia .google program ya G.P.S (earth) utaliona hilo shimo juu kileleni.

Najua lipo, lakini halipo pale uhuru peak wanapo summit wapanda mlima. Unaweza kuona kwa mbali na wakati mwingine kumefunikwa na barafu...halionekani kama unavyoona kwenye google earth au satellite pictures.
 
Daaah!! Afadhali nimepata pa kujifunza kitu.
Hv gharama za kukwea mlima pale ni kiasi gn ikiwa ni gharama ya jumla mkuu? Maana natamani sn kufanya utalii wa ndani huko kaskazini mwishoni mwa mwaka huu. Natanguliza shukrani mkui

Mkubwa kule gharama zinatofautiana ukiachilia mbali kiingilio, kuna zile za wale wasaidizi na guides ukijumlisha chakula na malazi inabidi muwe kakikundi ili kupunguza gharama.

Pia kuna mavazi maalum ikiwa ni pamoja na viatu, mahema, magodoro na madude flan unaingia humo kama blanket unapolala.

Lakini inategemea mnapita route ipi, ikiwa fupi gharama zinapungua. Sisi tulipewa mabegi na kila kitu kipya kuanzia twent, viatu, fimbo, majacket ya upepo na mvua kwa siku za mwanzo, mavazi, kuna lotion maalum ya jua, mataulo, magodoro ya kujaza upepo, tulikua vizuri kwa kweli. Pia kuna taa kwa ajili ya usiku na siju ya mwisho kwa kuwa mnatembea usiku ili mfike kileleni asubuhi.

jeez boy anauelewa sana na anaweza kushauri vizuri njia ipi ni bora pia namna ya kupunguza gharama.

Cha mwisho, lazima upime afya na ufanye mazoezi hata mwezi mmoja kabla ya kupanda mlima.
 
Hilo shimo linalosemwa ni hilo hapo, lipo mlimani juu lakini sio kwenye kilele cha mlima wanapofika wapandaji. Kwa maana hiyo, sio kila anaepanda mlima analiona hilo shimo.

Hilo shimo linalosemwa ni hilo hapo, lipo mlimani juu lakini sio kwenye kilele cha mlima wanapofika wapandaji. Kwa maana hiyo, sio kila anaepanda mlima analiona hilo shimo.

Nazani hapa umemaliza ubishi wote sasa......waliokuwa wanasema hapafikiki nazani wameona wenyewe.
 
Hilo shimo linalosemwa ni hilo hapo, lipo mlimani juu lakini sio kwenye kilele cha mlima wanapofika wapandaji. Kwa maana hiyo, sio kila anaepanda mlima analiona hilo shimo.

shimo wameliona je kuna aliethubutu kufika na kuingia humo shimoni au hata kuchungulia
 
Mtafute Gerald hando mtangazaji wa EFM week iliyopita katoka kupanda mlima ,maana kafika mpaka kwenye kilele atakusaidia ingia instergram utampata au needa ofisi kwake EFM K NET HOUSE
 
Mmmh ngoja waliowahi kupanda au wanaojua watujuze
Kama hujawah kupanda unacomment ili nini
 
shimo wameliona je kuna aliethubutu kufika na kuingia humo shimoni au hata kuchungulia

Mkuu hapo siwezi kutia neno, mimi sikuchungulia pale, na sijui kama inaruhusiwa. Pia sikuona mtu akichungulia wala sijawahi kuhadithiwa na mtu aliyechungulia lile shimo.

Kuna kipindi linakua limefunikwa kwa barafu kabisa hauoni chochote.

Ukiangalia hizi picha nilizoambatanisha, utaona kwamba kilele cha mlima kipo pembeni (picha ya kwanza kwenye barafu upande wa kushoto). Na kwenye picha ya pili, angalia palipoandikwa uhuru peak, unaweza kuelewa kwanini sio kila anaefika kileleni mwa mlima analiona hilo shimo.
 
Attachments

  • IMG-20170619-WA0001.jpg
    16.3 KB · Views: 42
  • IMG-20170619-WA0003.jpg
    34.3 KB · Views: 44
umejibu vizuri! ila kuhusu crater umekosea sana!! kajifunze tena crater ni kitu cha namna gani sawa mkuu
Mkuu sijui nikajifunze nini? Maana nilichojifunza Ile ni crater!!! Na formation ya crater kwa lugha nyepesi ni tundu linalotokea juu ya kilima baada ya mlipuko wa volcano mfano mlima kilimanjaro, [emoji291] na Kuna kitu kinaitwa caldera, hili ni shimo linalotokea baada ya volcano kulipuka na ardhi ku collapse mfano lile shimo la ngorongoro, kimsingi Ile sio crater ni caldera . Sasa hebu mjadala wetu uanzie hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…