Hivi ni lazima tunaosafiri kwenda Mkoani Mara tupite Mkoani Mwanza? Hakuna Chocho lingine la kufika haraka?

Hivi ni lazima tunaosafiri kwenda Mkoani Mara tupite Mkoani Mwanza? Hakuna Chocho lingine la kufika haraka?

Kwa kutokea Shinyanga kuna njia ya Mwigumbi, Maswa hadi bariadi then unatokezea Lamadi unaunga hadi Mara.

Kutokea Singida kuna chocho inapita kwenye pori la kijereshi hadi bariadi. Kutokea Arusha unapitia Serengeti. Kutokea Kagera au geita panda mtumbwi ukupeleke Mara direct.
Simiyu
 
Ile njia ya Arusha kama unatoka Dar unakata Chalinze Tanga vijijini moshi afu Arusha Babati utakuta njia panda ya mara unafika
Babati!?.Moshi.... Arusha,Makuyuni,Mto Mbu ,Karatu...Serengeti!
 
Mind you Genta.
Njia ya kupita Nyamswa, Mugumu Serengeti kuja kutokea Arusha hakikisha unamwenyeji au usafiri Mchana. Unaweza kupotea humo hifadhini ukazurura mpaka tenki la mafuta likasoma E.
Jamani zivumilieni Mbavu zangu kwani Nacheka mno kwa hizi Comments zenu.
 
Mwaka 2000 nilipita hiyo njia ya kupita Namanga Kenya kisha kuvuka Migori na kuingia Sirali Tanzania na kufika Kijijini Uzanakini nikiwa Hoi na sikuipenda tena na niliporejea Mkoani Dar es Salaam nilipata Lifti ya Ndege ya Jeshi iliyokuwa ikimbeba CDF Mstaafu Jenerali David Bugozi Musuguri kutoka Mkoani Mara kuja Kutibiwa Lugalo Military Hospital na Kuichukia kabisa hiyo Ruti ya Tanzania - Kenya - Tanzania.
Ile safari Agana na nyonga si mchezo hapo kama sio ndge hakuna nafuu route pekee nafuu ni hii ya Kanda ya kati fanya kama unatembea ukifika mwanza unapumzika kesho yake unamalizia safari
Fast jet alisaidia sana air Tanzania huwa siwaelewi kabisa hata wanafanya Nini cancel nyingi sana
 
Mwaka 2000 nilipita hiyo njia ya kupita Namanga Kenya kisha kuvuka Migori na kuingia Sirali Tanzania na kufika Kijijini Uzanakini nikiwa Hoi na sikuipenda tena na niliporejea Mkoani Dar es Salaam nilipata Lifti ya Ndege ya Jeshi iliyokuwa ikimbeba CDF Mstaafu Jenerali David Bugozi Musuguri kutoka Mkoani Mara kuja Kutibiwa Lugalo Military Hospital na Kuichukia kabisa hiyo Ruti ya Tanzania - Kenya - Tanzania.
Hahaha mwaka huo nami nilimtembelea Msuguri na kuoga kwenye bwawa lake pale nyumbani kwake nadhani anaendeleza ule ufugaji
 
Hahaha mwaka huo nami nilimtembelea Msuguri na kuoga kwenye bwawa lake pale nyumbani kwake nadhani anaendeleza ule ufugaji
Wake zake Wadogo na baadhi ya Watoto wake wanauendeleza pamoja na kufanya Kilimo pia ambacho Mzee Musuguri alikipenda na anakipenda kwani ndicho Kimekomboa Nduguze wengi pale Kijijini Butiama kwa Biashara na Chakula cha Nyumbani.
 
ONYO

Ukijijua Wewe ni Mhaya, Mnyaturu, Muha, Mnyiramba, Mrangi, Mkerewe na Mnyamwezi tafadhali kaa mbali na huu Uzi kwani nina uhakika kwa Ushamba wenu mkubwa hakuna mnachokijua na wote huwa hamna Ratiba za Kusafiri kutokana na kutokuwa na Pesa kama tulizonazo Watu wa Mkoa wa Mara ( Musoma ) wenye Maendeleo makubwa kuliko hiyo Mikoa yenu Duni.

Watani mpooooooo.......!!!!

Wengine karibuni katika Kuchangia.
Dar - Arusha- Serengeti- Mara.

Dar- Bariadi, Simiyu- Bunda- Musoma.

Dar- Mwanza- Musoma
 
ONYO

Ukijijua Wewe ni Mhaya, Mnyaturu, Muha, Mnyiramba, Mrangi, Mkerewe na Mnyamwezi tafadhali kaa mbali na huu Uzi kwani nina uhakika kwa Ushamba wenu mkubwa hakuna mnachokijua na wote huwa hamna Ratiba za Kusafiri kutokana na kutokuwa na Pesa kama tulizonazo Watu wa Mkoa wa Mara ( Musoma ) wenye Maendeleo makubwa kuliko hiyo Mikoa yenu Duni.

Watani mpooooooo.......!!!!

Wengine karibuni katika Kuchangia.
Shinyanga - mwigumbi - Bariadi - Lamadi - Bunda - nk haipiti Mwanza.
 
Kweli nilisahau kuandika kutokea wapi. Ni kutokea Mkoani Dar es Salaam Mkuu.
We popoma,panda Capricon Ya Musoma ikifika shinyanga kuna short cut ya kutokea Bariadi bila kufika Mwanza. Lakini siku hizi gari za Musoma zipo mpya akina Abood,Happy Nation na Johanvia. Jana niliona ofisi za Ally's Star nao naona wamekuja pia. Wakati nakuja Musoma mara ya kwanza niliona kuna fusra sana kwenye sekta ya usafiri wa mabus kwa route ya Dar. Naona hawa wenye mabus nao wamepata hiyo akili maana bus zimemiminika kwa haraka sana ndani ya muda mfupi.
 
Popoma hii njia ya Arusha ni ndefu sana bora ya Dar - Mwanza - Musoma.
Ya Arusha sio ndefu, sema ni mbaya, lami hakuna across the Serengeti

Ya Arusha Kilomita 1166,
Ya Kati Kilomita 1,344

NORTHEN CORRIDOR.PNG

Ya Kati Kilomita 1344

CENTRAL CORRIDOR.PNG
 
Wakati was utawala was Magufuli nilisikia meneja wa tanrod akizungumzia Kuna njia inasubiri daraja kujengwa Singida kwa mbele ambayo itapunguza km 600 Hadi Mara ;lakini mpaka Sasa sijasikia chochote
 
Back
Top Bottom