Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndiyo tupewe tu pesa 😜Ndugu usiwakopeshe wape tu hela Kama unataka undugu udumu .
Ukiachana na hilo MTU yeyote mkopeshe kiwango au kiasi ambacho UPO tayari kukipoteza.
Hana kwa wakati huo ila akipata atairudishaMwenzenu Mangi nimepigwa na kitu kizito. Yaani siamini. Nimekuwa na kiherehere cha kuwatetea wanawake kwenye karibu kila nyuzi zinazomponda mwanamke lakini hivi karibuni nimepigwa tukio hadi fikra zangu zimeyumba. Naomba wanawake mtanijibu maswali hapo chini lakini wanaume wenzangu mnisaidie pia kujibu.
Ni hivii kuna dada nilikutana nae kwenye shughuli maalumu ya kikazi ambako lilitukutanisha wafanyakazi wachache wa idara moja. Baada ya shughuli ya kikazi kuisha liliundwa group la umoja wa kuendeleza mahusiano baada ya kazi kuisha kwa maana ya shida na raha.
Uhusiano wa kirafiki uliendelea kati ya wanagroup tukichati mara Kwa mara na kuweka mipango ya kusaidiana.
Sasa siku moja huyo dada alinitumia meseji akiniomba nimkopeshe kiasi fulani cha pesa.Aliniahidi kunirudishia baada ya siku kadhaa.Kwa kuwa nilijua ni rafiki na tupo nae group moja sikumbania.Nilipomkubalia na kumuuliza nimtumie kwa njia gani? Alifurahi akaniomba nimuongezee kiasi zaidi ya kile alichoomba. Hapa Mangi nilisita kidogo nikamdanganya kuwa kuna mtu mwingine nilishamuazima ila angewahi kidogo tu njngempatia.
Mapichapicha yakaanza sasa baada ya siku ya kurejesha kufika. Nakumbuka nilichelewa kama siku mbili hivi kumuuliza kuhusu kinirejeshea fedha zangu. Yaani ni kama alijikausha akisikilizia kama nitamshtua au?
Baada ya kumtumia ujumbe akanijibu usjali niko kwenye kikao fulani nitakutumia baada ya kikao kwisha.. Nikamjibu poa. Mara siku ikaisha ikawa usiku ikawa mchana kajikausha. Kesho yake nikampigia hakupokea. Nikamtumia ujumbe akanijibu nitakutumia leo usjali.Nikaona isiwe tabu nikamsikilizia lakini wapi.Nayo ikapita ikawa usiku ikawa mchana.
Hiyo keshokutwa sasa nikawa nampigia hapokei basi nikaamua kumuandikia meseji moja tu kuwa naomba unirudishie hiyo fedha yangu siku yoyote utakayoona inafaa.Kumbuka hapo zimeshapita siku nne tangu ile siku aliyoniahidi.
Baada ya kumtumia hiyo meseji hajawahi kunijibu wala kunitumia fedha yangu.
Hii ni wiki ya pili sasa.Nahisi alifurahi na kusisimka sana baada ya kuona ule ujumbe wa mwisho.Kuwa sasa huyu fala kashanikatia tamaa.
Hivyo ndivyo jinsi nilivyopigwa hadi siamini maana ukimuona huyo dada huwezi mdhania ukimlinganisha na kazi anayofanya.
Sasa naomba niwaulize wanawake lakini pia na wanaume wenzangu maana nakaribia kukosa imani na mwanamke yeyote.
1)Hivi huyu dada atakuwa ni tapeli au ni aina ya wale wanawake wanaofikiri ukimkopa mwanaume ni kama umechukua msaada na hivyo haupaswi kurudisha tena?
2)Je huyu mwanamke ndio Ile aina ya wanawake ambao kwao kurejesha mkopo ni kutarajia mkopeshaji alegee na kumtaka kimahusiano ili rejesho lifanyike kwa njia isiyo rasmi.?
3)Je wanaume tukiwakopesha wanawake hatupaswi kuwadai maana ni haki yao kupewa(kama si kuhongwa) fedha na wanaume?
3)Je, kumdai mwanamke fedha ni kujishusha na kujidharaulisha uanaume wako?
4)Je, ni kweli kuwa mwanamke kukupa hela yake ni ngumu kama ngamia kupita tundu ya sindano lakini mwanamke kuipata hela ya mwanaume ni rahisi kama kumsukuma mlevi.?
Naombeni majibu yenu ili tu nirekebishe mtazamo wangu.
Asanteni.
Karibu.Kama nimekuelewa vile ndio maana nilistop kumfuatilia maana mwisho wake naweza kuzushiwaUsikopeshe mtu kama huna uthubutu wa kupoteza kiasi chote ulichokopesha.
Vinginevyo mkopaji aje ni hati za viapo toka mahakama kuu na ziwe na mihuri ya makama ya rufani😂😂😂😂. Vinginevyo aende benk au kausha damu.
Na kama ni lazma sana kukopesha, kopesha mwanaume maana anafaa kukoromea. Ukikopesha mwanamke hatalipa, ukimuwashia moto atajifanya ni mgogoro wa kimapenzi, na jamii itaamini hivyo.
Nitatoa visa vyangu vichache iwe ni funzo kwa wengine.
Wala sikumshobokea labda kama alijia baada ya hapo nitashoboka lakini wapi I was after my moneyAjabu mkeo/mama anaweza kukuomba ela nyumbani ukajibu sina ila mademu wa nje mnavyowashobokea sasa malipo yake ndohayo.......
Pole muhanga mwenzanguBora wewe ulikopesha mm nilipewa nimfanyie kazi tena bila hata advance, nikaipiga ile kazi nikamaliza na siku ya kumkabidhi nilikodi hadi boda boda kumpelekea. kufika pale akaniambia hela atanipa baada ya siku mbili mbele..
hizo siku mbili ni miez kadha sasa kila nikipiga sim anasema badae kesho, kesho inazaa badae inakuwa kesho tena nimedai mpka nimechoka nimeona tu nimuachie Mungu
Wanazingua sanaaA
Aise kumbe wapo wengi
🤣🤣🤣🤣 Ila Wanawakeakaniambia, siwezi kumfanya chochote yeye yuko na yesu na anajua kipato chake hakitoshi.
Yaani wewe acha tu aiseee! Ni darasa tosha🤣🤣🤣🤣 Ila Wanawake
Hana kwa wakati huo ila akipata atairudishai
Msamehe pleaseSidhani.Nimemwachia Mungu
Mkuu ata mimi kuna mmoja alinikopa laki na nusu afate mzingo akishauza ata nilipata pesa yangu mpaka sasa hivi hajanilipa na anafanya biashara na mimi sifanyi biashara.Mimi nilimkopea mmoja s
Shs 15k tu lakini hakunilipa mpaka leo alikuwa anaingiza pesa kuliko mimi.
Nimefljifunza kuishi kutokukopesha kwa mtu yeyote, kama naona kuna umuhimu wa kutoa pesa kwa mtu husika nampatia tu kiasi ambacho hakitaathiri akili yangu.