Mkuu
avogadro sometimes kama Hujui sheria inabidi ukae tu kimya usijiabishe mbele za watu...
Kuhusu Ndoa ya Watoto
Sheria ya Tanzania iliruhusu Mwanaume kumuoa mwanamke mwenye miaka 13 imebadilishwa nafikiri hata miaka 10 haifiki ikaongeza umri mpaka sasa ni miaka 15 Ruksa kuolewa au 14 kwa pendekezo la wazazi...
Soma sheria ya Ndoa 1971 kifungu cha 13(1) na (2)
Na kuhusu polygamy
Nakurudisha kwenye sheria hiyo hiyo ya ndoa sio kosa nenda kasome sheria hiyo kifungu cha 9 (3) na kifungu cha 10,Kinaeleza kuhusu aina za Ndoa Tanzania zimesema ni Monogamous na Polygamous... Na zimeelezea vizur kabisa nini maana zake na zinafungwaje nafikiri Go and read that..
Hata hivyo biblia yako pia iliruhusu ndoa hizo ukitaka ushahidi nitakuleta hapa nakuelimisha kwanza kuhus sheria
Kugandamiza haki za wanawake
Umesema kugandamiza haki na ukasema ikiwemo mojawapo kuwafunika manguo,kuwakataza kushirki katika utawala....
Sasa hapa siendi kwenye sheria ntaenda kwe ye bible yako..
Bible ndo kitabu cha kwanza kumgandamiza mwanamke mwanamke hakuhesabiwa kitu katika biblia..
- Unafahamu kuwa watoto wa Yakobo wako 13 mmoja ni mwanamke lakini kwakuwa tu ni mwanamke Hakuhesabiwa na unasikia wanakuambia kuna watoto 12 wa yakobo? Na makabila 12 ya israel je hilo kabila lake la huyo mwanamke kwanini halitajwi...kwa sababu biblia imekuwa kandamizi sana kuhusu mwanamke...
- Hakuna mtume wala nabii wa Kike aliyepewa heshima kwenye biblia..
- Wanawake walihesabiwa kama wazazi tu na sio watawala wa kiserkali wala kisiasa wala kidini...
Kuhusu kutawala umetoa hasira kabisa kwa waislamu..ngoja bhasi nilete ushaihidi kwamba nyote mko sawa...
Kuhusu kufunika kichwa
1 wakorintho 11:5-6,10,13,16
" Bali kila mwanamke asalipo, au anapohutubu, bila kufunika kichwa, yuaaibisha kichwa chake; kwa maana ni sawasawa na yule aliyenyolewa......
Maana mwanamke asipofunikwa na akatwe nywele. Au ikiwa ni aibu mwanamke kukatwa nywele zake au kunyolewa, na afunikwe.
Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani, kwa ajili ya malaika.Je! Inapendeza mwanamke amwombe Mungu asipofunikwa kichwa?
Lakini mtu ye yote akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi kama hiyo, wala makanisa ya Mungu."
kuwakataza katika utawala wanawake na kuwanyima priorit na kuwanyamazisha
1 Timotheo 2:11-14
"
Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna, Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu,
Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye, "Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa."
Pia unaweza ukapitia hapa
1 wakorintho 14:34-38
"
Wanawake na wanyamaze katika kanisa, maana hawana ruhusa kunena bali watii, kama vile inenavyo torati nayo.
Nao wakitaka kujifunza neno lo lote, na wawaulize waume zao wenyewe nyumbani mwao; maana ni aibu wanawake kunena katika kanisa.
Au je! Neno la Mungu lilitoka kwenu? Au kuwafikia ninyi peke yenu?
Mtu akijiona kuwa ni nabii au mtu wa rohoni, na ayatambue hayo ninayowaandikia, ya kwamba ni maagizo ya Bwana.
Lakini mtu akiwa mjinga, na awe mjinga..........
MY TAKE ON THIS
Mkuu dini zote hizi tatu zinafanana kimuuundo so usitukane nyingine ukadhani uko salama zote ziko sawa....
KUHUSU USTAARABU WA WAARABU..
wengi mmetukana sana kuhusu Ustaarabu wa waarabu bila kujali hata Mtume wenu Paulo,Alipopewa utume (kama anavyosema) kabla ya kwenda kukutana na wanafunzi wa Yesu alienda kwanza uarabuni na kupata ustaarabu wa Waarabu...
Soma wagalatia 1:16-18
"Alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu;
wala sikupanda kwenda Yerusalemu kwa hao waliokuwa mitume kabla yangu; bali nalikwenda zangu Uarabuni, kisha nikarudi tena Dameski.
Kisha, baada ya miaka mitatu, nalipanda kwenda Yerusalemu ili nionane na Kefa, nikakaa kwake siku kumi na tano."