Hivi ni kweli usimkopeshe rafiki yako kama ni wa kike?

Hana kwa wakati huo ila akipata atairudisha
 
Karibu.Kama nimekuelewa vile ndio maana nilistop kumfuatilia maana mwisho wake naweza kuzushiwa
 
Ukiona mtu anakwambia umkopeshe pesa na hamna ukaribu naye sana ujue ameshakopa kwa watu wake wa karibu anaofahamiana nao sana kiasi cha kwamba amekuwa hakopesheki anaona atafute watu wapya wa kuwakopa. Bora umuazime pesa ndugu yako wa familia moja, hata asiporudisha kama mlivyokubaliana anaweza kuirudisha kivingine maana hamuachi kushirikiana.

Mtu anaomba umuazime pesa mwambie aache mali kama dhamana inayothaminishika na kiasi cha pesa anachotaka umuazime ili kutengeneza uwajibikaji kwa wote kwamba yeye ana pesa yako na wewe una tv au laptop yake akizingua unapiga bei.
 
Pole muhanga mwenzangu
 
Kisa 1
Miaka mingi kidogo iliyopita, nilikuwa nafanya miamala kwenye Mpesa moja nzurii yenye makochi ya wateja.

Hapo aliajiriwa dada mmoja anayeonekana kuwa mtulivu na msabato wa kweli. Binafsi nimekuwa nikiwaheshimu sana wasabato kutokana na busara na utulivu wao.

Mara nyingi nilikuwa nakaa kwenye kochi nikifanya miamala,na kupiga story kidogo. Siku, miezi ikasogea, tukawa tumezoeana sana.

Long story short siku moja nafika namkuta analia mwekunduuu; baadae ikabainika aliibiwa zaidi ya 1M kwa utapeli. Nikampa pole nikamuacha analia pale.

Nilimuonea huruma ila nilikuwa na uzoefu wa kuponzwa na huruma zangu huko nyuma. So nikasema ngoja nijikaushe niende zangu.

Kesho yake ananipigia, ananiambia hela iliyoibwa, bosi wake anataka alipe yeye. Boss anasema yeye hajali cha nini wala nini, anataka hela yake na yeye ana nusu tu. Hivyo anaomba nimkopeshe kiasi kilichopaki na angenirudishia mshahara wake unaofuata. Nikachomoa ki dizaini.

Baada ya siku chache baadae, ananiambia amepata ajira kwenye shirika flani ila hajalipa hela iliyopotea. Sasa wasiwasi wake ni kuwa akienda kwa mwajiri mpya, mwajiri wa mwanzo atamripoti kuwa kamuibia ndio katorokea huko; so atafukuzwa kazi kabla ya kuanza. Nikaingiwa na huruma nikamkopesha ili anirudishie akifika kwa mwajiri wake mpya

Nikamkopesha, akaanza kazi mpya, nikamsubiria miezi hatimae mwaka halipi. Hadithi tu.

Mwisho , akaniambia hanilipi maana kipato chake kidogo, nikitaka anilipe, nimtafutie kazi inayolipa zaidi ya hiyo anayofanya. Nikachukia , nikamuambia nitamchukulia hatua kali. Akaniambia, siwezi kumfanya chochote yeye yuko na yesu na anajua kipato chake hakitoshi.

Long story short ni zaidi ya miaka 5 sijalipwa, niliacha kuulizia tena deni na namba nikafuta.

Sina nia ya kulipiza kisasi. Ili niishi bila bila hasira niliamua kuli neutralize deni hilo.
 
Wapo wanawake wanaokopesheka hela na kuirudisha kwa muda wa makubaliano

Ila wengi ukimkopesha anataka akulipe " in kind"
 
Mkuu ata mimi kuna mmoja alinikopa laki na nusu afate mzingo akishauza ata nilipata pesa yangu mpaka sasa hivi hajanilipa na anafanya biashara na mimi sifanyi biashara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…