Acha ubishi kwa Mambo ambayo tayari yapo kwenye Sheria.
Umewahi kusikia kuwa kuna chama cha waimbaji duniani? Sasa hao kina Diamond wanasimamiwa na nani Duniani?
Unajua kwanini Raisi hana mamlaka wala Jeuri ya Kumtengua Raisi wa TFF?
Kwaulize Cameroon na Sudan Serikali ilipoingilia Football, walipigwa Ban kushiriki mashindano yote ya Kimataifa kuanzia Club bingwa Afrika, Shirikisho, AFCON, CHAN, WORLD CUP na International friendly zote zilizopo kwenye Ratiba ya FIFA.
Na Ligi Kuu yenu haitotambuliwi na washindi hawatoshiriki mashindano ya Kimataifa.
Jaribu kufuatilia ndugu FIFA kwenye sheria zake ni Marufuku kwa Serikali yoyote kuingilia mpira wa Miguu. Hao kina Diamond na Wacheza Rede hawana Vyama vya kimataifa vinavyowasimamia wala hawana Sheria na Kanuni yoyote inayowaongoza ndiyomana hata Bongo Movie haina Kanuni yoyote zaidi ya kukokotwa na BASATA wakaishia kuimba mapambio.
Lakini FIFA wana sheria zao za kimataifa tena zina nguvu kuliko unavyodhani ndiyomana wanaweza kuishusha Daraja Timu yoyote na Nchi yoyote ile.
Unakumbuka Sakata la MORRISON? Mwakembe aliufyata na kuishia kulalamika kwa Maredio na TV tu lakini hakuthubutu kutia neno na Uwaziri wake.