Hivi ni kweli kuwa wenye herufi "M" kwenye kiganja wana bahati sana?

Ni Mungu tu ilifikia mahali aliachia baraka zake kwako mkuu,sina uhakika sana na sijawahi kufanya research ila naamini karibu aslimia 90 ya binadamu wana hiyo herufi M kwenye mikono yao including me na sidhani kama ina maana yoyote.
 
Mi nilisikia wazee wakisema, ukikuta mtu ana hiyo alama basi ujue kuwa kwenye uzao wao[Tumbo moja katika familia] wakwanza kuzaliwa ni mtoto wa kiume, tofauti na hiyo alama wakwanza katika huo uzao ni mtoto wa kike.
 
...waswahili bana...watu wa kutafta shortcuts kwa kila jambo....wakitoka kwenye viganjwa wataamia kwenye K fupi na ndefu n.k n.k....fanyeni kazi kwa bidii mtoke...tofauti za viganja ni sawa na tafauti za ufupi na urefu wa watu...ama unene na wembamba.....ni maumbile tu.....
 
Haya ni matokeo ya unajimu na utabiri. pia yawezekana kuhusishwa na ushirikina. Mafanikio ya kweli utayapata kwanza kwa iumtegemea na kumwomba Mungu. pili jitihada zako binafsi kama kujiendeleza kielimu au kujituma ktk kazi au kuwa mvumilivu au bidii ktk kazi au mipango mizuri na kuepuka matumizi mabaya ya rasilimali, lakini zaidi ya yote utafanikiwa ikiwa una sifa nyingi ktk hizi nilizozitaja. tuachane na herufi za kiganjani kwani ni sawa na kuturudisha kwenye utawala wa JK
 
...exactly....hata Mungu huwa anawasaidia wanaojisaidia....kuna watu wanashinda makanisani huko wakitafta upako na kuacha kufanya kazi....na matokeo yake wamebaki kuwa maskini wa kutupwa...huku wakiwapelekea hao manabii hata kile kidogo wanachopata....
 

Acha huo Ushirikina. Unawapa watu matumaini ya uwongo.
 
h
hata sie wenye majina yanayoanza na herufi M.
 
Sio kweli. Mi ninayo na nina changamoto kibao!
 
Dah.. ebwana sasa hapo "M" iko wapi? Mie naona kama ipo "yǒu" ya kichina tu. Wewe lala tu nyumbani na "M" usubirie wakuletee
 
Muache kuwateka watu akil hiyo sayance hamna juhudi zako ndo mafanikio yako...acha kujishulisha ukifuatlia herufi M za mikono
 
AISEE MAMBO YA KUFIKIRIKA HAYA WEWE ULIONA WAPI HERUFI INA BAHATI WAKATI
INABIDI UTAFUTE KWA JASHO LAKO NDO UPATE AISEE MAKUBWA MADOGO YANA........................
 

Hiyo si bahati ni wizi tu unakusumbuwa, si ungetangaza hayo maeneo, tena hii ishu si ya siku nyingi kwa kuwa inahusu M-Pesa ina maana redio zilishakuwepo zenye huduma ya ukarimu, ungeenda hata huko kumtafuta mwenye pochi yake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…