Hivi ni nani alileta huu usafiri wa boda boda Tz?

Usininukuu vibaya, nimesema boda boda na sio piki piki kwaajili ya matumizi binafsi.
Mkuu nikitoka na pikipiki natumia mafuta ya elfu 5 naenda na kurudi ofisini ila nikitoka na gari ninatumia 20k ya mafuta plus muda mrefu sababu ya folen najikuta inabidi kuamka mapema zaidi kuliko nikiwa na pikipiki.
 
Uchumi nchi hauwezi kukua..
Sababu nachofahamu uchumi wa nchi hukua kutokana na production ya bidhaa, ambazo pia huwa exported, sasa kama jamii ni watumiaji sana na wanazalisha kidogo kama kwetu hapa uchumi hauwezi kukua
Asantee sana kwanini sasa serikali yetu isiweke juhudi katika kuziondoa kabisa hizo boda boda ili nguvu kazi ya vijana ikatumike kuzalisha badala ya kukaa vijiweni wakisubiri abiria.
 
Mm ni tajiri sana, mazingira niliyopo huwa sisikii kelele za usafiri wa waliofeli maisha kama ulivyowaita, hivi huwa wana kelele? 🤣
Sio kelele bali wana fujo sana huko barabarani. Kama una chombo cha usafiri utakubaliana nami hawa boda boda ni kero sana.
 
Unajaribu kujionesha uko vizuri kimaisha ila unaakili za kimasikini.
Ukitumia akili vizuri utaelewa point yangu kuwa boda boda ni janga kwa taifa letu haswa vijana. Uchumi kamwe hauwezi kukua kwa kuwa na waendesha boda boda lukuki! Huoni uzalishaji umepungua?
 
Sio kelele bali wana fujo sana huko barabarani. Kama una chombo cha usafiri utakubaliana nami hawa boda boda ni kero sana.
Okey, Lakini huu si uhalali wa kusema ni usafiri wa waliofeli maisha maana hata wewe unaweza utumia, na kama upo mjini basi lazima kuna namna umeutumia ww, ndugu,mzazi au rafiki.
 
Ni kimbilio la mwisho na huo ndio ukweli kwasababu hakuna mtoto anaesoma anasema akikua anataka kuwa dereva boda boda!
 
Tatizo ni kwamba unakidhihaki usichokijua jombaa.
Hawa watu unaowabatiza jina la failures ndio watu pekee wanaozijua siri za wake za watu na michepuko yao.
Wenye nafasi ya kuombwa na kubembelezwa kwa upole(mapatano ya nauli) na binti au mwanamke yeyoye ambae ww huwezi ukamsimamisha na akasimama ama kuongea nae pia kukaa nae zero distance.
Ni moja kati ya kundi linaloongoza kwa kuingiza pesa kila siku aingiapo kazini. (Hakuna mwisho wa mwezi)
Ndio kada pekee yenye wasomi wa kila aina na ni wengi.
Ndio kazi ambayo kila mtu ana adui humo....kama hamli mkeo basi mtoto wako au mtoto wa ndugu yako.
Ni kundi kinalowasaidia sana madaktari wetu kupata uzoefu wa kazi yao haswa mifupa.
Ndo dereva pekee anayeweza kukufikisha kwenye fumanizi kwa wakati na ukafanikiwa. (Straight)
Ni kundi moja wapo lisilotesa akili katika kupanga bajeti katika matumizi ya pesa.
 
🤣 Fumbo mfumbie mjinga mwerevu huling'amua. Nimekuelewa mkuu
 
Ukitumia akili vizuri utaelewa point yangu kuwa boda boda ni janga kwa taifa letu haswa vijana. Uchumi kamwe hauwezi kukua kwa kuwa na waendesha boda boda lukuki! Huoni uzalishaji umepungua?
Hakuna point hapo, toka huko ulipopewa kazi ya mchongo njoo mtaani utafute kazi hata ya kuosha vyombo utajifunza kitu.

Fikiria Ajira hakuna ( serikali/ sekta binafsi, hawana uwezo wa kuwaajili wote), Vijana hawana mitaji ya kufanya biashara kubwa, hawa vijana hawakopesheki, huo uzalishaji unaousema wataufanya kwa miujiza???
 
Ni kimbilio la mwisho na huo ndio ukweli kwasababu hakuna mtoto anaesoma anasema akikua anataka kuwa dereva boda boda!
Hakuna anayesoma anasema akikua anataka kuwa machinga, mchezaji wa bendi, mama ntilie, mfanyakazi wa ndani, youtuber na tiktok, mcheza sarakasi, mfyatua matofali, mzibua vyoo, mlinzi n.k lakini wapo wanahudumia jamii na wengine wanapita hapo na kufikia malengo.

Halafu haijalishi kuwa ni usafiri unaoutumia kama last obtion au first, as long as unautumia basi ni usafiri wenye umuhimu. Wafanyabiashara wakubwa wanakodi boda kuwahi ndege, madaktari wanakodi kumuwahi mgonjwa mwenye hali mbaya, huenda mama/baba au mwanao akapata tatizo boda boda ikamuwahisha kwenye utatuzi. Sijajua unatumia vigezo vipi kupima umuhimu wa shughuli za binadamu wengine kwenye maisha yako lakini binafsi, kila kazi inayohitajiwa na kupokelewa na jamii ina nafasi muhimu sana.
 
Hakuna point hapo, toka huko ulipopewa kazi ya mchongo njoo mtaani utafute kazi hata ya kuosha vyombo utajifunza kitu.

Fikiria Ajira hakuna ( serikali/ sekta binafsi, hawana uwezo wa kuwaajili wote), Vijana hawana mitaji ya kufanya biashara kubwa, hawa vijana hawakopesheki, huo uzalishaji unaousema wataufanya kwa miujiza???
Kwahyo huyo aliompa boda boda ya mkataba alishindwa kumpa mkopo wa biashara?
 
Habari za jioni, usiku, mchana na asubuhi. Nimekuwa nikijuiliza sana ni nani alileta huu usafiri wa boda boda, maana nikikumbuka miaka ya nyuma usafiri tegemezi ulikuwa ni dala dala, teksi na gana gana. Ila ghafla zikaibuka maboda boda ambao wamekua kero sana kila sehemu kwa kuendesha piki piki kwa fujo sana. Ni nani haswa alileta huu usafiri na je aliwahi tegemea ungekuja kuwa kero namna hii na ndio kimbilio la failures wote wa maisha?View attachment 2421389
Wahaya ( Watani zangu Wakubwa kutoka Mkoani Kagera ) kwani Historically Waanzilishi wa hii Huduma ni Uganda ( Waganda ) hivyo na Wahaya ( Watani zangu Wapendwa ) kutokana na kuwa nao Jirani nao waliwaiga na kuja Kuitambulisha na kuifanya huku Tanzania.

Nakumbuka mara yangu ya Kwanza Kuona Huduma hii ya Bodaboda huko Kampala, Masaka, Mbarara na Luweero nchini Uganda ni ndani ya Miaka yangu Sita ( 6 ) ya Kitaaluma ( 1996 - 2002 ) niliyokuwa huko na kwa Tanzania imeanza mwaka 2004 na Kurasimishwa rasmi na Serikali ya Rais Mstaafu Kikwete mwaka 2005 na tunayo hadi hii leo.
 
Kwahyo huyo aliompa boda boda ya mkataba alishindwa kumpa mkopo wa biashara?
Bodaboda ni biashara ndogo ya usafirishaji,

So mkopo wa bodoboda ni mkopo wa biashara wenye masharti nafuu.
 
Hakuna anayesoma anasema akikua anataka kuwa machinga, mchezaji wa bendi, mama ntilie, mfanyakazi wa ndani, youtuber na tiktok, mcheza sarakasi, mfyatua matofali, mzibua vyoo, mlinzi n.k lakini wapo wanahudumia jamii na wengine wanapita hapo na kufikia malengo.

Halafu haijalishi kuwa ni usafiri unaoutumia kama last obtion au first, as long as unautumia basi ni usafiri wenye umuhimu. Wafanyabiashara wakubwa wanakodi boda kuwahi ndege, madaktari wanakodi kumuwahi mgonjwa mwenye hali mbaya, huenda mama/baba au mwanao akapata tatizo boda boda ikamuwahisha kwenye utatuzi. Sijajua unatumia vigezo vipi kupima umuhimu wa shughuli za binadamu wengine kwenye maisha yako lakini binafsi, kila kazi inayohitajiwa na kupokelewa na jamii ina nafasi muhimu sana.
Sasa huoni wimbi la vijana wengi kimbilio lao limekuwa boda boda na bado mchango wao kwenye maendeleo ya taifa ni hafifu?
 
Labda Tuwawezeshe kwenye kilimo. Kinyume na hapo hatuna pa kuwapeleka.
 
Back
Top Bottom