Hivi ni kweli kuwa wenye herufi "M" kwenye kiganja wana bahati sana?

Hivi ni kweli kuwa wenye herufi "M" kwenye kiganja wana bahati sana?

we zali lako tu mkuu,mi nina hzo alama mikono yote miwili na sina lolote lile na umri unasonga
 
Aliyepoteza hiyo pesa ni nani? Nadhan ni mtu mhangaikaji kama wewe... Na alilaani sana kupoteza hiyo ela... Wewe unafurahia.... Kufa kufaana
 
Hapo kaka umechemka mbaya...
Maana iyo M haionekani mbona hapo na izo bahati zinakuja tuu sio hicho kiganja maana mie naona dabo dabo tuu hapo au M ndio ilivyo hivyo kikwenu?!!
 
Maendeleo ya binadamu hushahidishwa na bidii yake kwenye kazi. Anayebisha anipe mechanism ya herufi M kwenye kwenye kiganja na maendeleo ya binadam
 
Masikini haishiwi ndoto! Kuna mtu humu JF hua anachukua vitu kama hivi na kuvianzishia Mada za kufikirika,hivi mpaka karne hii ya kidigital bado watu wana mawazo ya kijinga kabisa?!!
 
Hahahahaaa kijiji gani hicho mkuu?
Nisije kujichanganya nikaja huko nikarudi kilema bure!
[ATTACH=
Mbona kaa yangu imezidi ila mambo ngumu bado meku!
 
Attachments

  • 1460923428524.jpg
    1460923428524.jpg
    122.2 KB · Views: 113
Mhh! Hizi imani kazi kweli kweli, ndio yale yale ya kulala na Mama yako ndipo upadate utajiri.
Waswahili wana msemo, lisemwalo lipo.
Ni mara nyingi Sana nimekuwa nikisikia tetesi kuwa, watu wenye viganja vyenye alama ya "M " wana bahati Sana, Kwa upande wangu mimi ni muumini mzuri sana Wa Mungu, ila mkono wangu wa kulia una alama ya "M " wa kushoto hauna, binafsi nimekuwa na bahati Sana ktk maisha yangu, na hili nimeanza kuamini kuwa ni kweli kiganja chenye "M"ni bahati kubwa ukiwa nacho.
Nakumbuka ilikuwa 5/january/2012 nilipoamka asubuhi nyumbani nikiwa Sina hata cent, chakula ndani kilikuwa kimeisha, na sukari ilikuwa hamna, nilikuwa nimechanganyikiwa kabisa maana biashara yangu ilianguka
ilipotimia saa 2:30 asubuhi ile, simu yangu iliita, namba Ilikuwa ngeni, nilipokea na sauti ya kike ikasikika, ilikuwa ni girlfriend wangu Wa zamani anayeishi Kwa sasa Canada, alikuwa amekuja Tanzania bila kunitaarifu, yeye tayari ana uraia wa Canada na kaolewa na mzungu, alikuwa Amekuja kusalimia ndugu zake Arusha, nikaongea naye mambo mengi kisha nikamtania Kama kumjaribu anikumbuke basi hata hela ya soda, akaniambia nisubiri kidogo, nami nikaondoka kwenda kuhangaika angalau nipate hata pesa ya kununulia hata unga, ilipotimia saa 5 nikawa nimerudi nyumbani na sh 5000 tu niliyokuwa nimepewa na rafiki yangu.
Nikamkuta Mke wangu amechuma kisamvu anakichemsha bila kujua kitaliwa na nini.
Nikampatia ile elfu 5,nikakaa ndani nikiwa na mawazo ile mbaya, nikisubiria msosi nile, ilipotimia saa 6:30 mchana, sms ikaingia kwenye simu yangu, nilipotazama ilikuwa ni m pesa, yule girlfriend wangu alikuwa kanitumia sh 950,000 ,moyo wangu Ulienda kasi Kwa mapigo yaani sikuweza kuamini, nikahisi labda alikosea tu, nikatoka mbio ndani kwenda kutoa ile pesa, akawa ananipigia sipokei, baadae akatuma sms nadhani umepata pesa niliyokutumia, sikujibu, wakati nakaribia kwenye kibanda cha m pesa ili nitoe pesa, nikaokota pochi iliyokuwa imetuna na kuiweka mfukoni.
Nilizitoa pesa Haraka Sana, kisha nikamtaarifu kuwa nimepata na kumshukuru Sana, wakati narudi nyumbani nikaitazama ile pochi kuona ni kitu gani kilikuwemo, Duh! sikuamini tena, pochi haikuwa na anuani wala ID yoyote, ilikuwa na sh laki mbili, Kwa kweli sitaisahau hiyo Siku.
Siandiki kuwa furahisha watu, bali ni kweli tupu.
Tangia kipindi hicho hadi leo, kila nalofanya linakuwa.

Kiganja changu
 
Hv viganja mnavoonyesha mbna mi siioni hio M
Maisha Kuna bahati sawa ila bidii ni muhimu sana,changanya bidii na bahati
 
HERUFI ''M'' INA ASHIRIA WEWE MTU WA BAHATI KUBWA UNAWEZA KUWA NA PESA NYINGI AU KUWA KIONGOZI MKUU KATIKA MAMBO YA SIASA AU KUWA WEWE MTU MWENYE AFYA NZURI, AU KUWA NI MWANASHERIA AU HAKIMU AU KUWA MTU MAARUFU SANA. HERUFI ''M'' KWENYE KIGANJA CHAKO CHA MKONO WA KULIA INA ASHIRIA MAMBO MAZURI YA MAISHA YAKO YA BAADAE UTAFANIKIWA JITAHIDI.
What%25E2%2580%2599s%2Bso%2Bspecial%2Babout%2Ban%2B%25E2%2580%2598M%25E2%2580%2599%2Bon%2Bthe%2BPalm%2Bof%2Bthe%2BHand.jpg

Source Muugwana Blog
scientific proof please!
 
Masikini haishiwi ndoto! Kuna mtu humu JF hua anachukua vitu kama hivi na kuvianzishia Mada za kufikirika,hivi mpaka karne hii ya kidigital bado watu wana mawazo ya kijinga kabisa?!!
lakini asili ipo,haifai kudharauliwa moja kwa moja
 
abuu garcia nashangaa kila nikikuquote nikipost inagoma.

Anyway,nilikuwa nakuambi huenda siku yako haijafika (kama unaamini)

Pia.....uko na kiganja laini,hongera.
 
HERUFI ''M'' INA ASHIRIA WEWE MTU WA BAHATI KUBWA UNAWEZA KUWA NA PESA NYINGI AU KUWA KIONGOZI MKUU KATIKA MAMBO YA SIASA AU KUWA WEWE MTU MWENYE AFYA NZURI, AU KUWA NI MWANASHERIA AU HAKIMU AU KUWA MTU MAARUFU SANA. HERUFI ''M'' KWENYE KIGANJA CHAKO CHA MKONO WA KULIA INA ASHIRIA MAMBO MAZURI YA MAISHA YAKO YA BAADAE UTAFANIKIWA JITAHIDI.
What%25E2%2580%2599s%2Bso%2Bspecial%2Babout%2Ban%2B%25E2%2580%2598M%25E2%2580%2599%2Bon%2Bthe%2BPalm%2Bof%2Bthe%2BHand.jpg

Source Muugwana Blog
M inaandikwa hivyo?
 
Hv viganja mnavoonyesha mbna mi siioni hio M
Maisha Kuna bahati sawa ila bidii ni muhimu sana,changanya bidii na bahati
Bidii inahitajika kwa sana sio kulala tu tumbo juu
 
Nyie ndiyo mnaoua watu wengine kwa kisingizio cha utajiri. Huyo mganga kakudanganya na ukiendelea kumsikiliza atakuingiza matatani.
 
Back
Top Bottom