Kuna yule jamaa kule twitter anaitwa Sativa17....nilikuwa nafuatilia video yake akielezea jinsi alivyotekwa na kunusurika kufa baada ya kupigwa risasi ya kichwa.
Aliulizwa anafanya kazi gani akadai anafanya betting ( michezo ya kubashiri ) tu,, hafanyi inshu nyingine yoyote na kupitia hiyo betting ndio anaendesha maisha yake.
Sasa nimetafakari,, hivi ni kweli hii??,, mtu anaweza kuishi kwa kupitia betting bila kufanya shughuli nyingine za kumuingiza kipato.
NB😛pia huyo jamaa ni most wanted na watekaji wa nchi hii ( kwa madai yake mwenyewe ),,, so inawezekana kwa sababu kazi yake ni hiyo ya betting inamsaidia asikamatwe na watekaji??