Hivi ni kweli kuna satellite uko angani yaweza piga picha watu na kurekodi sauti katika uso wa dunia?

Hivi ni kweli kuna satellite uko angani yaweza piga picha watu na kurekodi sauti katika uso wa dunia?

Nilipozungumzia noise cancelation sikumanisha environmental factors mana naelewa radio waves haziko affected na environmental factors ila hiyo satellite itatambua vipi hii sauti ni ya wewe inayekurecord mana wanaoongea ni wengi, tupo kwenye AI ndio lakini precision haiwezi fika 100%
Ndio maana tukasema ili sauti yako.iwe detected lazima kuwpo na kitu kinaitwa third part...
Third part inajumuisha minara ya simu pamoja na electronics zake zote..

Mfano ni rahisi sana ku detect sauti kwa mtu ambaye yupo karibu na simu
 
Equation ya nini mkuu, wewe lete tu hiyo picha ya mtu iliyopigwa kutoka huko angani kwa kutumia satellite, nasema hivyo kwa sababu sijawahi kuona hicho kitu kwa hiyo ukileta utakuwa umenitoa ushamba.
Usi-complicate maisha tumia simu yako kikamilifu, nenda kwenye google map/map application kisha bonyeza search itakuletea ramani ya mfumo huo kisha bonyeza hapo juu nilipozunguushia kisha chagua satellite Itakuja ramani ya mfumo wa picha na uki-zoom itakuonyesha hapo ulipo kuanzia picha ya nyumba mpaka rangi ya bati (kiujumla picha ya nyumba uliyopo sasa hivi na za jirani, ila inategemea satellite ilipita lini mara ya mwisho maana kuna jengo linaweza likawa jipya linaweza lisionekane mpaka itakapopita mara ya pili maana huwa satellite huwa inazunguuka Dunia)
 
Out of point, hebu soma kwanza mtoa mada ameuliza nini then uje ujibu
Usi-complicate maisha tumia simu yako kikamilifu, nenda kwenye google map/map application kisha bonyeza search itakuletea ramani ya mfumo huo kisha bonyeza hapo juu nilipozunguushia kisha chagua satellite Itakuja ramani ya mfumo wa picha na uki-zoom itakuonyesha hapo ulipo kuanzia picha ya nyumba mpaka rangi ya bati (kiujumla picha ya nyumba uliyopo sasa hivi na za jirani, ila inategemea satellite ilipita lini mara ya mwisho maana kuna jengo linaweza likawa jipya linaweza lisionekane mpaka itakapopita mara ya pili maana huwa satellite huwa inazunguuka Dunia)
 
Oky hyo simu yako fanya hv bonyeza 61 alafu kuna namba zitakuja... Hizo namba zitakua 6

Utaandika pembeni alafu utaandika tena #+00600#
Baada ya hapo utatumia battan za sauti utachagua WQ hapo utatuma maneno utakayo andikiwa

Hapo utatuma na utapata picha yako kama zoezi hilo litafanyika mchana itakua poa
Hapa umeandika ugoro wa wapi??
 
Acha kujifanya mshamba mchangamfu, kutokujua kitu haifanyi hicho kitu kuwa kweli hali ya kuwa ni cha uongo, hata wewe msaidie lete picha ya mtu iliyopigwa kwa kutumia camera zilizofungwa kwenye satellite angani huko.
Hama Kazuramimba mkuu, ushajua kutumia simu sasa, hama huko
.
 
Kuhusu swali hilo, ni kweli kwamba teknolojia imepiga hatua kubwa sana, hasa katika nyanja ya upelelezi wa kijijini (remote sensing), mawasiliano, na uchambuzi wa data kupitia satellite. Hapa kuna maelezo ya msingi kuhusu mada hiyo:

1. Uwezo wa Satellite Kufuatilia

Satellite nyingi zinazunguka dunia kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu kama kamera za azimio kubwa (high-resolution cameras), ambazo zinaweza kuchukua picha zenye maelezo mazuri ya vitu vidogo kama magari au watu.

Kuna satellite za kijeshi na za kibiashara ambazo zina uwezo wa kuchukua picha zenye azimio la chini ya mita moja (sub-meter resolution). Hii ina maana kuwa wanaweza kuona maelezo ya maeneo kwa ukaribu sana.


2. Ufuatiliaji wa Sauti na Video

Ingawa satellite zenye uwezo wa kuchukua picha zenye ubora wa juu zipo, uwezo wa satellite kurekodi sauti moja kwa moja kutoka kwa mtu binafsi bado haujafanyika moja kwa moja. Hii ni kwa sababu mawimbi ya sauti yanahitaji kati (medium) kama hewa kusafiri, na satellite zipo angani.

Hata hivyo, teknolojia nyingine kama drones, vifaa vya kusikiliza sauti kutoka mbali (long-range microphones), au hata simu za mkononi, zinaweza kutumika kwa ajili ya kufuatilia sauti kwa karibu.


3. Teknolojia ya Ujasusi (Surveillance Technology)

Teknolojia ya AI (Artificial Intelligence) na Big Data sasa hutumika kuchambua picha na data zinazokusanywa kutoka satellite. Kwa mfano, mfumo wa Geospatial Intelligence hutumia data za satellite kutambua mabadiliko katika mazingira au kufuatilia shughuli za binadamu.

Pia, baadhi ya satellite zina vifaa vya infrared au radar sensors, vinavyoweza kuchunguza hata vitu vilivyofunikwa na mawingu au giza.


4. Je, Wanatumia kwa Watu Binafsi?

Kufuatilia watu binafsi kupitia satellite si jambo la kawaida, kwani ni gharama kubwa sana na linahitaji rasilimali nyingi. Serikali au mashirika makubwa mara nyingi hutumia teknolojia hii kwa masuala ya ujasusi, vita, au dharura za kimazingira.

Kwa watu wa kawaida, mawasiliano kama simu, mitandao ya kijamii, au vifaa vya IoT (Internet of Things) vinaweza kufuatiliwa kwa urahisi zaidi kuliko satellite.


Ushahidi wa Teknolojia Hii:

Satellite za kibiashara kama Maxar na Planet Labs hutumia kamera za azimio kubwa kwa kazi kama ramani za Google Maps na ufuatiliaji wa mazingira.

Mfano wa kijeshi ni satellite za Marekani za NRO (National Reconnaissance Office), ambazo zimetumika kwa miaka mingi kuchunguza maeneo ya vita au upelelezi wa kimataifa.

Vifaa vya AI kama Clearview AI vinaweza kuchanganua video na picha ili kutambua watu kupitia uso wao (facial recognition), teknolojia inayoshirikiana na picha za satellite.


Kwa hivyo, teknolojia ya kufuatilia kwa satellite ipo na imepiga hatua kubwa, lakini mara nyingi hutumika kwa malengo maalum, si kwa watu wa kawaida.

Credit : AI chartGPT
Asante mkuu,walau toka kwako nimepata mwanga., ubarikiwe sana.
 
Ndio maana tukasema ili sauti yako.iwe detected lazima kuwpo na kitu kinaitwa third part...
Third part inajumuisha minara ya simu pamoja na electronics zake zote..

Mfano ni rahisi sana ku detect sauti kwa mtu ambaye yupo karibu na simu
Umenikumbusha kwa utaalamu kama huo Israeli waliutumia dhidi isbullah kama sijakosea,katika zile pagers zao,au sio mkuu.
 
Stories za vijiweni hizo, hakuna technology ya hivyo na sidhani kama itakuja kuwepo.

Satellite hazipo jinsi mnavyodanganywa na hao NASA and other space agencies kama space X na TAKATAKA zingine,

Satellite hazina uwezo wa kuchukua sauti ya watu dunian wala kupata clear picture ya vitu ardhini, isipokuwa kwa kutumika technologia ya pili ya drones za kuchukua picha au surveillance balloon zinazotumiwa kunasa picha ktk maneno tofauti kwa ukaribu mkubwa.

Mpaka Sasa tangu hizo technologia zao za anga zianze kutumika, hakuna hata single Original photo, iliyokuwa published bila kuchujwa wala kuhaririwa na kuongeza fake features, namaanisha tangu technologia ya anga hasa matumizi ya satellite na vifaa vya anga za mbali, hakujawai kuoneshwa picha original ya umbo halisi la dunia kutoka ktk space/anga za juu, isipokuwa zinapigwa baadhi ya picha na kuzimodify/kuzihariri ndipo wanazipublish ktk makala/vituo vya habari, vitabu, vipindi vya tv, na hata ktk Google map.

Nifupishe, satellite hazina uwezo kama mnaodanganywa na hao Wahuni wa NASA, na huyo kibaraka wao Elon wa space X, na nduguzo wa Russia, India+china.

Pili satellite haziko ktk space, Bali zipo anga la juu hapa hapa dunian(najua wasomi vilaza hili watapinga na notes zao za kukalili),

satellite ni vidubwasha vilivyoundwa kwa malengo maalumu ya kipelelezi, ufuatiliaji wa mifumo ya mabadiriko ya tabia nchi, uchukuaji wa tarifa+mionekano ya mazingira ktk sehemu zisizofikika,

Satellite hazitumiki kutoa huduma za mawasiliano ya kijamii, Bali kwa mashirika maalumu, mfano jeshi, hospital, vyuo n.k, vile vile satellite hazitumiki kutoa huduma ya internet wala huduma ya kurusha mawimbi ya vipindi vya TV&radio kama mnavyodangwanya na hao Wahuni.

Sayansi ya anga Ina mengi ya Siri ambayo hayafundishwi na pengine 99% ya mlichofundishwa mashuleni kuhusu anga+dunia kiujumla ni uongo mtupu, maana Kuna watu wanafaidika na huu uongo wao wa kuihadaa jamii dunia nzima.

Acheni kuwasujudu hao watu weupe, hawana huo uwezo mnaowapa kama mnavyodanganyana ktk vijiwe vyenu vya kahawa na mabangi.

Utafiti wa sayansi ya muonekano+mazingira ya Ulimwengu/dunia siku ukiwekwa wazi, dunia itazuka vita ambayo haijawai kutokea, maana tumedanganywa mengi, tumelipia Kodi ktk UONGO, tumepoteza muda&pesa mashuleni kulipia kujifunza uongo na uozo wa hao mnaowapa sifa.

Geography ni elimu ya kitapeli, sayansi ya anga kiujumla ni utapeli mtupu
 
Picha kwa kiasi fulani inawezekana, sauti hapana. Sauri haiwezi kusafiri kwenye space kwa vile kuna vacuum so hata wangeweza kusikilixs kwa umbali huo kutoka space isingewezekana.

Raisi Trump alitweet picha za siri kwa "bahati mbaya" zinazoonyesha uwezo wa satelite za siri za US. Unaweza kuona hapa

Na hata wewe unaweza kununua picha za aina hii kutoka kampuni binafsi za satelite hii wanaita 15cm resolution.
 

Attachments

  • HD_15cm_Cars.jpg
    HD_15cm_Cars.jpg
    308.2 KB · Views: 2
Habarini wanajukwaa
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza,ni kwamba nilimsikia mtu mmoja akisema,ati wazungu ni balaa maana wamepiga hatua kubwa kitekinolojia,kwamba wamefikia hatua yakutengeneza satellite inayoweza kukupiga picha,kuchukua video yako,hadi sauti yako,(lkn ni kama wakihamua kukufatilia na kama kuna umuhimu huo),mi nikashangaa sana,lkn bado najiuliza inawezekanaje hili kufanyika,hivyo nimeona kama itawapendeza, naamini humu kuna wasomi wa namna mbalimbali,naomba kujua je ni kweli tekinolojia imepiga hatua kiasi hicho?
 
Back
Top Bottom