Hivi ni kweli kuwa wenye herufi "M" kwenye kiganja wana bahati sana?

Hivyo viganja kuna kipindi vilikua bonge la deal hapa kijijni kwetu. Ukiwa na M mkononi muda woooote ni kukunja ngumi unless otherwise wanaume wanaondoka na kiganja kama sio mkono mzima
Mkuu umenipa raha, mtu unatembea umekunja ngumi
9c3f798a0c99a8a714ff2b19091d8b86.jpg
vipi na Mimi nipo wakuuu?
 
Naamini katika kujituma kufanya kazi sahihi kwa bidii na mpangilio na kwa wakati! sitaki uamini kama mimi lakini mambo mengine ni ya kipuuzi sana, ndo maana watu wengi wamebweteka bila kujishughulisha katika shughuli sahihi na kwa bidi wakiamini watatoka (One day yes!)
 
ninayo 'm' mkono wa kulia,I play my part to create my own luck , kama ulivyo ujumbe wa signature yangu
 
Maskini haishiwi ndoto. Unajua pale unapokuwa huna kitu mfukoni akili huwa inafanya kazi sana kujua ni namna gani mambo yatakuwa sawa. Mipango ikigoma ndio basi mawazo ya faraja hutujia.. Mf nikitoka nikitembea naweza nikaokota hela... Unakuta mtu anatembea road anatoa macho kwenye kila karatasi atakayoiona.. Na mengine ndio kama hayo ya kuwa na "M"
 
Hebu ngoja kwanza niangalie cha kwangu.

Nimeshawahi sikia, sema sijawahi kuangalia kiganja changu hata siku moja.

Ngoja kwanza, basi nimeghairi
 
Watanzania kutokuwa na elimu hasara yake ndiyo hii tunategemea kusaidiwa tu, alaf kuna mijitu mingine inatabia mbaya mno inanguvu ya kufanya kazi lakini haichoki kuomba omba, kila ukikutana naye ni kuomba tu!
 
Mawazo ya kimaskini haya.

Mkuu hapo umenena, unajua watu wenye fikra za namna hii ni wale wanaotafuta utajiri wa haraka haraka bila kujishughulisha, anatamani hata akaibe, au kamari ilimradi tu atoke kimaisha, huu ni upumbavu kabisa, na ndiomaana pesa za namns hiyo huwa hazina baraka, hata uibe mil 100 zitakwisha muda mfupi tu.
 
Waswahili wana msemo, lisemwalo lipo.
Ni mara nyingi Sana nimekuwa nikisikia tetesi kuwa, watu wenye viganja vyenye alama ya "M " wana bahati Sana, Kwa upande wangu mimi ni muumini mzuri sana Wa Mungu, ila mkono wangu wa kulia una alama ya "M " wa kushoto hauna, binafsi nimekuwa na bahati Sana ktk maisha yangu, na hili nimeanza kuamini kuwa ni kweli kiganja chenye "M"ni bahati kubwa ukiwa nacho.
Nakumbuka ilikuwa 5/january/2012 nilipoamka asubuhi nyumbani nikiwa Sina hata cent, chakula ndani kilikuwa kimeisha, na sukari ilikuwa hamna, nilikuwa nimechanganyikiwa kabisa maana biashara yangu ilianguka
ilipotimia saa 2:30 asubuhi ile, simu yangu iliita, namba Ilikuwa ngeni, nilipokea na sauti ya kike ikasikika, ilikuwa ni girlfriend wangu Wa zamani anayeishi Kwa sasa Canada, alikuwa amekuja Tanzania bila kunitaarifu, yeye tayari ana uraia wa Canada na kaolewa na mzungu, alikuwa Amekuja kusalimia ndugu zake Arusha, nikaongea naye mambo mengi kisha nikamtania Kama kumjaribu anikumbuke basi hata hela ya soda, akaniambia nisubiri kidogo, nami nikaondoka kwenda kuhangaika angalau nipate hata pesa ya kununulia hata unga, ilipotimia saa 5 nikawa nimerudi nyumbani na sh 5000 tu niliyokuwa nimepewa na rafiki yangu.
Nikamkuta Mke wangu amechuma kisamvu anakichemsha bila kujua kitaliwa na nini.
Nikampatia ile elfu 5,nikakaa ndani nikiwa na mawazo ile mbaya, nikisubiria msosi nile, ilipotimia saa 6:30 mchana, sms ikaingia kwenye simu yangu, nilipotazama ilikuwa ni m pesa, yule girlfriend wangu alikuwa kanitumia sh 950,000 ,moyo wangu Ulienda kasi Kwa mapigo yaani sikuweza kuamini, nikahisi labda alikosea tu, nikatoka mbio ndani kwenda kutoa ile pesa, akawa ananipigia sipokei, baadae akatuma sms nadhani umepata pesa niliyokutumia, sikujibu, wakati nakaribia kwenye kibanda cha m pesa ili nitoe pesa, nikaokota pochi iliyokuwa imetuna na kuiweka mfukoni.
Nilizitoa pesa Haraka Sana, kisha nikamtaarifu kuwa nimepata na kumshukuru Sana, wakati narudi nyumbani nikaitazama ile pochi kuona ni kitu gani kilikuwemo, Duh! sikuamini tena, pochi haikuwa na anuani wala ID yoyote, ilikuwa na sh laki mbili, Kwa kweli sitaisahau hiyo Siku.
Siandiki kuwa furahisha watu, bali ni kweli tupu.
Tangia kipindi hicho hadi leo, kila nalofanya linakuwa.

Kiganja changu

Hujatuambia huyo girlfriend wako ilikuwaje kuwaje mpaka akakutema, then akaolewa na ZUNGU? Dah shida hizi jamani
 
Mleta uzi unaota ndoto za mchana. ..si ajabu utakuwa ni mpiga ramli wewe!
 
pigeni kazi acheni imani za kusadikika!! Ni kazi tu ndio mkombozi wa maisha yako.
 
Waswahili wana msemo, lisemwalo lipo.
Ni mara nyingi Sana nimekuwa nikisikia tetesi kuwa, watu wenye viganja vyenye alama ya "M " wana bahati Sana, Kwa upande wangu mimi ni muumini mzuri sana Wa Mungu, ila mkono wangu wa kulia una alama ya "M " wa kushoto hauna, binafsi nimekuwa na bahati Sana ktk maisha yangu, na hili nimeanza kuamini kuwa ni kweli kiganja chenye "M"ni bahati kubwa ukiwa nacho.
Nakumbuka ilikuwa 5/january/2012 nilipoamka asubuhi nyumbani nikiwa Sina hata cent, chakula ndani kilikuwa kimeisha, na sukari ilikuwa hamna, nilikuwa nimechanganyikiwa kabisa maana biashara yangu ilianguka
ilipotimia saa 2:30 asubuhi ile, simu yangu iliita, namba Ilikuwa ngeni, nilipokea na sauti ya kike ikasikika, ilikuwa ni girlfriend wangu Wa zamani anayeishi Kwa sasa Canada, alikuwa amekuja Tanzania bila kunitaarifu, yeye tayari ana uraia wa Canada na kaolewa na mzungu, alikuwa Amekuja kusalimia ndugu zake Arusha, nikaongea naye mambo mengi kisha nikamtania Kama kumjaribu anikumbuke basi hata hela ya soda, akaniambia nisubiri kidogo, nami nikaondoka kwenda kuhangaika angalau nipate hata pesa ya kununulia hata unga, ilipotimia saa 5 nikawa nimerudi nyumbani na sh 5000 tu niliyokuwa nimepewa na rafiki yangu.
Nikamkuta Mke wangu amechuma kisamvu anakichemsha bila kujua kitaliwa na nini.
Nikampatia ile elfu 5,nikakaa ndani nikiwa na mawazo ile mbaya, nikisubiria msosi nile, ilipotimia saa 6:30 mchana, sms ikaingia kwenye simu yangu, nilipotazama ilikuwa ni m pesa, yule girlfriend wangu alikuwa kanitumia sh 950,000 ,moyo wangu Ulienda kasi Kwa mapigo yaani sikuweza kuamini, nikahisi labda alikosea tu, nikatoka mbio ndani kwenda kutoa ile pesa, akawa ananipigia sipokei, baadae akatuma sms nadhani umepata pesa niliyokutumia, sikujibu, wakati nakaribia kwenye kibanda cha m pesa ili nitoe pesa, nikaokota pochi iliyokuwa imetuna na kuiweka mfukoni.
Nilizitoa pesa Haraka Sana, kisha nikamtaarifu kuwa nimepata na kumshukuru Sana, wakati narudi nyumbani nikaitazama ile pochi kuona ni kitu gani kilikuwemo, Duh! sikuamini tena, pochi haikuwa na anuani wala ID yoyote, ilikuwa na sh laki mbili, Kwa kweli sitaisahau hiyo Siku.
Siandiki kuwa furahisha watu, bali ni kweli tupu.
Tangia kipindi hicho hadi leo, kila nalofanya linakuwa.

Kiganja changu
sasa apa tunatamanisha tu maana mii nashika mpunga mwing afu sio wangu afu kiganja changu kina M inakalibiana na N aya bwana kila mtu na riziki yake
 
Huu ujinga muache kufanya kazi mtegemee viganja. Hivi waafrika mlilogwa??? Ndo maana hili bara likaitwa bara la giza duuh majanga... karne ya 21 watu wana mawazo mgando namna hii.
 
Back
Top Bottom