Hivi ni lazima tunaosafiri kwenda Mkoani Mara tupite Mkoani Mwanza? Hakuna Chocho lingine la kufika haraka?

Hivi ni lazima tunaosafiri kwenda Mkoani Mara tupite Mkoani Mwanza? Hakuna Chocho lingine la kufika haraka?

Napanga kwenda Kijijini Uzanakini Kutambika ama mwaka huu au mwakani au hata Mwaka Keshokutwa hivyo najiandaa taratibu na Njia za Kupita.
1. Dar- Arusha pumzika, pita njia ya Longido - Oldonyolengai- Wasso - Soitisambu- Klein's gate- Mugumu- Ikizu-Butiama.
2. Dar- Arusha pumzika, pita Karatu- Mbulu-Mkalama- Sibiti- Meatu- Bariadi- Lamadi Bunda-Ikizu-Butiama.
3.Dar-Arusha pumzika, pita Karatu-Ngorongoro-Serengeti- Ikoma Ikizu-Butiama.
Gari liwe imara 4WD na tairi zinazohimili mikiki, (Rough road)Mf: Land cruiser H/Top, Nissan patrol, Land Rover defender usijaribu huko Range Rover sport, Kluger, Rav 4, Harrier utaliacha huko njiani.
4. Njia nyingine Dar- Singida pumzika-Singida -Shinyanga - Maswa -lamadi -Bunda-Butiama, Gari lolote utafika Barabara ni nzuri (Lami).
SAFARI NJEMA MKUU.
 
Back
Top Bottom