Hivi ni sahihi mwanamke unayemchumbia akikuuliza kazi unayofanya?

Namora

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
410
Reaction score
1,014
Wakuu habarini👋

Naomba kupewa maelekezo na walio kwenye ndoa au watu wenye uzoefu wa maswala haya.

Je, hivi ni sahihi mwanamke unayemchumbia awe mke wako kukuuliza kwamba unafanya kazi gani?

Kuna rafiki angu alikua kampenda binti kamfata hado kwao kwa maongezi zaid ya uchumba ili achukue jiko. Lakini katika kuulizana ulizana maswali yule binti akamuuliza jamaa kua anafanya kazi gani? Jamaa akajibu ila badae alijitafakari juu ya hilo swali ikabidi aachane uchumba na huyo binti. Atafute mwingine

Tumejaribu kumshauri rafiki zake kwamba aendelee kua nae ila kagoma. Anasema kwamba kwanini aulizwe kazi anayofanya? Anataka ajue kipato anachopata? Je, akishajua kipato anachopata si baadae anaweza akampotezea akipata mwanaume mwingine mwenye kazi na kipato kizuri zaidi? Jamaa anasema huyo dada atakua yupo after money na sio kujenga familia katika hali zote za maisha.

So wazoefu naombeni majibu je jamaa kafanya sahihi au sio sahihi. Na mwanamke alifanya vibaya au vizuri kumuuliza kipato chake?
 
Lazima mtu ajue aisee kama mhalifu unataka kuangushia mtu jumba bovu
 
Sidhani kama yuko tayari kwa ndoa huyo!

Kaswali kamoja tu hako ameshapaniki? Majadiliano ya haya mengine atayaweza? 👇👇👇

Ndoa, kama vile nyumba, inahitaji msingi imara. Na msingi imara unajengwa, mbali na mambo mengine, na kufahamiana vyema na kwa undani sana. Ndiyo maana watu wanashauriwa sana waanzie kwenye urafiki kwanza. Huyu jamaa ni wazi kuna hatua zimerukwa maana automatically mpaka kufikia uchumba binti na hata familia yake wanapaswa kuwa wanajua angalau mambo ya msingi ya mchumbiaji/muoaji ikiwemo kazi anayofanya.

Hawa hata wakioana watakuwa na matatizo maana hata tabia zao za kweli sidhani kama wanazifahamu. Labda dronedrake aje awaokoe 😁
 
Hivi unadhani wachumba wanaulizana maswali gani mkuu?
 
Kuulizwa swali ni jambo moja.. kutoa jibu sahihi ni jambo lingine.

Kazi inategemea na mtu na mtu, kuna kipindi fulani nilikuwa nafanya kazi fulani ambayo sikupenda watu wangu wa karibu waijue. So nilidanganya sana ila kuna muda unajisahau unaangusha ID mezani au unaropoka tu kitu ambacho ni very strange.. so muda ulivyo zidi kwenda wakagundua.

Mwanzo wa mahusiano inategemea unafanya kazi gani ila hakuna swali linalokosa majibu hasa maswali ya kupimana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…