Biblia inakataza kuachana isipokua kwa sababu ya zinaa.
Maachano yote yanakatazwa wala huruhusiwi kuoa au kuolewa tena.
Achano la kusababishwa na zinaa halijasema wewe uliyemwacha mzinzi ubaki hivyohivyo bila kuoa ila limesema atakayemuoa yule mzinzi uliyemwacha kwa talaka anazini. Kwahiyo adhabu ya mzinzi ni kutalikiwa na kubaki bila mwenza
Mathayo 5:32
Lakini mimi nawaambieni, anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, anamfanya azini; na mwanamume akimwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini.

Mama D, kuwa makini unaposoma biblia andiko ulilonukuu ni Yesu anawa address wayahudi (those under the Mosaic law).
Sheria ya Musa inasema ni ruksa mtu kutoa hati ya talaka na kuoa/kuolewa tena.
Deuteronomy 24:1-2
1 Mtu akiisha kutwaa mke kwa kumwoa, asipopata kibali machoni mwake, kwa kuwa ameona neno ovu kwake, na amwandikie hati ya kumwacha, akamtilie mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake.
2 Naye akiisha kuondoka katika nyumba yake, ana ruhusa kwenda akawa mke wa mtu mwingine.
Kumbuka Yesu alikuja kuitimiliza sheria, kwa hiyo katika utimilifu wake ndipo akawaambia wayahudi;
Mathayo 5:32
Lakini mimi nawaambieni, anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, anamfanya azini; na mwanamume akimwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini.
Kumbuka pia baada ya sheria (torati) kutimilizwa, ilikuwa abolished. Yesu anawapa amri mpya ya upendo:
Yohana 13:33-34
33 Enyi watoto wadogo, bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi; mtanitafuta; na kama vile nilivyowaambia Wayahudi ya kwamba, Mimi niendako ninyi hamwezi kuja; kadhalika sasa nawaambia ninyi.
34 Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.
Mstari wa 33 hapo juu, Yesu anasisitiza kuwa sheria ilikuwa ni kwa ajili ya Wayahudi ili kuwaleta kwa Kristo, lakini hawakumkubali japo alikuja kuwakomboa kutoka kwny sheria, hivyo anawapa sheria mpya ya upendo wale walio mpokea (born again).
Jambo hili bado lilileta mgogoro hata hapo baadaye ndio maana Mtume Paulo analitolea tena ufafanunuza kwenye waraka wake wa kwanza kwa kanisa la korinto.
Kwa habari ya agano jipya (church age), muongozo ni huo wa Apostle Paul kwny kanisa la korinto i.e (1korint 7:10-11)
1 Corinthians 7:10-11
10 Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;
11 lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.
Ni katika msingi wa sheria mpya (upendo) ndipo suala la msamaha linaingia kutokana na upendo (agape/God kind of love)
1 Corinthians 13:4-5
4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
Ndio maana unaruhusiwa kutoa talaka lkn huruhusiwi kuoa/kuolewa ili pale upendo utakapo tenda kazi yake ya kusamehe kwa kuwa hauhesabu maovu, hapo mnaweza rejea kwny ndoa upya.