Hivi ni kweli serikali haifahamu kero ya usafiri wa mabasi ya Mwendokasi?

Hivi ni kweli serikali haifahamu kero ya usafiri wa mabasi ya Mwendokasi?

Poleni sana wananchi wa Ukanda wa Mbezi Yale ni mauaji
 
Yaan watu wa CCM wanafiki sana,mradi au kitu chochote kikifanya vizuri,MAMA ANAUPIGA MWINGI,ila kikiwa kibovu,mfano TANESCO,au barabara Mbovu,ccm haihusiki ni watu wengine wanaohusika.
Rubish
Ukiona sehemu yenye pesa haiendi vizuri ujuwe kuna wezi.
 
Sasa ukiwa mfupi watu wanavyobanana unaishia kunusa harufu ya vikwapa [emoji2]
Haya maisha haya bhana
 
Huu usafiri wa Mwendokasi ni kero sana na sio kwamba Hawaoni lakini wameamua kulifumbia macho hili jambo yaani utadhani watu huwa wanapanda bure yale magadi. Masaa matatu unasubiri usafiri halafu hata mabasi yakifika yanapaki pembeni bila hata kuwaonea huruma Wananchi. Kwa kweli huduma ya usafiri wa Mwendokasi ni janga tupu.
 
Dar ni sehemu ngumu sana kuishi kama kipato chako ni cha wastani

Cha msingi kama bado hujajenga ni vizuri ukaishi karibu na sehemu unapofanyia shughuli zako ili kuepukana na vurugu za usafiri.
 
Serikali kwa nini isiingilie kati inunue mabasi kama mwekezaji hana uwezo? Nakumbuka jirani zetu Rwanda wananchi wamelalamika kwamba kulikua na uhaba wa mabasi ya abiria katika jiji la Kigali, sasa serikali yao Imenunua mabasi 200 ili kusaidia wananchi wapate usafiri bila shida.
 
Kwani viongozi hao wanautumia huo usafiri
They don't care,nyie mkanyagane ,mbambiane humo,mjambiane,mchelewee usafiri,wao they don't give a f----

Ova
 
Yaan kiukweli ile njia ya mwendokasi ni kheri tungejenga fly over ya toka kimara to posta, speed ingekuwa ni not less than 50 Km ingekuwa ni tosha kabisa
Serikali ya CCM wanajuwa haya toka tumepata uhuru mwaka 1961 lakini utashangaa kila zama / awamu inayokuja ujinga ni ule ule na hakuna rais anayeshituka, wanaona sawa tu.
 
Samia akisikia malalamiko anachojua ni kutengua na kuteua Mkurugenzi Mtendaji tu.
 
Back
Top Bottom