Hivi ni kweli mtu anaweza kuendesha maisha yake kwa kutegemea betting tu?

Hivi ni kweli mtu anaweza kuendesha maisha yake kwa kutegemea betting tu?

Inawezekana sana sema tu hujakutana na watu tofauti tofauti wenye akili nzuri na maisha ya kiaina. Cha msingi usiwaige.

Ila kubeti kila siku sijawaona, wanabeti kwa msimu na kwa wiki siku kadhaa tu kwa stake kubwa. Na si kila anayepata hela uko anaweka stake. Wengine wanauza odds kwa mbumbumbu wanaokurupukia hela za haraka, wengine wanafanya matangazo ya makampuni ya kubeti, wengine wanafanya udanganyifu kwa edit ya stake na wins, wengine wanajihusisha na mitandao ya kupanga matokeo.

Sio kubeti tu, nimekutana na vijana wanaopata hela kwenye mambo ambayo huwezi dhania.
Mambo yapi hayo?
 
Kubeti sio kazi. Nistsrehe ukitaka kujua sio kazi unaweza kupata hata milion 60 na ukairudisha ndani ya muda mfupi tu. Ndio maana wewe ukishinda hawaoni shida kukulipa wanajua vile umeshinda utadhani utashinda tena ndio wanakupiga vizuri kwahiyo hamna namna eti utasema unaweka pesa kubwa odds chache . Imagine umeweka 1M ili ushinde 1.5 , kesho unaweka 1M unapoteza yote kiuhalisia imeshabaki na lost ya laki 5
Ukweli upo hapa.
 
_20250722_134055.JPG
 
Betting ni biashara ya pesa nyingi sana . Hujawa specific kuwa anaendesha maisha yake kwa biashara ya betting ama kubeti. Kama nikubeti nikiti kigumu pengine kisichowezekana lakini kama ni biashara ya betting inaweza kumuingizia pesa ambayo pengine hata ukoo wenu hakuna ambaye amewahi kuishika. Letsay anafanga mojawapo ya hizi kazi 1. Influencer wa kampuni za betting, affiliate marketing, social media marketing hiI zote zinaweza kuendesha maisha yake kwa kiasi kikubwa ukizingatia ana follower wakutosha
Umefafanua vizuri sana mkuu
 
Kuna jamaa mmoja namfahamu kila siku alikua anakula laki ndani ya wiki na nusu akaja akamalizia na laki 5 nikasema kazi ndio hii, ghafla alikua vyuma mfululizo akatangaza kuacha ku-bet
 
haya na sisi tunaokwenda kwa mchina na 200 na kuroka na 60k tunacomment wapi
 
tukumbuke ni michezo ya kubahatisha na sio kila siku mtu ana bahati....... na betting sijawahi jua 4mla yake
 
Hapana mkuu ila unaweza tu kuendesha maisha yako kwa kumtumaini na kumtegemea mwamba mkombozi wa waislamu kipenzi chetu cha dhati Imam Hussain ibn Ali A.S aliyeuwawa kikatili kuutetea, kuulinda na kuupigania uislamu dhidi ya dhulma, ukandamizaji, unyanyasaji na uonevu.

Mcheki mwamba hapo Chini kwenye battle of Ashura.

View attachment 3412964View attachment 3412965View attachment 3412966View attachment 3412967
We utakua MSHIA 😂

Washia wanajua sana kuhadithia hekaya za huyu mwamba
 
Ukikutana na wale magwiji jibu ni ndiyo... japo niseme kwa Tanzania sidhani kama wako. Kuna watu wanatumia software special kufanya analysis na wanatumia mikakati mingi sana. Vingenevyo: swali lako ni rahisi sana kujua jibu lake kama ukidhamiria. Kwa vipi? Tenga fedha eg sh milioni 50, kichwani mwako. Yes, fikiria kama una sh milioni 50 japo huna. Anza kubet kinadharia kama vile una bet fedha za kweli. Yaani kukiwa na mechi jifanye unabeti kiasi fulani halafu matokeo yakitoka toa au ongeza utakachopata kwenye betting yako ya nadharia. Ni muhimu sana uwe na nidhamu na ufanye kama unabet kikweli na usibet kila siku. Bet zile siku ambazo una uhakika kwa asilimia kubwa kuwa utashinda na andika kabisa mahesabu yako kwenye daftari kama unafanya jambo la kweli. Baada ya eg miezi sita au mwaka, angalia, utakuwa umepata au kupoteza kiasi gani?
Hapana ushasema kinadharia hivyo ni ngumu kuweka umakini kwa 100%,,kama ukiweka pesa truly
 
Kuna dogo namfahamu amemjengea Mama yake nyumba Tanga na yeye kajenga mbagala kwasababu ya betting, kwasababu yeye kwao ni waislam, hakuna anayejua, wanadhani ni kazi yake kwenye kampuni ya Muhindi 😀,ila dogo anafuatilia hadi bingwa wa Tajikistan, Jamaica au nchi yoyote ambayo wewe hujawahi ifikiria..... anaweza kukupa top five.......
 
Back
Top Bottom