Hivi ni kweli kuna satellite uko angani yaweza piga picha watu na kurekodi sauti katika uso wa dunia?

Ndio maana tukasema ili sauti yako.iwe detected lazima kuwpo na kitu kinaitwa third part...
Third part inajumuisha minara ya simu pamoja na electronics zake zote..

Mfano ni rahisi sana ku detect sauti kwa mtu ambaye yupo karibu na simu
 
Equation ya nini mkuu, wewe lete tu hiyo picha ya mtu iliyopigwa kutoka huko angani kwa kutumia satellite, nasema hivyo kwa sababu sijawahi kuona hicho kitu kwa hiyo ukileta utakuwa umenitoa ushamba.
Usi-complicate maisha tumia simu yako kikamilifu, nenda kwenye google map/map application kisha bonyeza search itakuletea ramani ya mfumo huo kisha bonyeza hapo juu nilipozunguushia kisha chagua satellite Itakuja ramani ya mfumo wa picha na uki-zoom itakuonyesha hapo ulipo kuanzia picha ya nyumba mpaka rangi ya bati (kiujumla picha ya nyumba uliyopo sasa hivi na za jirani, ila inategemea satellite ilipita lini mara ya mwisho maana kuna jengo linaweza likawa jipya linaweza lisionekane mpaka itakapopita mara ya pili maana huwa satellite huwa inazunguuka Dunia)
 
Out of point, hebu soma kwanza mtoa mada ameuliza nini then uje ujibu
 
Hapa umeandika ugoro wa wapi??
 
Acha kujifanya mshamba mchangamfu, kutokujua kitu haifanyi hicho kitu kuwa kweli hali ya kuwa ni cha uongo, hata wewe msaidie lete picha ya mtu iliyopigwa kwa kutumia camera zilizofungwa kwenye satellite angani huko.
Hama Kazuramimba mkuu, ushajua kutumia simu sasa, hama huko
.
 
Asante mkuu,walau toka kwako nimepata mwanga., ubarikiwe sana.
 
Ndio maana tukasema ili sauti yako.iwe detected lazima kuwpo na kitu kinaitwa third part...
Third part inajumuisha minara ya simu pamoja na electronics zake zote..

Mfano ni rahisi sana ku detect sauti kwa mtu ambaye yupo karibu na simu
Umenikumbusha kwa utaalamu kama huo Israeli waliutumia dhidi isbullah kama sijakosea,katika zile pagers zao,au sio mkuu.
 
Stories za vijiweni hizo, hakuna technology ya hivyo na sidhani kama itakuja kuwepo.

Satellite hazipo jinsi mnavyodanganywa na hao NASA and other space agencies kama space X na TAKATAKA zingine,

Satellite hazina uwezo wa kuchukua sauti ya watu dunian wala kupata clear picture ya vitu ardhini, isipokuwa kwa kutumika technologia ya pili ya drones za kuchukua picha au surveillance balloon zinazotumiwa kunasa picha ktk maneno tofauti kwa ukaribu mkubwa.

Mpaka Sasa tangu hizo technologia zao za anga zianze kutumika, hakuna hata single Original photo, iliyokuwa published bila kuchujwa wala kuhaririwa na kuongeza fake features, namaanisha tangu technologia ya anga hasa matumizi ya satellite na vifaa vya anga za mbali, hakujawai kuoneshwa picha original ya umbo halisi la dunia kutoka ktk space/anga za juu, isipokuwa zinapigwa baadhi ya picha na kuzimodify/kuzihariri ndipo wanazipublish ktk makala/vituo vya habari, vitabu, vipindi vya tv, na hata ktk Google map.

Nifupishe, satellite hazina uwezo kama mnaodanganywa na hao Wahuni wa NASA, na huyo kibaraka wao Elon wa space X, na nduguzo wa Russia, India+china.

Pili satellite haziko ktk space, Bali zipo anga la juu hapa hapa dunian(najua wasomi vilaza hili watapinga na notes zao za kukalili),

satellite ni vidubwasha vilivyoundwa kwa malengo maalumu ya kipelelezi, ufuatiliaji wa mifumo ya mabadiriko ya tabia nchi, uchukuaji wa tarifa+mionekano ya mazingira ktk sehemu zisizofikika,

Satellite hazitumiki kutoa huduma za mawasiliano ya kijamii, Bali kwa mashirika maalumu, mfano jeshi, hospital, vyuo n.k, vile vile satellite hazitumiki kutoa huduma ya internet wala huduma ya kurusha mawimbi ya vipindi vya TV&radio kama mnavyodangwanya na hao Wahuni.

Sayansi ya anga Ina mengi ya Siri ambayo hayafundishwi na pengine 99% ya mlichofundishwa mashuleni kuhusu anga+dunia kiujumla ni uongo mtupu, maana Kuna watu wanafaidika na huu uongo wao wa kuihadaa jamii dunia nzima.

Acheni kuwasujudu hao watu weupe, hawana huo uwezo mnaowapa kama mnavyodanganyana ktk vijiwe vyenu vya kahawa na mabangi.

Utafiti wa sayansi ya muonekano+mazingira ya Ulimwengu/dunia siku ukiwekwa wazi, dunia itazuka vita ambayo haijawai kutokea, maana tumedanganywa mengi, tumelipia Kodi ktk UONGO, tumepoteza muda&pesa mashuleni kulipia kujifunza uongo na uozo wa hao mnaowapa sifa.

Geography ni elimu ya kitapeli, sayansi ya anga kiujumla ni utapeli mtupu
 
Picha kwa kiasi fulani inawezekana, sauti hapana. Sauri haiwezi kusafiri kwenye space kwa vile kuna vacuum so hata wangeweza kusikilixs kwa umbali huo kutoka space isingewezekana.

Raisi Trump alitweet picha za siri kwa "bahati mbaya" zinazoonyesha uwezo wa satelite za siri za US. Unaweza kuona hapa

Na hata wewe unaweza kununua picha za aina hii kutoka kampuni binafsi za satelite hii wanaita 15cm resolution.
 

Attachments

  • HD_15cm_Cars.jpg
    308.2 KB · Views: 2
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…