Kuweka kumbukumbu sawa wewe ni mkristo bilashaka
Utajiskiaje ukiambiwa na muislamu kua ni heri ukaamini Allah ndio Mungu wa kweli na ukampuuza huyo unayemuamini sasa ili hata ukifa na usipate nafasi ya kukutana naye itakuwa fresh tu kuliko kujitia kibri na kumpuuza mtume muhammad na mwisho ukafa ukakutana na Allah?
Naheshimu sana mawazo yako
Scars na elimu yako pia.
Ukristo ni Kuwa mfuasi wa Yesu,
Swala la imani hadi ikajengeke katika roho yako ni lazima ipite kwenye akili zako, akili ikubaliane na kile unacho kisikia ndipo itajenga imani ndani yako.
Imani na ufahamu hutakiwi kuvitengenisha hata kidogo.
Ushauri wangu kwa mtu mwenye imani yoyote ile.
Ebu soma soma sana vitabu vya dini yako, usiishie kusikiliza mawaidha anayokupa labda mchungaji au nabii wako, ebu katafuta hivo vitabu na usome mwenyewe na omba Mungu akuongoze katika kusoma kwako na kujiongezea elimu, ukipata ukakasi popote pale ni muhimu kupitia, kujifunza na kusoma pia katika upande wa dini nyingine.
Nikujibu swali lako;
Binafsi ukristo wangu level niliyofikia niya kuzungumza na Mungu wangu,
Ninae Roho yule aliyetabiliwa kushuka tangu kipindi za manabii waliokuako kipindi cha mfalme Suleiman na Daudi.
Ninae ni Roho mtakatifu, ananisaidia vitu vingi sana, hasa kupambana na roho chafu za hapa duniani.
Roho huyo unipa amani sana.
Najiuliza niende wapi nikateseke Mala 100 zaidi ?
Kama kuna mtu ataweza kunishawishi na akili zangu zikaona kuwa kuna haja ya mimi kuwa Muislamu, aisee nipo tayri.
Ubaya ni kuwa watanzania tulio wengi tunapenda kubeba vitu kwa kusikia sikia tu kwa wakubwa zetu, tujitaidi kuwa wachunguzi wa mambo na tuishi kwa akili.
Hongera wewe Scars ni mtafiti mzuri, kuna wengine huu muda hawana kabisa.