Hivi ni ujinga, wivu au ni roho mbaya wanandoa waliotengana kuwazuia waliokua wenza wao kuwa na wenza wengine?

Lakini mahakama imeona kuna sababu zenye mashiko. Ushauri kwa wanaume wasizikimbie ndoa zao. Wakumbuke NDOA ni NDOANO.

Hivi talaka zinaruhusiwa siku hizi? mama D
Talaka zinaruhusiwa miaka yote, hakuna ndoa yoyote, narudia tena hakuna ndoa yoyote isiyokuwa na talaka.

Mahakama ndio chombo cha kisheria na kikatiba cha kuvunja ndoa.
 
Neno "uzinzi" hapo kwenye mathayo 5:23 lipo kimakosa hasa kwenye biblia za zamani, neno linalopaswa kuonekana hapo ni "maalimu" yaani ndoa ya ndugu wa damu yaani porneia.

Ni makosa ya watafsiri toka lugha asili ya icho kitabu kuja lugha yetu ya kiswahili ndio yaliofanyika, hivyo Yesu alitaka kumaanisha hakuna talaka kwa namna yeyote ile ipokuwa kama itagundulika walio-oana ni ndugu wa damu yaani maalimu, hapo ndoa ivunjwe na kila mmoja anakuwa huru kutafuta mwenza mwingine sio muoaji wala muolewaji.
 
Talaka zinaruhusiwa miaka yote, hakuna ndoa yoyote, narudia tena hakuna ndoa yoyote isiyokuwa na talaka.

Mahakama ndio chombo cha kisheria na kikatiba cha kuvunja ndoa.
Sheria ndizo zinaiongoza mahakama yoyote ile. Narudia tena, hakuna mahakama inayofanya maamuzi kama mwendawazimu bila kuzingatia sababu zenye mashiko.

Mfano, ndoa ya akina Halima Mdee ilipovunjwa (kinyemela?), now mahakama inataka kujiridhisha. Otherwise ingeweka muhuri wake na kuridhia hatua hiyo.
 
Ndoa inavunjwa na mahakama na siyo kanisani, hata mwanaume ana haki ya kuomba takaka mahakamani.
 
Hii ni Biblia yako wewe na tafsiri zako, na ndio sababu watu wengi wenye akili timamu wameshagunduwa hizi dini ni magubashi tu miradi ya sadaka.
 
Sijui kama hata unaelewa ulichokiandika.

Kazi ya bunge ni kutunga sheria, na kazi ya mahakama ni kutafsiri sheria na kutowa haki.
 
Hapa sijakuelewa umesema jack lazima apate tu, kwa vigezo gani? Walitafuta pamoja na mzee mengi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa wametengena siku nyingi sana. Huyu mama anamaanisha tangu walipotengana na mwenzake, baadaye hajawahi kuwa kwenye 'uhusiano' na mtu mwingine hata kama si uhusiano rasmi? Sababu ninavyoelewa biblia pia inatafsiri uzinzi wa mke ndio sababu ya kuachwa mke.
 
Kwenye maandiko sasa ila kimaatendo haya hayapo siku hizi. Mkishindwana talaka then kila mtu atafute ustaarabu wake
 
Talaka zinaruhusiwa miaka yote, hakuna ndoa yoyote, narudia tena hakuna ndoa yoyote isiyokuwa na talaka.

Mahakama ndio chombo cha kisheria na kikatiba cha kuvunja ndoa.
Kweli k1bisa, kanisa au BAKWATA etc hawawezi vunja ndoa. Infact ndoa za serikali
 


Mama D, kuwa makini unaposoma biblia andiko ulilonukuu ni Yesu anawa address wayahudi (those under the Mosaic law).

Sheria ya Musa inasema ni ruksa mtu kutoa hati ya talaka na kuoa/kuolewa tena.
Deuteronomy 24:1-2
1 Mtu akiisha kutwaa mke kwa kumwoa, asipopata kibali machoni mwake, kwa kuwa ameona neno ovu kwake, na amwandikie hati ya kumwacha, akamtilie mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake.
2 Naye akiisha kuondoka katika nyumba yake, ana ruhusa kwenda akawa mke wa mtu mwingine.

Kumbuka Yesu alikuja kuitimiliza sheria, kwa hiyo katika utimilifu wake ndipo akawaambia wayahudi;

Mathayo 5:32
Lakini mimi nawaambieni, anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, anamfanya azini; na mwanamume akimwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini.

Kumbuka pia baada ya sheria (torati) kutimilizwa, ilikuwa abolished. Yesu anawapa amri mpya ya upendo:

Yohana 13:33-34
33 Enyi watoto wadogo, bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; mtanitafuta; na kama vile nilivyowaambia Wayahudi ya kwamba, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja; kadhalika sasa nawaambia ninyi.
34 Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.

Mstari wa 33 hapo juu, Yesu anasisitiza kuwa sheria ilikuwa ni kwa ajili ya Wayahudi ili kuwaleta kwa Kristo, lakini hawakumkubali japo alikuja kuwakomboa kutoka kwny sheria, hivyo anawapa sheria mpya ya upendo wale walio mpokea (born again).

Jambo hili bado lilileta mgogoro hata hapo baadaye ndio maana Mtume Paulo analitolea tena ufafanunuza kwenye waraka wake wa kwanza kwa kanisa la korinto.

Kwa habari ya agano jipya (church age), muongozo ni huo wa Apostle Paul kwny kanisa la korinto i.e (1korint 7:10-11)

1 Corinthians 7:10-11
10 Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;
11 lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.

Ni katika msingi wa sheria mpya (upendo) ndipo suala la msamaha linaingia kutokana na upendo (agape/God kind of love)

1 Corinthians 13:4-5
4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;

Ndio maana unaruhusiwa kutoa talaka lkn huruhusiwi kuoa/kuolewa ili pale upendo utakapo tenda kazi yake ya kusamehe kwa kuwa hauhesabu maovu, hapo mnaweza rejea kwny ndoa upya.
 
Huyu bro anaonekana Upstair yupo vizuri sana, huyo mwanamke kinachoendelea hapo ni majuto ya kupoteza chuma kwa ujinga na upumbavu wake mwenyewe.!
 
Mama D, kuwa makini unaposoma biblia andiko ulilonukuu ni Yesu anawa address wayahudi (those under the Mosaic law).

Sheria ya Musa inasema ni ruksa mtu kutoa hati ya talaka na kuoa/kuolewa tena.
Deuteronomy 24:1-2

Tumetofautiana wapi🤗?

Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
 
Huyu bro anaonekana Upstair yupo vizuri sana, huyo mwanamke kinachoendelea hapo ni majuto ya kupoteza chuma kwa ujinga na upumbavu wake mwenyewe.!
Kweli inaonesha hivi sasa mwanamke anajuta hasa kwasababu sio mbunge tena kwahiyo mtonyo wa kumpa kiburi hakuna tena kama huyo bro anavyoeleza hapo. Unajua wanawake hawaoni mbali ndio sababu wanakuwa na viburi ila kwenye maisha ndio kila kitu. Ona miaka 18 imepita leo ndio umuhimu wa mtu unaonekana wakati alishasonga na maisha yake.
 
...na viela ela vyake vya ubunge ukute alipata kijana akawa anafanya ile kitu kama ajira rasmi akili zikamruka akamuona mume wake wa ndani kama ng'ombe sababu alipata vyote alivyohitaji (Pesa, mavazi na mapenzi) bila ya uwepo wake asijue muda ni mwalimu mzuri sana, inapoelekea ataanza kuokota makopo na akili zinaweza kumruka zote muda wowote sababu zimeanza kumruka kidogokidogo.
 
Tumetofautiana wapi[emoji847]?

Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
Nadhani tofauti yetu ilikuwa hapo kwenye kuoa/kuolewa baada ya talaka. Huko juu umecomment na nadhani ndio msingi wa thread yako kuwa watu wakiachana (wakristo) hata biblia inaruhusu kuoa/kuolewa tena.

Labda kinacholeta pia mkanganyiko kwenye hizi ndoa ni suala la sheria ya serikali. Ndoa tunazofunga na hatimaye kupewa vyeti ni kwa mujibu wa sheria ya serikali. Kwa mujibu wa sheria, mkitalikiana ni ruksa kuoa/kuolewa ila kikristo si jambo sahihi kwa mujibu wa maandiko km nilivyo eleza hapo juu.

Kwa kuwa ndoa ni 'mali' ya serikali kisheria, mkiachana hata ukioa/olewa hakuna shida kisheria ila changamoto itabaki upande wa imani (kikristo) ambayo nayo ni suala la imani ya wahusika, kwamba kwa kuoa/kuolewa tena mtakuwa mnatenda dhambi ya uzinzi.
 
Hii ni Biblia yako wewe na tafsiri zako, na ndio sababu watu wengi wenye akili timamu wameshagunduwa hizi dini ni magubashi tu miradi ya sadaka.
Kwaahiyo unataka kulazimisha ambacho unaona kwako ni rahisi ?, wewe sio wa kwanza walianza wayahudi wenyewe wa zama za musa na yesu.

Ugumu wa masuala ya ndoa hasa talaka hayajaanzia juzi wala leo. Mambo ya ndoa na talaka ni mambo yalioumiza kichwa tangu enzi za akina na musa mpaka yesu. Ndio maana hao wayahudi wa anzi za yesu baada ya kuona mambo ya kuishi na mke milele ni magumu sana mno wakataka wamlazimishe yesu (kama walivyo mlazimisha musa) alegeze kwa kuruhusu talaka kama mke akizingua, lakini Yesu bado alikaza kwa kupigilia msumari alichokiunganisha Mungu binadamu asikitenganishe, na kuwaongezea kuwa kwa ugumu wa mioyo yao walimlazimisha musa aruhusu talaka na sio takwa wala mpango wa Mungu tangu awali, ndio akakazia kuwa hakuna talaka isipokuwa kama waliooana itagundulika ni ndugu wa damu (greek bible imetumia neno porneia ambayo maana yake sio uznzi kama unavitaka kulazimisha, ila ni kama ndoa ya ndugu wa damu ivi, kwa kiswahili nafikiri ndio wanaita maalimu kama sijakosea)

Hivyo haijaanzia kwako wala leo haya mambo ya mke kuishi nae mpaka kifo chenu kuyaona magumu sana , yalikuwepo tangu musa na Yesu kiufupi hakuna kipya. Ndio maana badaa ya hiyo kauli ya Yesu kuhusu talaka petro alimwambia Yesu kama mambo ya ndoa ndio yalivyo (yaani hakuna kuachana mpaka kifo) ni asavali kuto-kuoa kabisa. Ndipo akijibiwa sio wote wanaliweza hilo.

Ugumu wako wa moyo na uzito ulionao wewe sio wa kwanza walikuwepo zaidi yako mpaka kuwasukuma manabii wageuza maneno ya vitabu vya maandiko kuhusu talaka.
 
Hawa viumbe huwa wanarudi mambo yao yakishakwama lakini unakuta walipomuacha mtu walimuacha kwa dharau. Hawajui huwezi kutokea dirishani ukabaki mshindi daima, kwasababu lazima update karma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…