Hivi ni kweli kuna siku sitakuwepo juu ya uso wa dunia?

Hili jambo linatisha sana sana hasa ukifanya Kazi mochwari kama Mimi na yale tunayokutana nayo huko
 
Tarehe 28/12/2024 tumezika ndugu na rafiki yangu mkubwa katika ndugu zangu wote. Aligongwa na gari usiku wa kuamkia tarehe Christmas. Siamini, sitakaa niamini na sujui kama itanitoka.
Mtu haumwi, Hana ugonjwa Wala tatizo lolote afe tu. Dah.
So, ni kweli tutakufa na tutazikwa. Inabidi tuamini na tukubaliane tu.
 
Kwani ilikuwa wapi kabla ya kuzaliwa?
 
Hili jambo linatisha sana sana hasa ukifanya Kazi mochwari kama Mimi na yale tunayokutana nayo huko
Mkuu huko mochware mnapaovarate. Zaidi ya kumtunza miili ya binadamu isiyo hai, kuna nini cha ziada?
 
Hakika utakufa; bila shaka, hakuna namna nyingine!!
 
RIP mkuu.
 
Huu uzi ukawe chachu ya kila mmoja wetu kutenda yaliyo mema na kumpendeza MUNGU ili tujiwekee hazina yetu mahali ambapo hakuna mwivi awezae kuiba,WANA AMANI NYINGI WAIPENDAO SHERIA YAKO WALA HAWANA LA KUWAKWAZA. happy new year friends.
 
Kifo ndio kitu pekee ambacho ni cha uhakika kwa binadamu. Vitu vingine vyote havina uhakika. Kwa hivyo huwa tunapanga mwakani nitanunua gari, nitaenda Dubai, nitapata degree lakini vyoooote hivyo havina uhakika.

Kufa ni uhakika tiketi yako imeshakatwa, tarehe ya safari inajulikana mbinguni, muda wa safari ushapangwa na seat yako tayari ipo. Inasubiriwa muda ufike tu. Kwaheri
 
Mimi ninaamini kifo ni tukio la kawaida la asili. Tulisubiri kama tunavyosubiri mwaka mpya. Kwa mda unapoishi jitahidi tu kuacha alama ili watu wajue kulikuwa na mtu wa jinsi yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…