Hivi ni kweli kuna maisha baada ya kifo?

Mkuu wewe ulishatambua wito wako/kipaji/kilichokuleta?

Na "kufanikiwa sana" unamaanisha material wealth?
 
Kwanini hataki kujitokeza hadharani tumshuhudie live live? Mimi nipo kati kati saivi nikiangukia kwa wanao amini Mungu hayupo sina hatia kabisa maana alisema tumtafute kwa bidii ila ndio hivyo sasa haonekani
Niliwahi kumuuliza mzee wa kanisa swali kama hili, nikamuuliza kwanini Mungu asiangushe sh. 50 hapa ili tu niamini...akasema wakati Wana wa Israel walipokuwa wanavuka Mungu alitokeza mlima wa moto kuwapa mwanga na bado waliasi. Nikamwambia me ndomana siamini hiyo story, haiwezekani moto mkubwa utokee hapa utusindikize all the way halafu niache kuamini... mwishowe nikaambiwa tu Mungu hajaribiwi na enzi za miujiza zimeisha imebaki Upendo na Imani tu.
 
Watu tuko on autopilot (zombie mode) amka asubuhi, hangaika huko duniani doing jobs you dont like ili upate pesa Kununua things you don't really need ili ku impress people you don't really like, urudi nyumbani usiku, angalia tv, lala, repeat, Hadi ufe!!!! Na wanao waendeleze u zombie life!!
 
Personal experience ndiyo chanzo cha majibu potofu, watu wa zamani asubuhi walivyokua wanaliona jua likichomoza mashariki na jioni kuzamia magharibi hawakuhitaji kufanya research wala kujisumbua na ndio maana wakaamini jua linatembea
Mambo yanahusu miili yetu yanaweza kueleweka zaidi Kwa personal experience.

Mfano mtu unajuaje anayekufa anajisikiaje/anaona nini unless na wewe uwe Unakufa!!!

Kuna vifaa vya ku simulate period pains na labor pains, na kifaa Cha kukufanya uhisi unafanya sit ups...sijawahi kujaribu lakini sidhani kama kinaweza ku simulate experience nzima ya labor kihalisi Kwa 100%
 
imebaki upendo na imani[emoji848][emoji848]
 
Mmh, sidhani kama ni sahihi kwamba ORGANS ndo zinasababisha UHAI. Hapana, siyo sahihi. UHAI ndo husababisha ORGANS zifanye kazi. Uhai unakuwapo hata kabla ya organs.
kwenye bibilia kama sijakosea binadamu alipuliziwa pumzi ambayo ndiyo uhai wakati akiwa tayari ameshaumbwa kwa maana nyingine akiwa na organs zake tayari
 
kweli hii ni zombie life
 
Kuna maisha baada ya kufa

Sorry kwa kiswahili changu

Hivi jiulizeni wale ambao walikufa kwa kurogwa yaani kufanywa misukule

Wapo au wamezikwa?

Sasa kama mchawi ana uwezo wa kumroga mtu na kumtowa katika ulimwengu wa mwili na kumfanya mtu uyo kuwa msukule

Mungu ana shindwaje kumtowa mtu katika ulimwengu wa mwili na kumpeleka katika ulimwengu wa kiroho?

Akili kichwani

Najua kuna wengine watabisha kuwa akuna misukule au akunaga uchawi ndugu haya mambo yapo kabisa na Mungu yupo
 
kufa hakuepukiki mzungu na ujanja wake wote amechemka kuzuia kifo decomposition sawa na roho nayo ina decompose pia??
Umeshawahi kufaint? Au kupigwa dawa ya usingizi wakati wa operation. Kama umewahi, kuna chocote unachokumbuka kilikuwa kikiendelea? I guess hakuna. Ukifa umekufa. There is nothing
 
Ndiyo;kuna maisha baada ya kifo,wala usidanganyike ndugu ,yaani swali la maishako baada ya kufa linajibiwa na maisha uliowahi kuishi tangu ulipozaliwa hadi dakik ulokufa ,tengeneza your best future do not loose any time
 
Maisha baada ya kifo yapo, utarudi kwa namna nyingine, kama kwa sasa ni mwanaume unaweza rudi ukiwa mwanamke baada ya miaka kadhaa, na utakufa na utarudi tena, ipo namna ya kuyajua haya kama utaweka mambo ya dini pembeni, mpaka hapo ulipo umesharudi mara nyingi tu, ipo hivyo, huwezi jua hayo mpaka uwe na akili kubwa, ambaye ni mkeo leo anaweza kuwa mumeo kwenye maisha ya baadae ama mwanao ama adui yako ama mama yako ama baba yako ktk future life, iko hivi ukitaka kujua hili kwanza tafta namna ya kujua maisha yako yaliyopita kabla ya hii present life, ( ipo past na future kwako, sasa ipo hivi, unaweza irekebisha future yako kwanza kwa kurudi past kisha hapa kwenye present ukafanya mashahihisho, mwili, tafuta kitabu kinaitwa One soul, many bodies, uanzie hapo,

Kama huamini haya mambo achana nayo lakini ukweli ndio huo, zipo imani nyingi zimezungumzia hili, Hata YESU alisema atarudi lakini watu hamtaki kujiuliza atarudi vipi, lakini binafsi naamini amesharudi sana, na ataendelea kurudi na kurudi, basi nawe ni hivyo sababu binaadamu ni immortal.
 
hii ya misukule ipo na tunaiona sasa hiyo ya Mungu hadi sasa ni imani ambayo inatawala zaid
 
Umeshawahi kufaint? Au kupigwa dawa ya usingizi wakati wa operation. Kama umewahi, kuna chocote unachokumbuka kilikuwa kikiendelea? I guess hakuna. Ukifa umekufa. There is nothing
so hizi nyingine ni mambo ya kiimani zaidi
 
Ndiyo;kuna maisha baada ya kifo,wala usidanganyike ndugu ,yaani swali la maishako baada ya kufa linajibiwa na maisha uliowahi kuishi tangu ulipozaliwa hadi dakik ulokufa ,tengeneza your best future do not loose any time
hiyo uliyosema hapo ni kiimani zaidi I mean kidini ambayo ndiyo hadi sasa wengi wanaamini hivyo
 
mke wangu hapo baadaye anakuja nioa ,yeye anakuwa mume na mimi nabadilika kuwa mke [emoji848][emoji848]

kwa maana hiyo watu wanamsubir Jesus kumbe amesharud kitambo tu[emoji848][emoji848]

kwa maana hiyo hii siri kuna wanaojua ukwel wakatengeneza mazingira ya kuwapotosha wengi ukwel[emoji848][emoji848]
 
Hayo mambo ya misukule ni imani tu not realy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…