Hivi ni lazima kila raia wa Tanzania awe na kovu la ile sindano ya ndui begani?


Wazimbabwe wanayo kwenye mkono kama Watanzania, Botswana wanayo kwenye Paja, hope hata zZambia na Malawi wanazo, so sio Watanzania pekeyao
 
 
Sasa mbona unajichanganya! Mara useme hiyo ndui ya bega la kushoto ilichanjwa mwisho miaka ya 70...na ukasema kuanzia miaka ya 80 ilichanjwa chanjo ya Kifua kikuu! Ahhahahahh...

Lazima usimame na kimoja, na lazima usiwe mtu wa kulalama.
Bwana mdogo usikurupuke!hiki kizazi kina shida sana ngoja nikuelimishe ili niendelee kutimiza ahadi za mwana TANU
1.Chanjo ya kifua kikuu(BCG) inachanjwa bega la kulia na imeanza hata kabla ya miaka ya themanini ujue hili
2.Chanjo ya ndui(small pox) ilikuwa inachanjwa bega la kusho,na chanjo ya mwisho ilitolewa mwaka 1979 tangu kipindi hicho haitolewi tena kwani ugonjwa huu ulishatokomezwa duniani

Ndiyo maana sisi wa miaka ya sabini na kushuka tuna makovu 2 begani(kulia&kusho) yaani la ndui na kifua kikuu....na kizazi chako kina kovu moja tu la chanjo la TB(bega la kuli)

Pia jitahidi kutumia simu yako kujieleimisha na si kutukana baba zako humu!google utapata habari nyingi!
 
kwani hakuna uwezekano wa kutoa chanjo isiyoacha alama?
Hizo chanjo mbili lazima zitoe alama....baada ya kuchanjwa kinatokea kidonda kikipona ndo kinaacha kovu!cha msingi mjiheshimu huko mliko!mtuwakilishe vizuri!kulaumu suala la chanjo ni sawa na kumtukana mzazi wako!umesikia!huenda bila hizo chanjo ungeshakufa kwa kifaduro!sijui unajua ni ugonjwa gani?google nasi ujielimishe
 
Chanjo ya TB (bcg) kovu lisipotokea unashauriwa kumrudisha mtoto achanjwe tena
 
Bora ww maelezo yako yamejitosheleza japokua na wasiwasi na credibility ya taarifa uliyotoa huyu mtoa mada kapita juujuu sijui anakimbilia wapi
 
Bora ww maelezo yako yamejitosheleza japokua na wasiwasi na credibility ya taarifa uliyotoa huyu mtoa mada kapita juujuu sijui anakimbilia wapi
My explanations are totally credible. Just believe me[emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12]
 
Yaani hapo ndio umemaliza unafikiri ujumbe umeeleweka sio nenda kalale
 
BCG vaccine is given for protection against Tuberculosis, hiyo ndui unayosema has been eradicated for decades now. Unaposema tuangalie namna nyingine ya chajo, wewe unataka namna ipi? Basi kafanye utafiti. Sisi tunajua alama ikionekana begani basi chanjo imeingia, isipoonekana unarudia tena.
 
Chanjo ya ndui( bega la kushoto) mara ya mwisho ilichanjwa mwaka 1979....watanzania waliozaliwa miaka ya kuanzia '80 hawana alama hiyo!bega la kulia ni alama ya chanjo ya kifua kikuu!
Mkuu watu wengi hawajaenda shule, kama wameenda basi hawakuwa na bidii kujua. Kwa kifupu watu bado hawana shule
 
Hahahahahha...Heshima yako mkuu.

Naomba kuuliza; umesema chanjo bega la kulia ni ya TB, haya sawa.....sasa mbona watu hao hao waliochanjwa wanaugua hiyo TB??!?!?!?!?!!?!??!?!?!??!?!?! Unataka kusema chanjo imeFail...??!?!?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…