Hivi ni kweli mtu anaweza kuendesha maisha yake kwa kutegemea betting tu?

Hivi ni kweli mtu anaweza kuendesha maisha yake kwa kutegemea betting tu?

Uki-refer tu hilo neno betting - kamari basi utagundua kua hata ukitaka kutegemea huo mchezo kama ajira basi maisha yako yakua yakubeti pia xo inawezekana maana maisha nikuchagua.
 
Kumbe unajua mkuu

Kampuni za betting kwanza kabisa haziweki ligi dhaifu na wakiziweka basi wana limit stake

Timu inayoshinda kila game haiwezi kukupa hela kwasababu odd zake zitakua ndogo mmno 1.05…. Uta stake sh ngapi upige hela?

Kampuni za betting sio wajinga odd nzuri utazipa kwenye game ngumu kutabiri matokeo, game rahisi wanafinya odd

Hapa Bongo weekend ulikua ukichukua Simba Yanga na Azam Win odd hazifiki hata 1.5
Lakini Polisi Vs Namungu Odd 2.3 kwa odd 2.1
Uongo, nimebetia yanga na simba mechi nyingi tu msimu huu na odds azikuwa ndogo hivi usemavyo UONGO.
 
Ul
Mkuu nimebet sana sana najua ninachokwambia

Kwenye betting kuna KUBAHATISHA tu
Hakuna odd ndogo za UHAKIKA…… HAZIPO

Unavyoa andika “mtu anatafua odd zake 1.5 anatia mzigo” ni as if ni guarantee

Kwanini uandikie mate wakati wino upo mkuu
Wewe hutaki hizo hela za bure bure kwenye betting kwa kuanza kuijua ligi ya bongo ukapiga hayo mahela?

Fainali na Chelsea Nilimuomba PSG goli moja tu Odd 1.2 laki yangu ikapotea kama upepo vile
Yaani sio washinde, wapate goli tu lakini kilichotokea sasa
Ulichosema ni ukweli mtupu asikiae na asikie, bora ukalime matikiti jangwani lakini sio kubeti.
 
Huyo jamaa Sativa17 mikeka yake mingi inatiki,anaweka mzigo laki tano au milioni moja anakula mara mbili....ata mkeka ukichanika bado hana hasara mara anakula sana
Dio kama Mimi naweka
1000176481.jpg
 
Kuna league huko asian, league za chinichini kuna timu huwa zinashindaga tu.....hii ni kweli kabisa
ligi mojawapo ni ligi kuu ya Malaysia. pale kuna timu inaitwa Johor Darul. yenyewe inashindaga tu. changamoto ni odds zake za kushinda, haizidi 1.1, ni 1.01 mpaka 1.09
 
Kusema tu ukweli kwa namna fulani inawezekana, mimi kuna kipindi nilikata tamaa kabisa na maisha, nikawa nabeti nakumbuka ni 2024 mwezi wa 7 hapo nilianza na 30000 lakini kufika mwezi wa 8 nilikuwa na 2,800,000 huu ulikuwa ni mtaji mkubwa sana kwangu wa kuanzia maisha.
Nilikuwa nabeti mechi za live game mojamoja tu kuanzia asubuhi hadi kesho asubuhi yaani masaa 24 na kipindi hicho upepo uliniendea vizuri 1000000 ya kwanza nilifanikiwa bila kuchaniwa mkeka hata 1😂 kampuni ilikuwa ni 1xbet.
 
Inawezekana tena sana. Na akipiga hesabu huenda kwa alicho ingiza kinawazidi wengi walio ajiriwa.
Kwenye kubett wengi hufail kwa ajili ya mtaji na tamaa ya kupata kikubwa.
 
Kuna yule jamaa kule twitter anaitwa Sativa17... nilikuwa nafuatilia video yake akielezea jinsi alivyotekwa na kunusurika kufa baada ya kupigwa risasi ya kichwa.

Aliulizwa anafanya kazi gani akadai anafanya betting ( michezo ya kubashiri ) tu, hafanyi inshu nyingine yoyote na kupitia hiyo betting ndio anaendesha maisha yake.

Sasa nimetafakari, hivi ni kweli hii? mtu anaweza kuishi kwa kupitia betting bila kufanya shughuli nyingine za kumuingiza kipato.

NB😛 pia huyo jamaa ni most wanted na watekaji wa nchi hii ( kwa madai yake mwenyewe ), so inawezekana kwa sababu kazi yake ni hiyo ya betting inamsaidia asikamatwe na watekaji?
Iwapo ccm inaweze,je unafikiri ni raia gani atashindwa kuishi kwa njia hiyo?
 
Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
 
Betting sio kazi ukitaka kuchanganyikiwa na maisha tegemea Betting kuendesha maisha.
Mara 10 hata muokota makopo at the end of the day u have assurance kuwa utapata kitu
Sio kazi then ni nini bei specific
 
Back
Top Bottom