Hivi ni nani anawadanganya watanzania kuwa lockdown haifanyi kazi? Hata kama tumeigomea, tuache kupotoshana!

Ajabu sana, wenye akili zao wamepiga lockdown, wametoa elimu na watu wameelimika na sasa wanaanza kufungua hizo lockdown kwa tahadhari kubwa sana, tunawaona hata kwenye supermarkets zao na maeneo mbalimbali walivyo na nidhamu ya hali ya juu (tunajipa moyo kwamba wanatuiga), upuuzi mtupu, sisi hakuna elimu iliyotolewa hata theluthi kulinganisha na kwao, zaidi tunaambiana tusitishane na huku watu wakiendelea kuteketea na kimdudu kikiendelea kusambaa, usipinge kwa kuwa halijakufika, na ukipinga likaja kukufika uje uunge mkono hoja usikae kimya kwa aibu, Lockdown ilitakiwa sana tu na siyo ya milele bali ya muda tu na elimu itolewe kwa kila njia, wale waliokuwa wakizika usiku wasambaze vipeperushi kutoa elimu namna ya kujikinga tukitoka, watu wangeogopa na wangeishi kwa tahadhari ya hali ya juu na ingesaidia sana kupunguza hofu iliyoko mtaani kwa sasa, kila mtu anamuogopa mwenzie, na wala kusingekuwa na mazishi ya usiku. Shule zimepigwa lockdown hakuna mishahara kwa walimu na wafanyakazi wengine wa shule, kwao tunaona ni sawa lokdaun ila kwenu nyinyi siyo sawa kwa sababu gani? Hakuna nchi hata jirani zetu aliyekufa kwa njaa, sisi tunakula sana ama vipi? Nimeagiza popcorns nyingine.
 
Asiyeamini ktk hili ni ubishi tu lakini ndio njia maridhawa ya kupunguza makali ya virusi popote duniani.
 
We umeshakufa or?
Hii ni brain kama ya anaekuongoza, inaonesha hupendi kabisa kitu kinaitwa strategy setting, crisis management and logistics ambapo namba au data zinahitajika sana kufanya analysis kabla ya kuchukua maamuzi.

Ukiwa na bahati mbaya ya kupata kiongozi asiyekuwa keen kwenye mambo hayo (lack of attentiveness to detail) lazima utapuuza hizo details na badala yake utaopt kwa waganga wa kienyeji maana huko hakuna namba wala matumizi ya akili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi hii haina Uwezo huo wa kuwagawia Raia chakula..... Hilo moja.

Pili.
Huwa kuna baadhi ya Maeneo huwa na njaa na Serikali hupeleka chakula cha msaada, I hope unajua Kile kinachotokea!
Nyie si mnasema Tanzania inalisha majirani wote? Iweje nyie mshindwe kuwalisha raia wenu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna nchi ambayo haitaabiki na corona Ulaya, lkn waliofanya lockdown hawako vizuri zaidi kuliko waliofanya ndicho nilichomaanisha, na kama una ushahidi kwamba Sweden imeathirika zaidi na corona kuliko nchi nyingine za Ulaya, karibu uweke hapa, ...
German wamefanya Lockdown na ni mfano wa kuigwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukishashiba unadhani kila mtu ni fisadi tajiri kama wewe!?

Kuna tunaobangaiza kutoka nje kila siku kwenda kutafuta huku na kule ili tusife njaa!

Wewe uko bize unaleta mifano ya ulaya! Bongo na ulaya wapi na wapi?

Hizo shule zenu za kata hazikuwafunza majedwali ya kuoanisha vinavyofanana?

Halafu, umezuiwa kujifungia? Kwanini usijifungie? Unataka kusindikizwa na kila mtu una ajenda gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania tuna shida kubwa sana yaani Kiongozi anasema yeye Uchumi kwake ndiyo priority namba moja swala maisha ya watu baadaye halafu kuna mazwazwa yanapiga makofi [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Tulinyimwa shule ili tushangilie kila kitu watakachosema watawala, usitulaumu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zambia zimepita wiki mbili bado wametufungia.

Ni hatua gani zinazotangazwa na serikali, kuendelea na mikusanyiko makanisani, misikitini, sokoni na kuwasifu wasiovaa barakoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa tafsiri sahihi ya lockdown

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani unavyo shupaa utadhani hauijui Tanzania...in Tanzania lockdown won't work bro and will never work
 

Mkuu hoja apa ni njaa

Serikali haina uwezo wa kuwapa at nusu kibaba cha dona wananchi wake kwa mwez mzima

Na ww unatakiwa utuambia hyo partial lockdown waliwafanyia nn wananchi wao!?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…