Hivi ni kweli kuna maisha baada ya kifo?

Mmmh! Hizo Amri kumi za Mungu zinajitosheleza kabisa mtu mtu anayezifata hawezi kufanya ushoga maana ataheshimu mwili wake na wa mwingine na ataona Mungu amempa sehemu inayoruhusiwa kutumia kwa Kila jambo, kwani Amri inaposema usitamani mke wa jirani yako maana yake Ili uwe salama basi uwe na mke wako na umtamani yeye peke yake na mke anaviungo vya kazi hiyo vinajulikana vilipo Sasa huyo atakayebadilisha maana yake tayari ameshakwenda kinyume na hizo Amri kumi.
 
1. Kama hakuna Mungu, basi kuamini Mungu yupo hakutakuwa na madhara kwako
Kiimani kuamini Mola yupo hakutoshi sababu hata makafiri wa Makka waliamini ya kuwa Mola yupo na ndiye aliyeumba na kuendesha mambo lakini walikufuru na kuwa Washirikina.

Maana ya kuamini uwepo wa Mola ni kusadikisha kwa moyo na kutamka kwa ulimi na kukatazika kwa yale aliyo yakataza na kuyatenda kwa yale aliyo ya amrisha. Kinyume na hapo bado hujaamini.
 
Duh ukishalazwa kwa udongo ndo imeisha hiyo sio poa
Yaani hilo hata akili inakataa,yaani ukifa ndiyo iwe basi tu sasa lengo la sisi kuwepo duniani ni nini ?

Huwa naona kabisa kuna tatizo la ufikiri kwa miongoni mwa watu.
 
Mimi kabla sijakujibu naomba nikuulize swali,unajuaje uwepo wa vitu visivyo onekana ?
ni ngumu kujua vitu visivyoonekana tokea utotoni tunaaminishwa vitu kiimani zaidi na kuhofia kuhoji kwa ile dhana kwamba utamkufuru Mungu lakini asili ya binadamu huwa ni hadi aone ndiyo ataamini ile ki kweli kweli tokea moyon kwa mfano hatuwezi kuona upepo ila tunaamini upo kwa sababu tunaweza kuthibitisha hilo bila shida yoyote ile na ndiyo maana tunaumbwa na utashi lakini huu utashi tuliokuwa nao hatuutumii tunaamin utashi wa wenzetu ambao upo tokea kale hizo.....kuhoji na kutaka kujua mambo kwa undani sio dhambi
 
Amri omegawanyika katika sehemu mbili.

Kuna amri ya kulazimisha kukataza
Na amri ya kulazimisha kufanya.

Unaweza kutii amri ya kuwacha makatazo lakini kwenye amri ya kufanya maamrisho ukawa zero kabisa.
 
Sasa hii waambie waumini ambao wanaendeshwa na hiyo dhana ambayo anaiamini niliyr m-quote
 
Umejibu vizuri sana,maana yake hata hivyo ambavyo huwezi kuvithibitisha na havionekani basi jua kabisa kuna ishara ya kuonyesha uwepo wa vitu hivyo.

Akili ya Mwanadamu iliyo salimika inakataa kabisa ya kuwa kifo ndiyo mwisho wako,inauliza sasa kwanini tunaishi ? Hawa wanao wadhulumu watu na kufanya ufisadi katika ardhi yaani wafanye tu kisha iwe basi kusiwe na malipo ? Akili inakataa hili katakata.

Uwepo wa moto,pepo na maisha ya kaburini,huthibitishwa kwa zile ishara zilizo ainishwa na Mitume na Manabii wa Mola toka kwa Mola mwenyeww.
 
Kama zimejitosheleza basi vilivyo nje na hayo makatazo hapo vyote ni halali
 
Sasa hii waambie waumini ambao wanaendeshwa na hiyo dhana ambayo anaiamini niliyr m-quote
Hapa nimeonyesha ya kuwa huyo uliye mnukuu alikosea katika mawazo yake.

Maana yake nakufundisha ukiwa unanukuu jambo hakikisha umelihakiki kwanza na kujua ukweli wake kabla hujaliweka katika mjadala.
 
Kama zimejitosheleza basi vilivyo nje na hayo makatazo hapo vyote ni halali
Uhalali wa jambo unaupimaje ? Kama tu kwa akili ya kawaida ya kibinadamu inajua ya kuwa kuua ni jambo baya na kudhulumu kadhalika. Kipimo chako cha uhalali wa jambo ni akili yako au ni nini hasa ?
 
Ui
Uisilamu ni Elimu tosha na hekima ndani yake,huyu amemaliza kila kitu
 
Uhalali wa jambo unaupimaje ? Kama tu kwa akili ya kawaida ya kibinadamu inajua ya kuwa kuua ni jambo baya na kudhulumu kadhalika. Kipimo chako cha uhalali wa jambo ni akili yako au ni nini hasa ?
Kwani kujitosheleza kwa kitu unakujua vipi?
 
Hata mimi kabla sijafa nilijiuliza sana hili swali...
 
Maisha yapo mkuu. Unaweza kurudishwa duniani kama panya. Me nahisi jamaa atakuwa kazaliwa tena kama kuku au ng'ombe kabisa
 
Ulosa sahihi kabisa mimi huwa nahitimisha kwa kusema hivi Watu huwa hawafikirii na hii imetokana na kujazwa ujinga wa Sayansi yaani mtu anakuja kabisa anasema ukifa umekufa,yaani hata akili tu ya kawaida inakataa,yaani niishi nife halafu iwe basi tu ? Akili inakataa kabisa.
 
Halafu unakuta unayaandika haya na hujui ROHO ni nini ? Aisee kuna watu visirani sifuri kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…