Hivi ni Taasisi yetu tu au Taasisi zote za Umma pesa imekua ngumu kwa Wafanyakazi?

Ili nalo neno man. Nimekula leo x3 nimshukuru Mungu. Ingawa nilitamani nile vizuri zaidi, niende Century Cinemax kuangalia Movie, nnavotoka nitoke na Krussher ya kishua pale jirani ila ndio ivo.. Ngoja nilale kesho nikaumie tena.

Unaona sasa kumbe hata hauna mambo makubwa kiongozi. Kanuni yangu ni moja tu, kufurahia maisha kwa kiwango chochote kile katika hatua yoyote niliyonayo. Usikabidhi kabisa mtu mwingine jukumu la wewe kujipenda, jipende kwanza wewe.

Hata kama nna 50k mfukoni, weekend movie muhimu, nikipata na ka juice kwenye vile vimigahawa vya Mlimani City au kahawa moyo unaridhikaaaa.

Kesho mambo yasipoenda sawa itabidi tugawane upendo kiongozi weekend upate faraja ya movie kuongeza furaha na nguvu za kupambana. Tutagawana hicho hicho tutakachojaliwa. Umeleta andiko kwa machungu sana mkuu
 
Hahaha hiki kipindi kujispoil mtu unaogopa maana haujui kesho yako. Uwa najiuliza hii ofisi ndio itakayonitoa nitusue maisha au Mungu kanipangia pengine mi sijui?
 
Yap πŸ’― pesa haikimbizwi kabisa
Kama mkuu wa mkoa alivyosema inategwa

Haya maisha haya...au basi tu. Kuna kipindi nilipata upenyo wa kupata pesa kirahisi mno, ilikua ni maamuzi yangu tu kwamba nitengeneze kiasi gani kwa siku (Ilikua naweza kupata hadi 500k) ila nafsi ilikua inanisuta, ikabidi tu niwaambie wahusika kwamba kuna kitu hakipo sawa mahali. Ni kweli nilizikosa zile pesa lakini nna amani na furaha hadi kesho. Vinginevyo mngeshangaa tu The Monk amepotea jukwaani.

Ni vizuri sana kuwa na ndoto, jitihada, bidii, maarifa na kila aina ya ubunifu kwenye kutafuta pesa, ila hakikisha afya yako, furaha yako, amani yako na uhuru wako hauathiriki kwa namna yeyote ile, hapo sijaongelea heshima yako.
 
Hahaha hiki kipindi kujispoil mtu unaogopa maana haujui kesho yako. Uwa najiuliza hii ofisi ndio itakayonitoa nitusue maisha au Mungu kanipangia pengine mi sijui?

Mie napenda sana kujispoil hata kama kwa kiwango kidogo ila siwezi kujisahau mwiko. Endelea kujiuliza hayo maswali mkuu, mawazo mazuri ndio mwanzo wa matokeo mapya. Kila kitu kinaanza kwenye mawazo.
 
Ili nalo neno man. Nimekula leo x3 nimshukuru Mungu. Ingawa nilitamani nile vizuri zaidi, niende Century Cinemax kuangalia Movie, nnavotoka nitoke na Krussher ya kishua pale jirani ila ndio ivo.. Ngoja nilale kesho nikaumie tena.
Shida yako sio hela. Shida yako ni matumizi makubwa. Bajeti yako unapanga kwa kuangalia posho.
 
Kwani mishahara hamlipwi?
 
Hapo hatujaongelea magoli ya Mama!

Ila pesa haijawahi kutosha. Ogopa sana kitu kinachogombaniwa na Kila mtu. Unakipata Kwa tabu na dhoruba na usipokua makinibaada ya kukipata kinakuponyoka kama upepo.

How are you?
Hela ipo kwa wachache wale wakula kwa urefu wa kamba ila asilimia kubwa tubonga lugha moja ....maumivu

Niko poa wangu wewe je?
 
Hela ipo kwa wachache wale wakula kwa urefu wa kamba ila asilimia kubwa tubonga lugha moja ....maumivu

Niko poa wangu wewe je?

Kwahiyo sio tu kuwa na kamba, iwe ndefu pia. Kweli tusizeeke mapema?
Ila naweka mkono kifuani nabonga all is well, sitaaibika milele. Hata kama Kwa sasa hali ni ngumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…