Hivi ni kweli kwamba huwezi kuwa tajiri kama umeajiriwa au unamfanyia kazi mtu?

Unaweza ukawa Tajiri kwa kuajiriwa kwa njia mbili kubwa :-

1. Uwe unalipwa mshahara mkubwa sana.
2. Uwe una matumizi madogo sana, kutoka kwenye huo mshahara.
Kisha ufanye kazi kwa muda wa maisha yako yote. Otherwise, sahau kuwa tajiri kwa kutegemea ordinary paycheck.
Kama nakuelewa hv mkuu [emoji817]
 
Nautamani huo Umri wako aisee, yaani na huu ufahamu nilonao sasa kutajirika hata kama ingeshindikana ila ningekuwa napigania Kombe Moja tu .... 🤗
Tupe basi madini.ungefanyaje mimi pia nina age 22 napambania kombe mjini hapa
 
Unaweza ukawa Tajiri kwa kuajiriwa kwa njia mbili kubwa :-

1. Uwe unalipwa mshahara mkubwa sana.
2. Uwe una matumizi madogo sana, kutoka kwenye huo mshahara.
Kisha ufanye kazi kwa muda wa maisha yako yote. Otherwise, sahau kuwa tajiri kwa kutegemea ordinary paycheck.
Pia ajishughulishe na Mambo mengineyo tofauti na hayo kwani Kuna kufukuzwa kazi pia
 
Kwema wakuu?

Mimi ni kijana wa miaka 20 na ndo kwanza nimeanza maisha ya kujitegemea na ndoto yangu ni kuwa tajiri siku moja.

Nimekua nikisikia baadhi ya watu hasa hawa motivational speakers wakisema kuwa huwezi kutajirika kama utafanya kazi za kuajiriwa tu na hii imenifanya kuona kama sipo kwenye njia sahihi ya kutimiza ndoto yangu.

Imekaaje hii wadau, kuna ukweli ndani yake?
Kwani kujiajiri nako si kuajiriwa?
 
  • Tajiri aajiriwi, bali yeye ndio anaajiri (anatoa ajira).​
  • Kama umeajiriwa, tumia hicho kipato kama mtaji kwa muda fulani; kisha nenda kafanye mambo yako ya kujijenga kitajiri/kujiajiri.​
  • Tunatamani sana tukuone unanunua mgodi, unajenga viwanda, unaenda kuwekeza nje n.k​
  • Pambana kutimiza ndoto zako​
 
Kabla hujatuuliza hilo swali tuoneshe tajiri mmoja tu ambaye unamfahamu ameajiliwa.

Halafu hakuna tajiri wa umri wako labda wa kurithi au land of opportunity kama Marekani.

Kwa nchi za dunia ya tatu una miaka mingine 20 ya kuukaribia utajiri kama utafanikiwa kujiajiri Kwa mafanikio.
Mkuu Shabiby alinunua gari yake ya YuTong akiwa na miaka 19 kwhy usimtishe eti kisa umri wake mdogo
 
Kwa nchi za ulimwengu wa kwanza ni wengi wameajiriwa na ni matajiri kama wana michezo mbali mbali au mtu kama Sundar Pichai CEO wa google kwa hapa kwetu fanya utafiti.
 
Kwema wakuu?

Mimi ni kijana wa miaka 20 na ndo kwanza nimeanza maisha ya kujitegemea na ndoto yangu ni kuwa tajiri siku moja.

Nimekua nikisikia baadhi ya watu hasa hawa motivational speakers wakisema kuwa huwezi kutajirika kama utafanya kazi za kuajiriwa tu na hii imenifanya kuona kama sipo kwenye njia sahihi ya kutimiza ndoto yangu.

Imekaaje hii wadau, kuna ukweli ndani yake?
Hata nikiiba?🤔🤔
 
Una probability kubwa ya kuwa tajiri. Kama umeanza kuyaona mambo haya kwa umri huu (kama umesema kweli, maana wengine wanadanganya umri), kama una nia, hapana shaka utatumia muda wako na rasilimali utakazojaliwa kuutafuta utajiri. Siku zote penye nia kuna njia, tunakutakia kila la heri katika kutimiza ndoto yako ya utajiri. Kikubwa, unatakiwa kuijua thamani ya pesa hata iwe ndogo kiasi gani, kwani hiyo pesa ndogo ndio hukua na kuwa kubwa. Usitumie pesa ovyo, hata watu wakisema wewe ni bahili, usijali bali angalia malengo yako. BE AGGRESSIVE ON MONEY!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si kweli. Inategemea na jinsi unavyotumia kipato chako, je unajiwekea akiba ambayo ikiwa nyingi utaweza kufanya uwekezaji? Au kila ipatacho huishia viti virefu kuipombea na kuifuskia?
Uamuzi ni wako!
 
Una probability kubwa ya kuwa tajiri. Kama umeanza kuyaona mambo haya kwa umri huu (kama umesema kweli, maana wengine wanadanganya umri), kama una nia, hapana shaka utatumia muda wako na rasilimali utakazojaliwa kuutafuta utajiri. Siku zote penye nia kuna njia, tunakutakia kila la heri katika kutimiza ndoto yako ya utajiri. Kikubwa, unatakiwa kuijua thamani ya pesa hata iwe ndogo kiasi gani, kwani hiyo pesa ndogo ndio hukua na kuwa kubwa. Usitumie pesa ovyo, hata watu wakisema wewe ni bahili, usijali bali angalia malengo yako. BE AGGRESSIVE ON MONEY!

Sent using Jamii Forums mobile app
Agreed [emoji817]
Bonge la ushauri.....me mwenyewe naendelea kusimamia misingi hii
 
Hivi ili uitwe tajiri,lazima uwe unamiliki pesa kiasi gani? au uwe unamiliki vitu gani?
 
Huwezi kuwa tajiri kwa kuajiriwa kwasababu chanzo kikuu cha kipato ni mshahara, marupurupu na posho za hapa na pale ambazo hazitaweza kukupatia utajiri - labda uibe kwa aliyekuajiri au mahali pengine.

Hivyo, inategemea kwako wewe utajiri ni nini au una maana gani? Ukishapima kiwango cha utajiri unachotaka kukifikia, basi jiulize Je, unaweza kuufikia utajiri huo kwa kuajiriwa au inabidi ujiajiri? Mshahara utakuwa kiasi gani? Utakuwa unatumia muda kiasi gani kufanya kazi yako ya kuajiriwa? Kama unataka kumiliki nyumba nzuri kwa ajili ya familia na gari moja au mawili kwa ajili ya kutemmbelea au biashara, hayo ni mambo unayoweza kuyafanya kwa urahisi ukiwa umeajiriwa, ingawa huo si utajiri. Lakini ni vigumu kumiliki biashara kubwa, kiwanda, mgodi , au wazo kubwa litakalowezesha kuwaajiri mamia au maelfu ya watu uliowaajiri watakokuwa chini yako, hapo ndipo kuna uwezekano wa kuwa tajiri. Huwezi kufanya au kusimamia au kumiliki miradi au biashara kubwa kwa kuajiriwa kwasababu muda wako mwingi kama si wote utakuwa ukiutumia kumtumikia mwajiri wako badala kujijengea utajiri wako. Hivyo, mwajiri wako ndiye atakayekuwa tajiri na SI WEWE.
 
Inategemea umeajiriwa wapi na katika nafasi gani.
Kwema wakuu?

Mimi ni kijana wa miaka 20 na ndo kwanza nimeanza maisha ya kujitegemea na ndoto yangu ni kuwa tajiri siku moja.

Nimekua nikisikia baadhi ya watu hasa hawa motivational speakers wakisema kuwa huwezi kutajirika kama utafanya kazi za kuajiriwa tu na hii imenifanya kuona kama sipo kwenye njia sahihi ya kutimiza ndoto yangu.

Imekaaje hii wadau, kuna ukweli ndani yake?
 
Sahihi Marekani land of opportunity ina matajiri wengi sana waliotokana na kuajiriwa.

Back
Top Bottom