DiasporaUSA
JF-Expert Member
- Aug 27, 2016
- 23,382
- 29,639
Sio kweli.Kwanza ni chanjo. Pili ni alama ya utanzania.
Mimi nina docs muhimu zote za nchi hii na nilizipata bila kuwa na hiyo alama.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio kweli.Kwanza ni chanjo. Pili ni alama ya utanzania.
Chanjo ya ndui bado inaendelea kutolewa, ugonjwa ulifanikiwa kudhibitiwa kwa chanjo hiyo inayokuachia kovu na kiutaratibu kovu lisipotokea yapaswa kurudiwa tena mpaka kuwepo na kovu.
Chanjo hii ikidungwa yatarajiwa kuacha kovu mahali ilipochomwa na isipoacha kovu mzazi anatakiwa kumrejesha mtoto achomwe kwa upya mpaka itokee kovu, kuna uwezekano mzazi wako hakuzingatia hilo hivyo unaweza kuwa ulichomwa na kovu halikutokea na kuhurejeshwa kuchomwa tena....Mimi sina, shuleni sikuwahi kuona mtu ambaye hana hiyo alama ukizingatia mimi nafatilia sana. Nilidokezwa na mtu kuwa ukikosa maana yake hukupata chanjo hiyo na inamaanisha ukuzaliwa hospitali kwani ni lazima yeyote aliyezaliwa hospitali awe nayo, ni kweli sikuzaliwa hospitali. Nilimuuliza mama akadai chanjo zote nilipata but siamini sana. Lika langu wooote wana alama hii
Asante umezidi kunipa mwanga zaidi. Bahati mbaya cheti cha kliniki nilipoteza muda mrefu sana kabla sijawa na uwezo wa kutafakari mamboChanjo hii ikidungwa yatarajiwa kuacha kovu mahali ilipochomwa na isipoacha kovu mzazi anatakiwa kumrejesha mtoto achomwe kwa upya mpaka itokee kovu, kuna uwezekano mzazi wako hakuzingatia hilo hivyo unaweza kuwa ulichomwa na kovu halikutokea na kuhurejeshwa kuchomwa tena....
ndui alama ya utanzania iyoNimekaa na makabila tofauti na hata kipindi nasoma tunaoga pamoja kila ninaemwangalia mkononi lazima awe na kovu la ile sindano ya ndui begani je,hivi ni sheria au huwa inatokea tuu kwa kila anaechomwa hii sindano.
Asantee, huo ugonjwa upoje haswaa kiongozi?Bado ipo. Hiyo chanjo imeuangamiza kabisa ugonjwa wa Ndui ambao ulikuwa tishio sana.
Mnamo mwanzoni mwa miaka ya 1700, mji wa Boston, Massachusetts kama ilivyokuwa kwa dunia nzima kipindi hiko, ulikumbwa na ugonjwa mbaya wa Ndui uliosababisha vifo vya watu wengi. Inakadiliwa watu zaidi ya milioni 300 walifariki kwa ugonjwa wa Ndui duniani kote.Asantee, huo ugonjwa upoje haswaa kiongozi?
Leo hii, zaidi ya miaka 300 baadae, tiba na teknolojia ya chanjo imepiga hatua kubwa ambapo magonjwa kama Surua na Polio ni magonjwa yanayokaribia kutokomezwa kabisa katika uso wa dunia.
Chanjo ni dawa ya kibaologia ambapo kipande cha ugonjwa au ugonjwa uliofubazwa uingizwa kwenye mwili wa binadamu kama namna ya kujenga kumbukumbu kwenye kinga ya mwili dhidi ya ugonjwa fulani.
Duh Kumbe Waafrika ndio walianza kutumia chanjo ya ndui kabla ya wengine.Mnamo mwanzoni mwa miaka ya 1700, mji wa Boston, Massachusetts kama ilivyokuwa kwa dunia nzima kipindi hiko, ulikumbwa na ugonjwa mbaya wa Ndui uliosababisha vifo vya watu wengi. Inakadiliwa watu zaidi ya milioni 300 walifariki kwa ugonjwa wa Ndui duniani kote.
Ugonjwa wa Ndui kipindi hiko ulikuwa kama hukumu ya kifo kwa waliougua na hata wagonjwa wachache waliopona waliachwa na makovu na vilema kwenye miili yao.
Lakini mnamo mwaka 1716, mtumwa wa kiafrika aitwaye Onesimus alimwambia mmiliki wake, bwana Cotton Mather, kuwa anafahamu siri ya ugonjwa wa Ndui. Onesimus alieleza kuwa alipokuwa Afrika alifanyiwa upasuaji mdogo na kupewa sehemu ya ugonjwa kwenye mwili wake na hivyo kumsababishia kinga dhidi ya kuugua tena ugonjwa huo.
![]()
Upasuaji huo mdogo ulijumisha kusuguliwa juu ya ngozi kwa maji maji kutoka kwenye vidonda vya mgonjwa wa Ndui na hivyo kumfanya kuwa na kinga ya ugonjwa huo.
Mather, alishangazwa na simulizi hiyo ambapo ilimbidi kufanya uchunguzi kwa watumwa wengine wa kiafrika ambao pia walimthibitishia juu ya ukweli wa tiba hiyo. Simulizi ya tiba hii kutoka kwa mtumwa wa kiafrika haikupata ushawishi mkubwa kwenye jamii ya watu weupe ila Mather aliendelea kuhubiri juu ya teknolojia hii.
Mnamo mwaka 1721, Mather pamoja na daktari mzungu Boylston Zabdiel walifanikiwa kujaribu teknolojia hiyo kwa mara ya kwanza ambapo walianza na mtoto wa Mather na baadhi ya wakazi wa Boston. Tiba hiyo ilionyesha mafanikio makubwa sana kwani kati ya watu 242 waliopata tiba hiyo ya chanjo ni watu 6 tu waliofariki kwa ugonjwa wa Ndui ikilinganisha na uwiano wa vifo 7 kwa kila wagonjwa 40 bila ya chanjo.
Mwaka 1796. Edward Jenner alifanikiwa kutengeneza chanjo ya kwanza rasmi kutokana na kirusi cha Ndui wa ng’ombe na hatimaye chanjo ya Ndui ikawa ni ya lazima kwa wakazi wote wa Boston, Massachussets.
Kutokana na mafanikio hayo na maboresho mbalimbali, mwaka 1980, shirika la afya duniani WHO walitangaza kuwa ugonjwa wa Ndui umetokomezwa rasmi katika uso wa Dunia.
Mwaka 2016, Onesimus alipewa heshima ya mtu bora wa wakati wote kwenye mji wa Boston. Mengi hayasemwi juu ya kifo cha Onesimus ila alifanikiwa kununua uhuru wake mwenyewe kwa kumlipa mmiliki wake kiasi sawa cha kuweza kununua mtumwa mwingine.
Leo hii, zaidi ya miaka 300 baadae, tiba na teknolojia ya chanjo imepiga hatua kubwa ambapo magonjwa kama Surua na Polio ni magonjwa yanayokaribia kutokomezwa kabisa katika uso wa dunia.
Chanjo ni dawa ya kibaologia ambapo kipande cha ugonjwa au ugonjwa uliofubazwa uingizwa kwenye mwili wa binadamu kama namna ya kujenga kumbukumbu kwenye kinga ya mwili dhidi ya ugonjwa fulani.
Shida yangu NI kwanini waliamua kuchanja wtz wote sehemu moja, mbona mataifa mengine hawana hii alama?Ndui ni smallpox, chanjo yake huwa ukichomwa panavimba na kutengeneza lengelenge (blister) ambalo likikauka huacha kovu. Ndio hiyo alama ya ndui.
Yes ni lazima kuchoma, kuna magonjwa ambayo yalisumbua miaka ya nyuma na kuua watu wengi sana duniani lakini baada ya kupatiwa chanjo ni lazima kila kichanga achomwe. Mfano hiyo smallpox, chickenpox, polio n.k
Ukiona wamama wanapeleka vichanga vyao clinic moja ya sababu ni kuenda kuchomwa hizo chanjo.