Kuhukumu na kunyima watu uhai ni laana katika nchi, Damu ndio uhai wa mtu, na damu inapomwagwa kwa ukatili, hulia mbele za Mungu kwa kutaka kisasi juu ya nchi
Kwa nini utaratibu wa mtu kukamatwa na kisha kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, unapuuzwa?
Kwa nini mtekaji na mwamuzi wa uhai wa wengine, wewe unajihisi kwamba maisha yako ni shwaari kiasi kwamba kesho huna nayo taarifa na kwamba itakuwaje unapochukua maamzi ya kutoa uhai wa watu, Je watoto na familia yako iko salama kiasi gani?
Ni wakati gani umewahi kufikiria juu yako wewe unapochukua uamzi wa kudulumu uhai wa wengine kwamba, ingelikuwa ni wewe ungefanya nini?
Je, Mdudu alikuwa jambazi lililoshindikana kiasi cha kuwa Gaidi?
Mdude amehatarisha maisha ya wengine kiasi cha kufikia hatua ya yeye kuuliwa?
Nakubaliana kabisa na hukumu ya kifo kwa mtu yeyote Gaidi, maana mtu aina hiyo, hana huruma ya maisha ya awaye yote
Je Mdude alikuwa Gaidi?
Kuna mahali nchi yangu haiko sawa wallah!