Hivi ni rasimi sasa tuamini Mdude Kauliwa na watekaji?

Hivi ni rasimi sasa tuamini Mdude Kauliwa na watekaji?

mkulimamiwa

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2025
Posts
2,591
Reaction score
5,315
Kinachonipa nguvu, ni pale binadamu yeyote, masikini, tajiri, mwenye mamlaka n.k, woote lazima tuonje mauti

Shida inaanzia hapa!

Kuhukumu na kunyima watu uhai ni laana katika nchi, Damu ndio uhai wa mtu, na damu inapomwagwa kwa ukatili, hulia mbele za Mungu kwa kutaka kisasi juu ya nchi

Kwa nini utaratibu wa mtu kukamatwa na kisha kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, unapuuzwa?

Kwa nini mtekaji na mwamuzi wa uhai wa wengine, wewe unajihisi kwamba maisha yako ni shwaari kiasi kwamba kesho huna nayo taarifa na kwamba itakuwaje unapochukua maamzi ya kutoa uhai wa watu, Je watoto na familia yako iko salama kiasi gani?

Nyinyi wadhulumu uhai wa watu tena kwa ukatili wa hali ya juu, Vuta picha ya Mdude halafu fanya uwe ni wewe, ni halali utendewe unyama huo?

Na Je, Mdude alikuwa jambazi sugu kiasi cha kusithili adhabu hiyo?

Mdude amehatarisha maisha ya wengine kiasi cha kufikia hatua ya yeye kuuliwa?

Nakubaliana kabisa na hukumu ya kifo kwa mtu yeyote Gaidi, maana mtu aina hiyo, hana huruma ya maisha ya awaye yote

Je Mdude alikuwa Gaidi?

Kuna mahali nchi yangu haiko sawa wallah!
 
Hii shughuli inaonekana imeisha. Mbaya zaidi kwenye hili uwezekano wa familia kumzika mpendwa wao ni finyu sana.

Jamaa ni mtata ila sikubaliani na kuupoteza uhai wa mtu.
Ni kweli, Jamaa alikuwa mtata, lakini ni kweli alistahili kuuliwa?

mbona wengine tunaona wanashikwa na kupelekwa Jela, ilikuwaje kwa yeye?
 
Aliyetoa ruhusa ya kumuua Mdude Nyagali ni SAMIA SULUHU HASSAN

Huyu kahaba wa Kizanzibar ana roho mbaya mno!
 
Ukiweka list ya watu walionyanganywa uhai tukianzia kwa Mwendazake hadi huyu bi aingaya wanaweza fikia 200 na ushee wanaojulikana.

Hii ni hatari sana, kosa lao kubwa kupelekea kifo ni kuikosoa Serikali takatifu isiyo na dhambi haoa Duniani - Serikali ya chama sikivu cha mapinduzi.

Mdude kama wamekuua kweli basi pumzika kwa amani - hapa Duniani wote tunapita tu.
 
Kuhukumu na kunyima watu uhai ni laana katika nchi, Damu ndio uhai wa mtu, na damu inapomwagwa kwa ukatili, hulia mbele za Mungu kwa kutaka kisasi juu ya nchi

Kwa nini utaratibu wa mtu kukamatwa na kisha kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, unapuuzwa?

Kwa nini mtekaji na mwamuzi wa uhai wa wengine, wewe unajihisi kwamba maisha yako ni shwaari kiasi kwamba kesho huna nayo taarifa na kwamba itakuwaje unapochukua maamzi ya kutoa uhai wa watu, Je watoto na familia yako iko salama kiasi gani?

Ni wakati gani umewahi kufikiria juu yako wewe unapochukua uamzi wa kudulumu uhai wa wengine kwamba, ingelikuwa ni wewe ungefanya nini?

Je, Mdudu alikuwa jambazi lililoshindikana kiasi cha kuwa Gaidi?

Mdude amehatarisha maisha ya wengine kiasi cha kufikia hatua ya yeye kuuliwa?

Nakubaliana kabisa na hukumu ya kifo kwa mtu yeyote Gaidi, maana mtu aina hiyo, hana huruma ya maisha ya awaye yote

Je Mdude alikuwa Gaidi?

Kuna mahali nchi yangu haiko sawa wallah!
rasimi?
 
Back
Top Bottom