Hivi ni lazima tunaosafiri kwenda Mkoani Mara tupite Mkoani Mwanza? Hakuna Chocho lingine la kufika haraka?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
ONYO

Ukijijua Wewe ni Mhaya, Mnyaturu, Muha, Mnyiramba, Mrangi, Mkerewe na Mnyamwezi tafadhali kaa mbali na huu Uzi kwani nina uhakika kwa Ushamba wenu mkubwa hakuna mnachokijua na wote huwa hamna Ratiba za Kusafiri kutokana na kutokuwa na Pesa kama tulizonazo Watu wa Mkoa wa Mara ( Musoma ) wenye Maendeleo makubwa kuliko hiyo Mikoa yenu Duni.

Watani mpooooooo.......!!!!

Wengine karibuni katika Kuchangia.
 
Hope ni kutokea dar popote utakapopita ni lazima ufike usiku au kesho kabisa mfano ni Arusha Serengeti mara au Dar Arusha Nairobi Sirari napo parefu Ile safari ni kipengele nadhani ukipita hapo kwa wasingida ndio inakuwa rahisi zaidi
 
Wengine wanapitiaga Arusha huko mto wa mbu.. Pia naskia lipo chocho la nje mitaa ya Shinyanga kama sio Tabora unatokea karibu serengeti
Kama anatokea Dar hakuna nafuu yoyote kwake. Bora apitie njia ya Dar kwasababu hiyo ya Arusha kimeo. Hataweza kupita getini Ngorongoro kwasababu atafika pale ishakuwa usiku. Popoma kama anataka kuwahi apande tu ndege.
 
Kwa kutokea Shinyanga kuna njia ya Mwigumbi, Maswa hadi bariadi then unatokezea Lamadi unaunga hadi Mara.

Kutokea Singida kuna chocho inapita kwenye pori la kijereshi hadi bariadi. Kutokea Arusha unapitia Serengeti. Kutokea Kagera au geita panda mtumbwi ukupeleke Mara direct.
 
Hope ni kutokea dar popote utakapopita ni lazima ufike usiku au kesho kabisa mfano ni Arusha Serengeti mara au Dar Arusha Nairobi Sirari napo parefu Ile safari ni kipengele nadhani ukipita hapo kwa wasingida ndio inakuwa rahisi zaidi
Mwaka 2000 nilipita hiyo njia ya kupita Namanga Kenya kisha kuvuka Migori na kuingia Sirali Tanzania na kufika Kijijini Uzanakini nikiwa Hoi na sikuipenda tena na niliporejea Mkoani Dar es Salaam nilipata Lifti ya Ndege ya Jeshi iliyokuwa ikimbeba CDF Mstaafu Jenerali David Bugozi Musuguri kutoka Mkoani Mara kuja Kutibiwa Lugalo Military Hospital na Kuichukia kabisa hiyo Ruti ya Tanzania - Kenya - Tanzania.
 
Washa chombo saa 10 usiku then ondoka Dar kupitia bagamoyo, korogwe, Arusha, mto wa Mbu, Ngorongoro, Fort Ikoma gate, Serengeti hapo utaamua kuingia njia ya Mugumu - Tarime au Ikizu nyamuswa then unastop Butihama kuweka maua kwenye kaburi la Father of Nation kisha unaitafuta makutano mbele kidogo kwa mbali unaliona Ziwa Victoria.

Musoma hiyo hapo.
 
Kumbe umewahi kupanda ndege!
 
Kama anatokea Dar hakuna nafuu yoyote kwake. Bora apitie njia ya Dar kwasababu hiyo ya Arusha kimeo. Hataweza kupita getini Ngorongoro kwasababu atafika pale ishakuwa usiku. Popoma kama anataka kuwahi apande tu ndege.
Acha Bangi hiyo Nauli ya Ndege niitoe wapi? Kwa Uzi huu najua nitacheka mno kwa Comments zenu hasa nyie Wapuuzi Watani zangu niliowachokoza kwa Makusudi hapo juu.
 
Ipo Njia ya Arusha lakini unatakiwa uwe na gari ngumu na sio hizi mayai mayai.

Lakini pia kama unajiweza unaweza pita Nchi jirani ya Kenya hii inaitwa boda to boda utaenda kutokeza boda ya Sirali.

Haya kila la kheri.
 
Washa chombo saa 10 usiku then ondoka Dar kupitia bagamoyo, korogwe, Arusha, mto wa Mbu, Ngorongoro, Fort Ikoma gate, Serengeti hapo utaamua kuingia njia ya Mugumu - Tarime au Ikizu nyamuswa then unastop Butihama kuweka maua kwenye kaburi la Father of Nation kisha unaitafuta makutano mbele kidogo kwa mbali unaliona Ziwa Victoria.

Musoma hiyo hapo.
Asante kwa huu Mwongozo wako Mkuu ila umenifanya nicheke sana kwa huu mtiririko wako wa Kimaelezo.
 
Back
Top Bottom