Kituko
JF-Expert Member
- Jan 12, 2009
- 9,555
- 9,357
Habari za muda huu wadau,
Naleta mapendekezo kwa Serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwamba ni vyema sasa tukatafuta utaratibu mwingine wa kutoa chanjo ya ndui kwa sababu za kiusalama.
Hii chanjo kwa sasa imekuwa kama alama ya mtanzania hii ni sawa na mfugaji kuweka alama yake katika mifugo jambo ambalo ni hatari sana kwa usalama wa taifa letu.
Kila mtanzania ukimkagua kwenye bega la kushoto ana alama hii ni hatari sana.
Ningeshauri Serikali kuja na chanjo ambayo haiachi alama kwenye bega kwa sababu niliyoieleza hapo juu.
Nashukuru endapo Serikali italifanyia kazi wazo langu.
Wazimbabwe wanayo kwenye mkono kama Watanzania, Botswana wanayo kwenye Paja, hope hata zZambia na Malawi wanazo, so sio Watanzania pekeyao